STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 24, 2014

Yohan Cabaye ajiandaa kutwaa taji la pili la Ligi Ufaransa

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/01/31/article-2549777-1B1CA23300000578-208_634x471.jpgKIUNGO Yohan Cabaye nyota wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Ufaransa PSG, Yohan Cabaye anajiandaa kunyakua taji lake la pili la ligi hiyo iwapo timu yake hiyo itapata ushindi katika pambano lao dhidi ya Sochaux litakalochezwa Jumapili.
PSG imebakisha pointi tatu tu kutetea taji hilo baada ya jana kupata ushindi mwembamba dhidi ya Evian TG na kuzidi kuikimbia Monaco, wapinzani wao wa karibu waliopo nafasi ya pili na waliowaacha kwa pointi 10 huku ligi ikisaliwa na mechi nne kabla msimu haujafungwa.
Cabaye aliyesajiliwa kwenye usajili wa majira ya baridi akitokea Newcastle United ya Uingereza anasema atakuwa mwenye furaha iwapo PSG itatwaa taji hilo ambalo kwake itakuwa ni mara ya pili baada ya kunyakua mara ya kwanza mwaka 2011 akiwa na Lille.
Mkali huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Ufaransa, anasema angependa kuongeza medali nyingine ya dhahabu katika chumba chake kupitia PSG.
"Tuna hamu kubwa ya kupata mafanikio ya kunyakua taji hilo na kitu hicho ni muhimu sana kwangu," alisema Cabaye, 28 na kuongeza; "Itakuwa vyema kama nitanyakua ubingwa huo nikiwa na PSG."
Mwishoni mwa wiki Cabaye alifanikiwa kunyakua Kombe la Ligi wakati PSG ilipoicharaza Olympique Lyon mabao 2-1 kwa mabao la Edinson Cavani na kudai ingawa hajawahi kunyakua Kombe la Ligi au Kombe la Mfalme mara mbili, lakini katika ligi anaamini itafanikiwa na anajiandaa kushangilia furaha ya ushindi huo anaousubiri kwa hamu.

Sturridge arejea,, Chelsea ikipanga kupumzisha nyota wake

http://www3.pictures.zimbio.com/gi/Daniel+Sturridge+Liverpool+v+Fulham+Premier+HI6EojIbLKll.jpg
Daniel Sturridge
http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/03/06/article-2288964-09591184000005DC-339_306x423.jpg
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
 WAKATI kocha Jose Mourinho akidaiwa kutaka kuwapumzisha wachezaji wake nyota wake katika pambano lao la Ligi Kuu dhidi ya Chelsea ili kuitafutia kasi Atletico Madrid katika mechi ya nusu fainali ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wapinzani wao Liverpool wanachekelea kurejea kwa Daniel Sturridge.
Sturridge anategemewa kurejea kutoka katika majeruhi katika mchezo huo wa Jumapili ambao watakwaana na Chelsea.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye miaka 24 alikuwa akilalamika maumivu ya msuli katika ushindi wa mabao 3-2 waliopata dhidi ya Manchester City Aprili 13 hivyo kupelekea kutolewa nje. 
Toka apate majeruhi hayo alikosa mechi moja lakini sasa anategemewa kurejea tena uwanjani kuisaidia Liverpool katika mchezo huo muhimu ambao kama wakishinda utawafanya kuendelea kujikita kileleni hivyo kuweka hai matumaini yao ya ubingwa wa Ligi Kuu. 
Sturridge amesema kwa sasa anajisikia vyema na ni mategemeo yake atakuwepo katika mchezo huo wa Jumapili lakini itategemea kama kocha Brendan Rodgers atamchagua.
Katika hatua nyingine, Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amesema anataka kuwapumzisha nyota wake kwa ajili ya safari kwenda Anfield kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool Jumapili ijayo. 
Chelsea bado wako katika kinyang’anyiro cha taji la ligi wakiwa wamebakiwa na michezo mitatu lakini Mourinho anataka kuhamishia nguvu zake katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid. 
Katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa juzi, Chelsea iling'ang'aniwa na wenyeji wao Atletico kwa kutoka suluhu.
Hata hivyo, kocha huyo amesema uamuzi huyo wa kuwapumzisha baadhi ya nyota wake unaweza usiwe wa kwake kuufanya kwa sababu anataka kusikiliza na mawazo ya wengine. 
Kipigo cha mabao 2-1 walichopata Chelsea kutoka kwa Sunderland mwishoni mwa wiki iliyopita kinamaanisha hata kama wakishinda mchezo wa Anfield inaweza isitoshe kuizuia Liverpool kushinda taji la ligi baada ya kupita miaka 24.
Liverpool inaoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 80, huku wapinzani wao waliopo nafasi ya pili wana pointi 75 moja zaidi ya ilizonazo Manchester City iliyo na mchezo mmoja zaidi ya timu hizo mbili za juu zilizocheza mechi 35.

Bomu jingine lalipuka Kenya

MATUKIO  ya kigaidi yamekua yakichukua vichwa vya habari mara nyingi nchini Kenya hasa baada ya nchi hiyo kupeleka wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wanamgambo wa kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.
Saa tatu na nusu usiku wa April 23 2014  bomu jingine limelipuka ndani ya gari karibu na kituo cha Polisi Nairobi.
Waziri wa mambo ya ndani amethibitisha kwa kusema Polisi wawili wamepoteza maisha kati ya watu wanne ambao wameuwawa huku hao wengine wawili wakihofiwa kuwa ni Mahabusu waliokuwemo kwenye gari hilo na Polisi.

Mhe Temba, Chegge Waueni sasa!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0xQoDnodEV9YYagUy0z9ZP5UpB52s4xbJjVzKwckA9t_5NJAr8AiEwl5VLg4SNI0Eai2GGsmoYGrWg7xq_-dy-LFWWRWtAzTTh_YVzi9J0tS628PHayncwU1-X7JWpIpqp6zF5OQ5/s1600/Temba+and+Chege.jpgNYOTA wa muziki wa kizazi kipya wanaotoka kundi la TMK Wanaume Family, Chegge na Mhe Temba wanatarajia kuachia hewani wimbo wao mpya uitwao 'Waue' waliowashirikisha 'membaz' wa Mkubwa wa Wanawe.
Wasanii walioshirikishwa na wakali hao ni Maromboso na YP ambao nao wanatokea 'ukoo' wa TMK Wanaume Family na Mkubwa na Wanae.
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe na Meneja wa wasanii hao, Said Fella 'Mkubwa' aliiambia MICHARAZO kuwa, wimbo huo utaachiwa 'audio' na video wiki mbili zijazo baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.
Mkubwa, alisema wimbo huo umerekodiwa katika studio zao za Mkubwa na Wanae chini na mtayarishaji, Shirko na video imefanywa na Adam Juma kupitia kampuni yake ya Visual Lab.
"Wasanii Temba na Chegge wamekamilisha kurekodi 'audio' na video ya wimbo wao uitwao 'Waue' wallioimba na Maromboso na YP, na tunapanga kuachia kazi hizo kwa pamoja wiki ijayo," alisema.
Chegge na Mhe Temba wamekuwa wakitoa kazi za pamoja mbali na zile za binafsi za kila mmoja nje ya nyimbo za kundi lao la TMK Wanaume Family.

Mashauzi, Sikinde kuwasindikiza Talent Band

http://4.bp.blogspot.com/-O6fGijIG-Xg/TpazwGlqCXI/AAAAAAAAAIQ/RB1Z12Ke5k8/s320/Hussin+Jumbe
Hussein Jumbe 'Mtumishi'

http://api.ning.com/files/QB639EYNFoD4efIjz*tu6A-tokrUhXrM*zilTmqFjwPaPBf8MRFVKag*kDP98VUlJn2dEoatnVAzlwDEnsygi3UIFRYdWmh1/MITIKISIKOYAPWANIDARLIVE16.JPG?width=650
Ishi Mashauzi atakayemsindikiza Hussein Jumbe na Talent Band
KUNDI maarufu la muziki asilia la Ngoma Afrika na kundi la muziki wa taarab la Mashauzi Classic, yanatarajiwa kupamba uzinduzi wa albamu mpya ya Talent Band utakaofanyika wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MICHARAZO, Mkurugenzi wa Talent Band, Hussein Jumbe alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika Aprili 30 kwenye ukumbi maarufu Kisuma Night Park lililopo eneo la Temeke Mwembeyanga na watasindikizwa na makundi hayo mawili.
Jumbe alisema pia bendi yake ya zamani ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' watakuwepo ukumbini kumpiga tafu kwenye uzinduzi huo wa aina yake.
"Natarajia kufanya uzinduzi wa albamu ya bendi yetu ya Talent iitwayo 'Kiapo Mara Tatu' na makundi ya Mlimani Park, Mashauzi Classic na Ngoma Afrika watanisindikiza siku hiyo pale Mwembeyanga," alisema.
Jumbe alisema kuwa, maandalizi ya uzinduzi huo unaendelea vyema na kuwataka mashabiki wa muziki wa dansi kujitokeza kupata burudani ambayo wameikosa kwa muda mrefu jijini Dar es Salaam.

Arsenal yaingia mbio za kumwinda van Gaal

http://www.101greatgoals.com/wp-content/uploads/2014/04/Louis-Van-Gaal-Bayern-Mun-001.jpg
Kocha van Gaal
 KLABU ya Arsenal imedaiwa kufanya mawasiliano na kocha Louis van Gaal, anayetajwa kuchukua mikoba ya David Moyes aliyetimuliwa na klabu ya Manchester United juzi.
Duru za kispoti zinasema kuwa, Arsenal imelazimika kuwasiliana na Mholanzi huyo kutokana na kutokuwa na uhakika na mustakabaliwa wa kocha wake Arsene Wenger. 
Hata hivyo Arsenal bado ina matumaini kuwa Wenger atasaini mkataba mpya wa miaka miwili waliokubaliana Octoba mwaka jana, lakini inajulikana anaweza kujiuzulu kama akishindwa kufikia malengo aliyojiwekea baada ya kumalizika kwa msimu. 
Imebainika kuwa Mfaransa huyo aliwaambia marafiki zake kuwa anafikiria kuacha kuinoa Arsenal kama awatashinda Kombe la FA na kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu. 
Kutokana na hali hiyo kumekuwa na mipango ya muda mfupi inayofanywa na Arsenal, mojawapo ni kujaribu kufanya mazungumzo na Van Gaal ambaye mkataba wake na timu ya taifa ya Uholanzi unamalizika baada ya Kombe la Dunia.
Mbali na kuwindwa na Arsenal, kocha huyo pia amekuwa akitajwa kunyemelewa na klabu za Manchester United na Tottenham Hotspurs ambao nao wanataka achukue nafasi ya Tim Sherwood mwishoni mwa msimu huu.
Kocha huyo mwente rekodi za kuvutia amekuwa akiwania kutokana na uwezo wake wa kuwaongoza na kuwadhibiti wachezaji hata wale wakorofi. 

Januzaj aichagua Ubelgiji

http://i.huffpost.com/gen/1235023/thumbs/o-ADNAN-JANUZAJ-570.jpg?6
Januzaj
WINGA chipukizi wa klabu ya Manchester United, Adnan Januzaj ameamua kuiwakilisha Ubelgiji katika michuano ya soka ya kimataifa. 
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Marc Wilmots ametangaza katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter amefurahishwa na uamuzi uliochukuliwa na mchezaji huyo. 
Januzaj amezaliwa jijini Brussels akiwa na wazazi wenye asili ya Kosovo na Albania na kujiunga na United mwaka 2011. 
Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa na nafasi ya kuzichezea nchi za Kosovo, Albania, Turkey, Serbia na hata Uingereza lakini sasa anaweza kuwemo katika kikosi cha Ubelgiji kitakachoshiriki Kombe la Dunia. 
Kikosi kamili cha wachezaji 30 wa Ubelgiji kinatarajiwa kutajwa Mei 13 mwaka huu.

Kocha mpya Stars kutua nchini Jumamosi

http://www.clubofmozambique.com/pt/sectionnews/data/entretenimento/mart_nooij.jpg
Huyu ndiye kocha mpya wa Taifa Stars

 KOCHA Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26 mwaka huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.
Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkenya kuzihukumu Stars na Intamba Murugamba

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbouke40Ajpgip-WYtuNcSkslDTj7_vx1cW1lSk8TTr-VrfSpd48or2vfOoU95GSaeEPAw2h5x4McRiOOgSk6nbUS6SUXQKo3lzFQl3LThJA16UJsJRVH5TDtfBRQTKxdCPu8d59WboTi_/s400/waamuzi.jpg
Mwamuzi Ogwayo atakayezichezesha Stars na Intamba Murugamba
MWAMUZI Anthony Ogwayo mwenye beji ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa keshokutwa (Aprili 26 mwaka huu)  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ogwayo katika mechi hiyo ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, atasaidiwa na Gilbert Cheruiyot na Oliver Odhiambo wote pia kutoka Kenya. Mwamuzi wa mezani atakuwa Israel Mujuni wa Tanzania.
Burundi inatarajia kuwasili nchini leo (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways na itafanya mazoezi kesho (Aprili 25 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza tangu kuanza kwa mpango wa maboresho wa timu hiyo.
Makocha wa timu zote mbili pamoja na manahodha wao kesho (Aprili 25 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mechi hiyo.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.

Zawadi za washindi Ligi Kuu Tanzania Bara zatangazwa

* Amissi Tambwe kuzoa Mil 5.2
* Azam kama bingwa kunyakua Mil 75
Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Azam watakaozoa Mil 75
Tambwe wa Simba kajihakikishia Sh Mil 5.2
MSHAMBULIAJI Amisi Tambwe wa Simba atalamba Sh. milioni 5.2 za zawadi ya mfungaji bora zitakazotpolewa na wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kampuni ya huduma ya simu ya Vodacom Tanzania baada ya kuibuka mfungaji bora wa msimu wa 2013/14 wa ligi hiyo.

Aidha, timu yenye nidhamu italamba Sh. milioni 16 ikiwa ni ongezekon la Sh. milioni moja ikilinganishwa na ilivyokuwa msimu uliopita.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim katika mkutano na waandishi wa habari muda mfupi uliopita kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

ZAWADI ZA WASHINDI LIGI KUU BARA 2013/2014
Bingwa: Sh. Milioni 75
Mfungaji Bora: Sh. Milioni 5.2
Timu yenye Nidhamu; Sh. Milioni 16
Kipa Bora: Sh. Milioni 5.2
Refa Bora; Sh. milioni 5.2
  Mwalim amesema mabingwa Azam FC watazawadiwa Sh. milioni 75 ikiwa ni ongezeko la Sh. milioni 5 ikilinganishwa na ilivyokuwa msimu uliopita.   Kipa bora, mwamuzi bora watapata Sh. milioni 5.2 kila mmoja ikikwa ni ongezeko la Sh. 200,000.Timu yenye nidhamu italamba Sh. milioni 16, ikiongezeka kutoka Sh. 15 ya msimu uliopita zilizochukuliwa na Yanga.   Silas Mwakibinga, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), aliyekuwa amefuatana na Mwalim kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, alisema tarehe ya kutolewa kwa tuzo hizo itatangazwa baada ya wiki moja.

Kivumbi Europa League kutimka leo Juve yaifuata Benfica

Juve itavuna nini leo Ureno
KIVUMBI cha Nusu Fainali  ya Ligi Ndogo ya Ulaya (UEFA Europa League) kinatarajiwa kutimka usiku wa leo wakati timu nne zilizotinga hatua hiyozitakapopepetana kwenye viwaja viwili tofauti.
Klabu za Sevilla na Valencia zote kutokea Hispania zilizopangwa kucheza pamoja zitakutana kwa mara ya kwanza katika hatua hiyo, wakati mabingwa wa Italia Juventus watakwaruzana na Benfica ya Ureno katika mechi zinazotarajia kuwa na msisimko wa aina yake.
Valencia na Sevilla ambazo zilipindua matokeo yao ya awali walipolazwa ugenini na kushinda nyumbani kwa idadi kubwa ya mabao dhidi ya Porto na Basel zinakutana kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Ulaya.Mechi za mkondo wa kwanza baina ya timu hizo mbili itaanziua nyumbani kwa Sevilla kabla ya wiki ijayo kuwafuata wapinzani wao hao.
Timu zote mbili zimewahi kunyakua taji hilo kwa vipindi tofauti, Sevilla mara mbili mfululizo mwaka 2006 na 2007 na wenzao walitangulia mwaka 2004.
Juventus itakayokuwa ugenini ilishawahi kunyakua taji hilo mara tatu mwaka 1977, 1990 na 1993 na ingependa kufanya kweli katia michuano ya mwaka huu baada ya ndoto zao na kutamba Ligi ya Mabingwa Ulaya kukwama na kutolewa kwenye hatua ya 16 Bora.
Waitalia hao wanaoelekea kutetea taji lao la Seria watakutana na Benfica ambao hawajawahi kunyakua taji hilo la Europa, ingawa mkononi tayari wana taji la ligi kuu ya nchi yao ya Ureno.
Ikitamba na nyota wake kama Carlos Tevez, Andre Pirlo, Paul Pogba na wengine Juventus itahitaji ushindi ugenini ili mchi yao ya marudiano wilki ijayo iwe nyepesi ingawa watarajie kupata upinzani mkali kwa mabingwa hao wa Ureno inayotambia wakali wake kama Lima kutoka Brazil., Rodrigo, Cordozo, na Andre Gomes

Real Madrid yaizima Bayern Munich, ila kazi wanayo ugenini

Benzema (9) akishangiulia bao lake pekee lililoizamisha Bayern Munich
MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich imekubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa wenyeji wao Real Madrid katika mechi ya mkondo wa kwanza ya Nusu fainali ya pili ya michuano hiyo iliyochezwa usiku wa kuamkia leo mjini Madrid -Hispania.
Baoa pekee la dakika ya 19 ya mchezo lililotumbukizwa kimiani na Karim Benzema lililitosha kuwapa wenyeji ushindi huo mwembamba kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Katika mchezo huo ilishuhudiwa wachezaji ghali wa klabu ya Real Madrid wanaodaiwa kuwa wagonjwa kupishana katika kipindi cha pili na kuwapa faraja vijana wa Carlo Ancelotte kupumua kabla ya wiki ijayo kurudiana na Wajerumani hao waliopoteza bafasi kadhaa za kufunga katika mechi hiyo.
Real Madfrid itakabiliwa na kazi nzito katika mchezo wa marudiano ili kulinda ushindi huo na kuvuta unyonge wa kutolewa mara katika hatua hiyo na wapinzani wao hao.