STRIKA
USILIKOSE
Sunday, May 19, 2013
Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa atiwa mbaroni kisa...!
Warembo Miss Tabata 2013 kutembelea Mbuga ya Mikumi
Miss Tabata wakiwa kwenye pozi ya picha ya pamoja |
WAREMBO watakaoshiriki kinyang'anyiro cha shindano la Miss Tabata
2013 watatembelea mbuga ya wanyama ya
Mikumi wikiendi ijayo.
Mratibu wa shindano hilo
Godfrey Kalinga mapema leo kuwa, lengo la ziara hiyo ni kukuza utalii wa ndani.
Alisema kuwa warembo hao pia watapata fursa ya kujua vivutio vilivyomo kwenye
mbuga hiyo iliyoko mkoani Morogoro.
“Hii siyo mara yetu ya kwanza
kuwapeleka warembo wetu mbugani. Tumekuwa tukifanya kila mwaka,” alisema
Kalinga.
Kapinga alisema kuwa
ziara hiyo imedhaminiwa na CXC Africa.
Shindano la kumsaka Miss
Tabata litafanyika Mei 31 katika ukumbi
wa Da’ West Park, Tabata.
Wadhamini wa shindano
hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito
Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
Warembo watakaoshiriki
kwenye shindano hilo linaloandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts ni
Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19),
Kazunde Musa Kitereja (19), Rehema Kihinja (20), Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23),
Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na Suzan Daniel (18).
Warembo watano watachaguliwa
kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la
Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Simba na Yanga zaingiza Mil, 500, zenyewe zazoa Mil. 250
Simba na Yanga zilipoumana jana uwanja wa Taifa |
PAMBANO la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000.
Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.
Golden Bush Veterani yaendeleza ubabe Dar
Wakali wa soka la maveterani Dar, Golden Bush |
Timu hiyo ilipata ushindi katika michezo ya Bonanza iliyofanyika kwenye viwanja wa Staki Shari, Ukonga ambapo wakali hao waliwacharaza wapinzani wao hao.
Mabao ya Di Natale na 'kisiki' wa zamani wa Moro Utd na Yanga, Yahya Issa yalitosha kuizamisha Ukonga Veterani na kuwafanya Golden Bush kurejea maskani mwao wakichekaaa kwa ushindi huo.
Msemaji wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' alisema licha ya ushindi huo bado hakufurahishwa kwa vile walipania kutoa kipigo zaidi ya hicho.
Ticotico alisema wamekuwa na mazoea ya kuzigonga timu pinzani mabao kuanzia manne hiyo ushindi wa 2-0 wanaona kama hawakutenda haki kwa Ukonga.
Subscribe to:
Posts (Atom)