Messi akifurahia kufunga baio |
Messi akifanya vitu vyake |
Messi ni shiida |
Akijiandaa kufunga penati iliyozaa bao lake la kwanza |
Barcelona wakipongezana |
Suarez akishangilia bao lake |
MSHAMBULIAJI Nyota wa Argentina, Lionel Messi alifunga hat trick ya 24 ya La Liga, huku Luis Suarez akifunga mabao mawili wakati Barcelona wakiizamisha Rayo Vallecano.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga wakiishusha Real Madrid ambayo Jumamosi ilifungwa ugenini na Deportivo la Coruna.
Barcelona walianza kuandika bao la kwanza dakika ya tano kupitia kwa Luis Suarez akimalizia kazi nzuri ya Xavi kabla ya Gerrard Pique kufunga la pili dakika ya 49.
Messi alianza kuandika karamu yake ya mabao kwa kufunga bao la tatu la Barcelona kwa mkwaju wa penati dakika ya 56 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 63 na 68.
Bao la sita la Barcelona lilifungwa dakika za lala salama na Suarez akimaliza kasi nzuri ya Messi.
Rayo Vallecano walipata bao lao la pekee la kufutia machozi katika dakika ya 81 kwa mkwaju wa penati kupitia Bueno.