Okwi (25) akishangilia bao na wachezaji wenzake |
Raha ya ushindi |
Elias Maguli akimtoka beki wa Yanga aliyeanguka |
BAO pekee la kiufundi lililofungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya 51 limeiwezesha Simba kuizima Yanga katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Okwi, raia wa Uganda alifunga bao hilo baada ta kupenyezewa pande safi na Ibrahm Ajibu na kumchungulia kipa Ally Mustafa Barthez aliyekuwa ametoka eneo lake la kujidai na kupiga 'mashine' ya umbali wa mita 27 na kuiandikia Simba bao hilo.
Bao hilo liliwafanya wapenzi wa Yanga kulala
mapema na kuwafanya viongozi na wanachama wa Yanga waliokuwa wakitamba mapema kwamba Simba si saizi yao kuzima simu zao.
Ushindi huo umeifanya Simba kuendelea kuwatesa Yanga ambao walitoka kuwtaungua kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe 2 Desemba mwaka jana.
Simba imefikisha pointi 26 kwa ushindi huo na kushika nafasi ya tatu ikiwaengua Kagera Sugar, japo Yanga wanaendelea kuongoza msimamo wakiwa na pointi 31, moja zaidi ya Azam waliopo nafasi ya pili.
Dalili za Simba kuitambia Yanga zilianza kuonekana mapema kwenye uwanja wa Taifa, baada ya timu yao ya vijana U20 kuwanyuka wa Yanga mabao 4-2.
Katika mchezo huo Haruna Niyonzima
alitolewa uwanjani kwa kadi Nyekundu baada ya kupewa kadi ya njano ya pili kwa kupiga mpira huku filimbi ya mwamuzi Martin
Saanya wa Morogoro, ikiwa imepulizwa.
Vikosi vilikuwa hivi:
SIMBA
SC: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhan, Mohhamed
Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Abdi Banda/Simon Sserunkuma, Ramadhani
Singano, Jonas Mkude, Ibrahim Ajib/ Elias Maguli, Said Ndemla na Emanuel Okwi.
YANGA
SC: Ally Mustafa,Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir
Haroub, Kelven Yondani, Said Juma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amis Tambwe, Mrisho
Ngassa/ Khap Sherman na Danny Mrwanda/ Hussein Javu.
No comments:
Post a Comment