Vumbi Dekula Kahanga akipagawisha mashabiki katika ukumbi wa Lilla Wien, nchini Sweden unaofahamika zaidi kama 'Nairobi Ndogo' |
MWANAMUZIKI mahiri wa zamani wa bendi ya Orchestra Marquiz, Allain Dekula Kahanga 'Vumbi' akiwa na kundi lake la Dekula Band 'Ngoma ya Kilo' linalowajumuisha wakali kama Bobo Sukar, Yaya Sella na Sam Kasule wanatarajia kutambulisha nyimbo mpya kwenye onyesho litakalofanyika Mei 17-18.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Vumbi ameitumia blog hii hivi punde ni kwamba onyesho hilo litafanyikia kwenye ukumbi wa Lilla Wien maarufu kama 'Little Nairobi' nchini Sweden.
Vumbi alisema mashabiki wa bendi hiyo na wengine wa muziki waliopo Sweden na maeneo ya jirani watapa burudani kabambe kupitia nyimbo za albamu zao za zamani wakiwa kundi moja la Makonde Band na nyingine binafsi ikiwamo mpya inayoandaliwa kwa sasa.
Mcharaza gitaa huyo ambaye ni mtunzi na muimbaji, alisema watakaohudhuria maonyesho hayo mawili mfululizo bila shaka watasuuza nyoyo zao kwa namna Dekula Vumbi walivyojiandaa kuwapa kitu roho inapenda.
|
TANGAZO LAO LINASOMEKA HIVI
"Wazee Wapewe" present's;
Sammy Kasule,Bobo Sukari & Yaya Sella
Dekula Band (Ngoma Ya Kilo)
Place: Lilla Wien"Little Nairobi"
Date:17-18/05/2013
Time:21.00-01.00
Addr: Swedenborgsg.20
Pendel: Södra Station
Sammy Kasule,Bobo Sukari & Yaya Sella
Dekula Band (Ngoma Ya Kilo)
Place: Lilla Wien"Little Nairobi"
Date:17-18/05/2013
Time:21.00-01.00
Addr: Swedenborgsg.20
Pendel: Södra Station