Emmanuel Adebayor |
BAO la dakika ya 83 lililtumbukizwa kimiani na Emmanuel Adebayor muda mfupi uliopita limeiwezesha Tottenham Hotspur kuiengua kwenye nafasi ya nne timu ya Arsenal baada ya kuinyuka Stoke City nyumbani kwake mabao 2-1.
Spurs kwa ushindi wa leo imefikisha pointi 69, mbili zaidi ya Arsenal ambayo inatarajiwa kushuka dimbani Jumanne kuumana na Mabingwa wapya wa FA, Wigan Athletic.
Wageni hao walishutuliwa kwa bao la mapema la dakika ya tatu tu ya mchezo huo lililowekwa kimiani na Steven N'Zonzi kabla ya Spurs kuchomoa dakika 17 baadaye na Clint Dempsey na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe bao 1-1.
Kipindi cha kilianza kwa wenyeji kumpoteza kiungo wake Charlie Adam baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano kwa kumchezea vibaya Jan Vertonghen na kutolewa hivyo katika dakika ya 47.
Ndipo zilipokuwa zimesalia dakika saba pambano hilo kuisha Mtogo Adebayor aliiandikia Spurs bao la pili na la ushindi lililokuwa likihitajika na kuifanya Spurs kuvuna pointi zote tatu na kukwea nafasi ya nne ikiitoa kwa muda Arsenal.
Ligi hiyo inaendelea muda huu kwa mechi kadhaa ambapo tayari baadhi ya nyavu za viwanja vinavyochezwa zimeshatikiswa mabao.
No comments:
Post a Comment