STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 12, 2013

Azam yaikata maini Simba, yatinga CAF kwa kishindo

Azam Fc yaliokata tiketi ya kucheza michuano ya CAF na kuzima ndoto za Simba
TIMU ya Azam imezifuta ndoto za waliokuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania, Simba kupata nafsi ya uwakilishi wa nchi katika michuano ya kimataifa mwakani baada ya jioni hii kuidadavua Mgambo JKT kwa mabao 3-0 na kunyakua nafasi ya pili kwa msimu wa pili mfululizo.
Azam ilikuwa ikimenyama na Mgambo inayosaka pointi moja ya kujinusuru kushuka daraja kwenye pambano pekee lililochezwa leo na lililofanyika katika uwanja wa Chamazi, Mbagala Dar es Salaam.
John Bocco 'Adebayor', Kipre Tchetche na Joackins Atudo ndiyo waliioifungia Azam mabao na kuifanya inyakue pointi tatu na kufikisha pointi 51 ambazo haziwezi kufiwa na timu yoyote hata Simba waliokuwa wakiiota nafasi ya pili baada ya kupata ushindi wa mechi tatu mfululizo na kurejea kwenye nafasi ya tatu.
Azam inaungana na Yanga kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa ya Afrika mwakani, yenyewe ikicheza tena Kombe la Shirikisho la Yanga wanaoisubiri Simba Mei 18 katika mechi ya kufunga dimba itacheza Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kipigo cha jioni ya leo kimezidi kuitia tumbo joto Mgambo inayosaka pointi moja katika mechi ya pili sasa bila mafanikio, ili kujiepusha kushuka daraja na sasa kulazimika kusubiri pambano lake la mwisho dhidi ya African Lyon kuwaamua kama wataungana na wapinzani wao hao walioshuka daraja au la.
Mgambo ina pointi 25 na tishio la kuenguliwa katika nafasi na timu za Toto African na Polisi Moro zenye pointi 22 kila mmoja ambazo pia zikishinda mechi zao za mwisho huenda zikafikisha idadi hiyo na kusubiri kuangalia tofauti na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa ila iwapo kama Polisi watalala kwa Lyon.

No comments:

Post a Comment