Mwanajeshi anayedaiwa kuuwawa DR Congo |
Taarifa hizo zinamtaja mwanajeshi huyo kuwa ni Rajab Ahmad Mlima aliyeshambuliwa kwa risasi wakati akijaribu kuwalinda wakazi wa mji wa Kiwanja na Ratshruru Kaskazini mwa mji wa Goma dhidi jeshi la waasi hao wa M23.
Kifo cha mwanajeshi huyo kimekuja wakati watanzania wakiwa bado hawajasahau mashujaa wao waliouwawa Sudan Kusini na DR Congo hivi karibuni katika harakati za kulinda amani katika nchi hizo.
Mwenyezi Mung Ailaze mahali pema Peponi Roho ya mwanajeshi huyo. Ameen