MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo imetupilia mbali rufaa ya
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.
Sheikh Ponda alikata rufaa kupitia wakili wake Juma Nassoro kupinga hatia ya adhabu
aliyohukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidai kuwa
hapakuwa na ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani kwa mashtaka
yaliyokuwa yakimkabili.
Kesi nyingine inayomkabili kiongozi huyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu ambayo inasikilizwa na Jaji Augustine Shangwa imeahirishwa hadi
Novemba 20, mwaka huu.