STRIKA
USILIKOSE
Tuesday, August 26, 2014
TFF yaja na sheria kali kwa wauza, wanunua mechi
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeamua kuanzia sasa adhabu kwa watu wanaotoa rushwa au kupanga matokeo katika mchezo huo itakuwa ni kufungiwa maisha kujishughulisha na mchezo huo. Taarifa katika tovuti ya TFF imesema kwamba hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo juzi. Kwa muda sasa, kumekuwa na tuhuma nyingi za wachezaji na marefa kuhongwa ili kupanga matokeo- lakini hakukuwa na sheria madhubuti ya kupambana na hali hiyo- lakini kwa hatua hii mpya ya TFF dhahiri itasaidia kupunguza mchezo huo mchafu.
Aidha, baada ya Libya kujitoa kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika (AFCON) za 2017, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limealika nchi wanachama kuomba uenyeji wa fainali hizo.
Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24, mwaka huu imeamua Tanzania kuomba uenyeji wa fainali hizo.
“Tunatambua kuwa moja ya masharti ya kuandaa fainali hizo ni pamoja na nchi kuwa imeandaa moja ya mashindano ya vijana. Lakini kwa kuwa suala hili liko katika mazingira maalumu (exceptional circumstances) tunaamini CAF watafikiria ombi letu kwa msingi huo,”.
Awali Libya ilipewa uenyeji wa fainali hizo 2015, lakini zikahamishiwa Afrika Kusini kutokana na sababu za kiusalama. Hivyo, Libya ikapewa fainali za 2017 ambapo sasa imejitoa yenyewe kuandaa fainali hizo.
Wakati huo huo: Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi mpya wa Mashindano kuanzia Septemba 1 mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo, Wambura alikuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF kuanzia Januari 1, 2011. Nafasi hiyo sasa iko wazi na itajazwa baadaye na Kamati ya Utendaji.
26 waitwa Stars kuivaa Morocco
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Mart Nooirj ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kitakachocheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco.
Mechi hiyo, ambayo imo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), imepangwa kuchezwa Septemba 5 mwaka huu nchini Morocco.
Wachezaji wapya waliomo kwenye kikosi hicho ni kiungo Said Ndemla wa Simba SC na washambuliaji Mwagane Yeya wa Mbeya City na Juma Luizio wa ZESCO United ya Zambia.
Kikosi kamili ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Azam), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio ZESCO, Zambia).
Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
BASI LA HOOD LAGONGANA NA LORI ARUSHA
Basi la Hood lililopata ajali asubuhi ya leo eneo la Kikatiti, Arusha.
Raia wakishuhudia ajali ya basi la Hood ilivyotokea.
BASI la kampuni ya Hood lililokuwa
likitoka Arusha kwenda Iringa llimepata ajali asubuhi ya leo eneo la
Kikatiti, Arusha. Basi hilo lilitaka kugongana uso kwa uso na lori la
mizigo, ndipo katika kukwepana ikatokea ajali hiyo. Abiria wa basi wamenusurika , ila lori lilidumbukia darajani na hakukuwa na mtu aliyepoteza maisha.Mario Balotelli akabidhiwa namba ile ile 45
MSHAMBULIAJI nyota wa Italia, Super Mario
Balotelli amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Liverpool kwa pauni
milioni £16 akitokea AC Milan kwa mkataba wa miaka mitatu na kukabidhiwa jezi namba 45.
Balotelli, 25 alitua mchana wa jana Melwood na kumalizana na uongozi wa Liverpool kabla ya kusaini mkataba huo na kukabidhiwa jezi yenye namba hiyo ambayo amekuwa akitumia kuanzia Manchester City na AC Milan alikotokea kwa sasa.
Alifanyiwa ukaguzi wa afya na mtaalamu wa mambo ya utabibu wa Liverpool Ryland Morgans.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City atakuwa akilipwa kwa wiki kiasi cha pauni £125,000 ndani ya uga wa Anfield,
alihudhuria pambano la usiku wa jana dhidi ya Manchester City, ambapo klabu yake mpoya ilinyukwa na ile aliyoichezea kabla ya kwenda Milan.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Balotelli akiweka pozi
mbele ya kikombe cha Ulaya ambacho Liverpool imetwaa mara tano huku mara
ya mwisho ikiwa ni 2005
Balotelli akiwa amepozi pembeni ya nembo ya klabu yake mpya ya Liverpool.
Balotelli akisaini mkataba wa kuichezea Liverpool akiwa anarejea England baada ya miezi 18 kupita tangu aondoke Manchester City kwenda AC Milan na kuifungia mabao 30.
Hivi ndivyo Di Maria alipotua Manchester United
KIUNGO
Angel di Maria amewasili viwanja vya mazoezi vya Manchester United,
Carrington kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa Pauni 60 kutoka Real
Madrid ya Hispania.
Nyota
huyo wa Argentina aliyeng'ara kwenye Kombe a Dunia amewasili England
huku viongozi wa Old Trafford wakiendelea na mazungumzo na Real Madrid
juu ya kukamilisha uhamisho wa dau la rekodi Uingereza.
Di
Maria, mwenye umri wa miaka 26, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake
usiku huu ambao utamfanya alipwe Pauni 200,000 kwa wiki kwa zaidi ya
miaka mitano, mshahara ambao pia utamfanya awe mchezaji wa pili kulipwa
zaidi katika klabu hiyo baada ya Nahodha, Wayne Rooney.
Uhamisho
wote utaigharimu United zaidi ya Pauni Milioni 90 na mchezaji huyo
ataingia moja kwa moja katika kikosi kilichojeruhiwa cha Louis van Gaal
kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu iliyopanda Ligi Kuu, Burnley.
Liverpool yamkaribisha Balotelli kwa kichapo
Balotelli akiishuhudia Liverpool ikilala Etihad kwa mabao 3-1 |
Kun Aguerro akishangilia bao lake walipoifumua Liverpool mabao 3-1 |
Machester City ni kama ilimkaribisha tena Balotelli kwenye dimba la Etihad kwa kuwaonyesha kuwa wao ni zaidi kwa ushindi huo ambao umeifanya timu hiyo kujogea kwenye nafasi za juu za msimamo wa ligi hiyo iliyomaliza raunid mbili za awali.
Mabao mawili ya Stevan Jovetic na jingine la Sergio 'Kun' Aguerro yalitosha kuwazima vijogoo vya Anfield ambao wanahaha kusaka mbadala wa mshambuliaji wao nyota waliyemuuza Barcelona, Luis Suarez.
Liverpool ingeondoka patupu Etihad kama siyo beki wa City Zabaleta kujifunga na kuwaoa bao la kufutia machozi na kuwapa wakati mgumu kujiandaa kuwakabili Tottenham Hotspur ambao wanaoongoza msimamo kwa sasa japo wanalinda pointi na Chelsea na City walioruhusu nyavu zao kufungwa bao moja tofauti na Spurs ingawa zote zina pointi 6 na mabao matano ya kufunga.
Subscribe to:
Posts (Atom)