STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 19, 2013

Emmanuel Okwi kutua rasmi leo akitokea Uganda

Emmanuiel Okwi
 BAADA ya wanachama na mashabiki wa Yanga kuyeyushwa juu ya ujio wa mshambuliaji wao mpya wa kimataifa kutoka nchini Uganda, Emmanuel Okwi, imethibitika kwamba mchezaji huyo atatua leo saa 1:30 kutoka sasa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga muda mcahche uliopita Okwi atatua kwenye uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa MJKN saa 9:30.
Taarifa inasema kuwa Okwi atatu akitokea kwa Uganda kwa Shirika la Ndege la Rwanda na kuwahimiza
wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kumlaki.
"Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi anatarajiwa kutua leo mchana majira ya saa 9:30 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyererer akitokea nchini Uganda kwa shirika la ndege la Rwanda.
Hii ni taarifa rasmi kwa wapenzi wa soka, wanacham na mashabiki kuwa rasmi mchezaji huyo atawasili leo na kupokelewa na viongozi wa klabu ya Yanga pamoja na mashabiki na wanachama kwa ujumla.
Ujio wa Emmanuel Okwi leo unafuatia kukamilisha masuala yake yaliyokuwa yamembakisha nchini Uganda na moja kwa moja leo ataungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa jumamosi dhidi ya Simba SC katika Nani Mtani Jembe. " Taarifa ya Yanga inasomeka hivyo.

Salum Sued 'Kussi' arejea dimbani akisubiri kwa hamu duru la pili

Amerudi! Kussi (kushoto) akiwajibika katika moja ya mechi za timu yake ya Mtibwa Sugar kabla ya kuumia

BEKI wa kati wa kutumainiwa wa Mtibwa Sugar, Salum Sued 'Kussi', aliyekosa sehemu kubwa ya duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kuwa majeruhi amepona na sasa anajiandaa na duru lijalo la pili.
Akizungumza na MICHARAZO, Kussi, aliyewahi kuwa nahodha wa Taifa Stars kwa miaka mitano mfululizo, alisema kuwa majeraha yaliyokuwa yakimuandama na kumfanya asiitumikie timu yake duru lililopita yamepona na ameanza kujifua.
Nahodha msaidizi huyo wa Mtibwa, alisema japokuwa mazoezi ya pamoja ya klabu yake hayajaanza rasmi, lakini yeye anaendelea kujifua kwa sasa jijini Dar es Salaam ili kujiweka fiti kwa duru lijalo ambalo amelipania ili kuisaidia klabu yake.
"Baada ya kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi nashukuru nimeanza kujifua mwenyewe mtaani kwa sasa kujiweka fiti zaidi kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na duru la pili," alisema Kussi.
Aliongeza ana hamu kubwa ya kurudi tena uwanjani kuipigania timu yake ambayo ilimaliza duru la kwanza ikishika nafasi ya sita kwa kukusanya jumla ya pointi 20 kutokana na mechi 13.
Kussi aliyewahi kuzichezea klabu za Yanga na Azam, alipata majeraha hayo mapema mara baada ya kuanza kwa duru la kwanza na kumfanya kushindwa kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu.
Beki huyo mrefu alisema anaamini duru lijalo litakuwa gumu na hivyo ni lazima ajiweke vyema zaidi kuhakikisha Mtibwa inamaliza katika nafasi nzuri wakati ligi hiyo itakapomalizika Aprili mwakani.