STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 12, 2014

TCRA waitoza faini, yaipa onyo Times FM, kisa...!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUCfyBMCPGb1kGs84BKKyY7GJqi99M0X_vtw7Se01slrZVrI959nyXlBWA-Ym_pkRRrzOuXM2LwxbpBD_zgni4015OzXit1Vg3SgqfjKu5zNEbYsgFW3mz2W3nbR59ivFs9sk1oE-utYw/s1600/CIMG5207.JPG
Mtangazaji wa Mitikisiko ya Pwani wa Times FM, Dida akiwa kazini
KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo kali kwa kituo cha Redio cha Times Fm, pamoja na faini ya kulipa kiasi cha Sh milioni 1, kutokana na kukiuka vifungu vya maadili na kanuni za utangazaji, vilivyopo katika leseni ya utangazaji inayotolewa na mamlaka hiyo.
 
Akisoma hukumu hiyo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margareth Munyagi, alisema ‘ Times Fm’ imepewa adhabu hiyo baada ya watangazaji wake kukiuka taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo, kwa kutangaza hewani maneno yanayokiuka maadili ya utangazaji.
 
Munyagi alisema kwa nyakati tofauti kupitia kipindi chake cha ‘Hatua tatu’ kilichorushwa saa 3 hadi saa 5 asubuhi na ‘Mitikisiko ya Pwani’, kilichorushwa mchana wa Agosti 29 mwaka huu, watangazaji wa vipindi hivyo walisikika wakizungumzia dondoo zilizolenga kuhamasisha ngono bila kuzingatia muda huo ambao watoto wengi wanaweza kusikiliza.
 
Alisema kiutaratibu muda ambao dondoo hizo zilikuwa zikitangazwa, si muda muafaka kwa kuwa vipindi hivyo pia vingewezwa kusikilizwa na watoto na kwamba muda wa dondoo kama hizo kutolewa unapaswa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 alfajiri.
 
Aidha alisema utetezi uliotolewa na Mkurugenzi wa Redio hiyo, Leule Nyaulawa haukidhi haja mbali na kulipokea shitaka lililotolewa dhidi yao.
 
Nyaulawa alisema suala la kupata watangazaji wazuri Tanzania bado ni changamoto kutokana na vyuo vingi kuzalisha watangazaji wasio na uwezo mzuri.
 
Pia alisema kupitia kwa utetezi wake watakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili kuepusha kurudiwa kwa kosa kama hilo na mengine yaliyopo katika leseni za utangazaji huku kamati hiyo ikitoa muda wa mwezi mmoja kwa Times Fm kulipa faini hiyo au kukata rufaa kama haikuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao.

Ureno yafumuliwa na Ufaransa, Benzema zaidi ya Ronaldo

http://level3.soccerladuma.net/cms2/image_manager/uploads/News/179201/7/default.jpg
Benzema akifunga bao la kuongoza la Ufaransa
http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/10/11/1413055734828_lc_galleryImage_Portugal_s_Cristiano_Rona.JPG
Ronaldo akilalamika
https://media.zenfs.com/en_GB/Sports/Eurosport/1330493-28603425-2560-1440.jpg
Wachezaji wa Ufaransa wakimpongeza Pogba baada ya kufunga bao la pili la nchi yake wakiilaza Ureno 2-1
TIMU ya taifa ya Ufaransa imeitambia Ureno kwa kuilaza mabao 2-1 katika pambano la kirafiki la kimataifa, huku ikishuhudiwa nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo akishindwa kumaliza pambano kwa kuumia goti.
Mwanasoka Bora huyo wa dunai alitoka uwanjani dakika ya 76 baada ya kuumia akiwa ameshuhudia mchezaji mwenzake ambaye hivi karibuni alimwagia sifa akidai ndiye namba 9 Bora duniani akiwa amefunga bao moja na Paul Pogba akifunga la pili.
Benzema anayecheza na Ronaldo katika klabu ya Real Madrid alifunga bao la kuongoza dakika ya tatu tu kabla ya Pogba anayecheza Juventus kuongeza la pili dakika ya 65 na Ureno ilipata la kufutia machozi dakika ya 78 lililofungwa na mtokea benchi Ricardo Quaresma kwa mkwaju wa penati.

England wachonga kwa kuikung'uta San Marino

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02367/lennon_2367930b.jpgKOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema amefurahishwa na utulivu wa kikosi chake wakati wakitafuta mbinu za kuifunga San Marino katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya uliofanyika katika Uwanja wa Wembley. 
Uingereza ilikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili kabla ya kluongeza mengine matano katika kipindi cha pili na kuwafanya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 katika mchezo huo. 
Hudgson amesema kikosi chake kifanya kazi ngumu kuipenya ngome ya San Marino iliyowapa usummbufu lakini utulivu na subira kwa wachezaji wake vilifanya mchezo huo kuja kuonekana rahisi. 
Mabao ya Uingereza katika mchezo huo yalifungwa na beki Phil Jagielka, nahodha Wayne Rooney aliyefunga kwa penati, Danny Welbeck, Andros Townsend na bao la kujifunga wenyewe lililofungwa na Alessandro Della Valle aliyebabatizwa na mpira uliopigwa na Rooney. 
Ushindi huo unawapeleka Uingereza kileleni mwa msimamo wa kundi E kwa tofauti ya mabao dhidi ya Lithuania baada ya timu zote hizo kushinda mechi zao mbili walizocheza.

Dk Ndumbaro kitanzini, TFF yaomba radhi kwa upotoshwaji

Add caption

KIKAO cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimefanyika jana kujadili matukio ya hivi karibuni, hasa mwenendo wa wadau wa Bodi ya Ligi. Shirikisho linatoa tamko kwa umma kama ifuatavyo:

1. Kamati ya Utendaaji imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni mpya za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo inaomba radhi kwa wadau ambao wameguswa na kusumbuliwa na matukio hayo.

2.Kufuatia matukio hayo, Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, imefungua mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Damas
Ndumbaro ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba. Pia wadau wote waliohusika na upotoshaji huo
wakiwemo wafanyakazi wa TFF na Bodi ya Ligi watashughulikiwa kulingana na nafasi zao.

3.Kutokana na madai ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati ya Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla.

4.Kamati ya Utendaji itaendelea kuboresha Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi (Governing Regulations) ili kuweka uwiano wa utendaji na kuepusha tofauti
kati ya Bodi ya Ligi, vilabu na TFF. Aidha Kamati ya Utendaji itafanya kila linalowezekana kuboresha ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya Ligi kwa lengo la
kuwa na ligi zinazoendeshwa kisasa (Professional Leagues).

HUYU NDIYE MISS TANZANIA WA 20

MISS Tanzania mpya Sitti Abass Zuberi Mtemvu akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika shindano lililoshirikisha warembo 30 na kufanyika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Sitti Mtemvu ametwaa taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Happyness Watimanywa na kuwa mrembo wa 20 tangu shindano hilo liliporejeshwa tena nchini mnamo mwaka 1994 na kutwaliwa na Aina Maeda.

Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu, Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam. Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.
Picha zote na Othman Michuzi.
Redd's Miss Tanzania aliemaliza muda wake,Happiness Watimanywa akimpisha crown,Redd's Miss Tanzania wa sasa,Sitti Mtemvu.