Na Boniface Wambura
TIMU ya soka ya Rukwa
imeanza vizuri michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini
ya miaka 15 baada ya leo kuichapa Katavi mabao 4-0 katika mechi
iliyochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya.
Mabao
ya washindi yalitiwa wavuni na Tumaini Boniface dakika ya 13 na 65,
Francisco Mkanga akipachika la pili dakika ya 29 wakati la mwisho
lilifungwa dakika ya 75 na Innocent Ahombile.
Katika
kituo cha Zanzibar, wenyeji Mjini Magharibi imeibuka na ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Kaskazini Pemba kwa mabao ya Faisal Salum na Masoud
Mohamed.
Mechi
ya pili katika kituo hicho ilikuwa kati ya Kusini Pemba na Kusini
Unguja. Bao pekee lililofungwa na Othman Abdallah lilitosha kuipa
ushindi wa 1-0 timu ya Kusini Pemba.