STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, November 5, 2014

CAF bado yaing'ang'ania Morocco AFCON 2015

http://viasat1.com.gh/v1/vnews/uploads/caf.jpg 
SHIRIKISHO la soka barani Afrika limesema linatambua juu ya mlipuko wa ugonjwa Ebola barani Afrika licha ya kugomea ombi la kuahirishwa kwa fainali za mataifa ya Afrika 2015.
Waandalizi wa mwezi Januari nchi ya Morocco italazimika kusubiri mpaka Jumamosi kuamua kama bado wanataka kuendelea kuandaa fainali hizo ama laa.
Hapo kabla walionyesha wasiwasi ya kuendelea na maandalizi hayo kufuatia kuripuka kwa ugonjwa huo kwa kasi kubwa katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Katibu mkuu wa Caf Hicham El Amrani amesema
"tunafahamu juu ya hali ya mambo ilivyo, na si hali nzuri kwa kila mmoja wetu.
"tunajua juu ya tahadhari inayopaswa kuchukuliwa na mataifa lakini ni muhimu kuongeza hofu.

Athari za Ebola kwa Soka la Afrika mpaka sasa:

Sierra Leone imesimamisha shughuli zote za soka
Caf imezifungia Guinea, Liberia na Sierra Leone kuandaa michezo ya kimataifa
Seychelles imeondoa mchezo wake wa kufuzu AFCON dhidi ya Sierra Leone.

Kiongozi mwengine wa Kiislam auwawa Kenya

http://cdn.geeskaafrika.com/wp-content/uploads/2014/11/SheikhSalim_BakariMwarangi-690x350.jpg?505d48
Sheikh Salim Bakar Mwarangi
MAUAJI dhidi ya viongozi wa Dini ya Kiislam yameanza tena nchini Kenya, baada ya watu wasiojulikani katika  mji wa Mombasa wamemuua kwa kumpiga risasi kiongozi mashuhuri na mwenye msimamo wa wastani wa dini ya kislamu.
Sheikh Salim Bakari Mwarangi ambaye ni mwanaharakati wa kampeni dhidi ya itikadi kali alipigwa risasi wakati alipokuwa akirudi nyumbani kutoka msikitini jumanne usiku.
Viongozi sita wa dini ya kiislamu badhi yao wenye itikadi kali na wale walio na misimamo ya wastani wameuawa mjini Mombasa tangu mwaka 2012.
Eneo la pwani ya kenya lenye waislamu wengi limekumbwa na misururu ya mashambuli ya mabomu yanoyoaminika kutekelezwa na watu walio na uhusiano na kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia.
BBC

HAYA NDIYO MATOKEO YA DARASA LA SABA


1.Twibhoki (Mara),
2.Mugini (Mwanza),
3.PeaceLand (Mwanza),
4.Alliance (Mwanza),
5.Kwema (Kahama - Shinyanga)
6.St.Severine (Kagera),
7.Rocken Hill (Kahama - Shinyanga),
8.Tusiime (DSM),
9.Imani (KLM)
10.Palikas (Kahama - Shinyanga)





HIZI NDIZO ZA KWANZA KUFUZU 16 ULAYA

Karim Benzema scores Real Madrid's opener against LiverpoolAleksander Mitrovic scores a dramatic last minute equaliser for Anderlecht against ArsenalBorussia DortmundWAKATI kivumbi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ikitarajiwa kuendelea usiki wa leo, michuano hiyo jana ilishuhudia timu mbili za Real Madrid ya Hispania na Borussia Dortmund ya Ujerumani zikiwa timu za kwanza kufuzu hatua ya 16 Bora katika makundi yao.
Madrid aliwapata nafasi hiyo baada ya kuidonyoa Liverpool kwa bao 1-0 lililofungwa na Karim Benzema, katika mechi za Kundi B, wakati Dortmund inayonolewa na Jurgen Klopp iliinyuka Galatasaray kwa mabao 4-1 n kufuzu hatua hiyo kutoka kundi D.
Timu zimefikisha jumla ya pointi 12 kila moja katika kundi lake na kufuzu moja kwa moja katiak hatua inayofuata na kusubiria kujua timu itakazoungana nazo kwenye mechi za raundi ya tano zitakazochezwa baadaye.
FC Basel wapo nyuma ya Real Madrid baada ya usiku wa jana kuinyuka Ludogorets Razgrad ya Bulgaria kwa mabao 4-0.
Mabingwa wa La Liga, Atletico Madrid ilitakata ugenini baada ya kuilaza Malmo kwa mabao 2-0 katika mechi ya kundi A huku Olympiakos wakisalia nafasi ya pili baada ya kunyukwa ugenini mabao 3-2 na Juventus.
Katika mechi za Kundi C Bayer Leverkusen wamejiimarisha kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya Zenit Saint Petersburg, Benfica wao walifufua matumaini yao ya kusonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Monaco.
Arsenal wao wameendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Dortmund baada ya kushindwa kulinda ushindi wake na kujikuta wakitoa sare ya mabao 3-3 na Anderletch katika Uwanja wa Emirates.
Timu hiyo ilikuwa mbele kwa mabao 3-3 hadi dakika ya 60 kabla ya wageni kurudisha bao moja baada ya jingine na kufanya matokea kuwa sare na kumkasirisha meneja wao Arsene Wenger aliyeitupia lawama safu yake ya ulinzi.

Copy n Win at: http://bit.ly/copy_win

RATIBA SDL HII HAPA MPANDA KUANZA NA UJENZI



MICHUANO ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu ambapo Mpanda United itakuwa mwenyeji wa Ujenzi Rukwa.
Mechi hiyo ya kundi A itachezwa kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga. Siku hiyo hiyo katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya Mvuvumwa FC na CDA (Lake Tanganyika, Kigoma), na Milambo dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kundi B mechi za ufunguzi ni kati ya Pamba na JKT Rwamkoma kwenye Uwanja wa CCM Kirumba huku Bulyanhulu FC ikiwa mwenyeji wa AFC kwenye Uwanja wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga.
Abajalo FC ya Dar es Salaam itaikaribisha Kariakoo FC ya Lindi kwenye mechi ya kundi C itakayochezwa Uwanja wa Karume. Nazo Kiluvya United na Transit Camp zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.
Kundi D mechi tatu za ufunguzi ni kati ya Town Small Boys na Volcano FC (Uwanja wa Majimaji, Songea), Njombe Mji na Mkamba Rangers (Uwanja wa Sabasaba, Njombe), na Wenda FC dhidi ya Magereza Iringa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya

Abuu Ntiro arejeshwa Stars, Nooij atangaza kikosi

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane, akimjumuisha beki wa zamani wa Yanga Abuu Ntiro.
Akizungumza Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.
Wachezaji wapya waliojumuishwa katika kikosi hicho ni Ntiro anayeichezea Kagera Sugar, Hassan Isihaka wa Simba.
Kikosi kamili cha timu hiyo ni kama ifuatavyo:
Makipa: Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga).
Mabeki: Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).
Viungo: Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji:
Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo