KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24
kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu
jijini Mbabane, akimjumuisha beki wa zamani wa Yanga Abuu Ntiro.
Akizungumza Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema
kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye
hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye
Uwanja wa Gymkhana.
Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager itaondoka kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili
kabla ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.
Wachezaji wapya waliojumuishwa katika kikosi hicho ni Ntiro anayeichezea Kagera Sugar, Hassan Isihaka wa Simba.
Kikosi kamili cha timu hiyo ni kama ifuatavyo:
Makipa: Aishi Manula (Azam) na
Deogratias Munishi (Yanga).
Mabeki: Abubakar Mtiro (Kagera Sugar),
Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka
(Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua
(Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari
Kapombe (Azam).
Viungo: Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo
(Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said
Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji: Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP
Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo
No comments:
Post a Comment