|
Arsenal watashangilia kama hivi kwa Bayern Munich leo |
|
Baadhi ya wachezaji wa Bayern Munich wakijifua tayari kwa mechi ya leo |
KIVUMBI cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kinatarajiwa kuendelea tena leo kwa mechi mbili kali zitakazowakutanisha mabingwa watetezi, Bayern Munich itakayuokuwa ugenini kuvaana na Arsenal, huiku Am Milan wakiwaalika Atletico Madrid katika mechi za mkondo wa kwanza za 16 Bora.
Tayari mechi mbili za awali za hatua hiyo ziliochezwa usiku wa kuamkia leo na kushuhudia matokeo ya kusisimua ambayo yamewafanya mashabiki wa kandanda ulimwenguni kuote kutaka kuona mechi ya leo nazo zitakuwa na matokeo ya aina gani.
Arsenal wanaoongoza Ligi Kuu ya England, wanakumbuka kipigo walichopewa na watetezi hao kwenye uwanja wao wa Emirates katika mechi baina yao kulala 3-1 kabla ya kwenda kushinda ugenini 2-0 lakini ikang'oka michuanoni wa Bavarian hao.
Hata hivyo vijana wa Gunners wameapa kupata ushindi leo nyumbani na kwenda kufanya kweli ugenini ili kuvuka hatua hiyo ya 16 Bora ilityokwama kwa karibu misimu minne.
Gunners wanapaswa kupigana kiume mbele ya vijana wa Pep Guardiola kwa sababu Bavarian wapo katika kiwango bora msimu huu kama ilivyokuwa misimu miwili mfululizo iliyopita.
Ikiwa imetoka kuing'oa mashindanoni Liverpool waliowapopoa kwenye ligi mabao 5-1 katika mbio za kuwania kombe la FA, Arsenal wameapa kufa na Bayern katika mechi ya leo kaa alivyonukuliwa beki wake wa kati anayetoka Ujerumani Per Mertesacker aliyedai kuwa itawakuwa "mechi mbili sahihi" kwa Arsenal kusonga mbele, lakini hilo ndilo muhimu na si kuonyesha kuikubali sana Bayern.
"Tunatakiwa kwenda kucheza mechi mbili sahihi dhidi yao," alinukuliwa
"Tunajua tunaweza kuwafunga kwa sasa, hivyo labda kiakili tupo katika hali nzuri kuliko mwaka jana.
"Tuliwakubali sana katika mchezo wa kwanza baada ya hapo, ilikuwa kazi rahisi kwao.
"Ladba tumejifunza kitu fulani kutokana na somo hilo na tutafanya vizuri wakati huu.
"Sasa tunayo nafasi nyingine na fursa ya kuwafunga mabingwa. Tunataka kupata mafanikio ya kipekee msimu huu, hivyo tunapaswa kuwafunga walio bora.
"Hilo si kwa Manchester City na Chelsea tu, pia na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya."
Hata hivyo Arsenal itamkosa kiungo Mikel Arteta anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyozawadiwa katika hatua ya makundi dhidi ya Napoli, wakati Jack Wilshere na Bacary Sagna, ambao walikuwa katika benchi dhidi ya Liverpool wakitarajiwa kuwamo, huku Kieran Gibbs na Santi Cazorla, waliocheza kipindi cha pili na Tomas Rosicky, aliyekuwa amepumzishwa wote wakirejeshwa katika mechi ya leo.
Kwa upande wa Kiungo Mathieu Flamini anaamini kuwa ushindi dhidi ya Liverpool utawahamasisha kufanya vizuri dhidi ya Bayern.
Flamini alisema kukichapa kikosi cha Brendan Rodgers ambacho kipo katika kiwango cha juu ni changamoto kwao kufanya vizuri katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwamba kufungwa na Bayern msimu uliopita haiwezi kuwa sababu ya Arsenal kufanya vibaya tena.
Wapinzani wao Bayern imeendelea kuongoza katika ligi ya ndani baada ya Jumamosi kushinda 4-0 dhidi ya Freiburg licha ya kuwapumzisha Jerome Boateng, David Alaba, Thiago na Mario Goetze.
Ushindi huo unaifanya Bayern kushinda mechi 13 mfululizo za Bundesliga huku ikiwa imeshuka dimbani mara 46 bila kufungwa. Mechi pekee iliyopoteza msimu huu ni ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nyumbani dhidi ya Manchester City, ikiwa tayari imejihakikishia kusonga mbele hatua ya 16 bora.
Itashuka uwanjani leo bila winga wa Kifaransa Franck Ribery, ambaye ni majeruhi, na Xherdan Shaqiri aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuzipa pengo lake na aliyefunga mara mbili dhidi ya Freiburg, lakini atakuwa nje kutokana na kuwa majeruhi wa paja.
Pamoja na hali ya ushindi wa msimu uliopita jijini London, walipopata ushindi wa mapema kupitia kwa Toni Kroos na Thomas Mueller hivyo kuwa mbele kwa mabao 2-0 ndani ya dakika ya 21, nahodha wa Bayern Philipp Lahm bado anaihofia Arsenal.
"Mechi ni tahadhari kwetu," Lahm alisema. "Tulikuwa wazuri sana jijini London, tulifikiri hakuna lolote linaweza kutokea kwetu katika mchezo wa marudiano. Yote kwa yote ghafla tukawa tumechapwa 2-0 na kulikuwa bado na dakika chache za kucheza. Ukweli inaonyesha kuwa mambo yanaweza kwenda haraka katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Tutakuwa na kukumkumbu ya hilo katika akili zetu."
Lahm alisema anaitupia macho ya karibu Arsenal huku angalizo lake likiwa kwa Wajerumani wenzake Mertesacker, Mesut Ozil na Lukas Podolski, pamoja na Kinda ambaye hajaichezea timu ya taifa Serge Gnabry.
Mechi ya marudiano kwa timu hizo itachezwa Ujerumani Machi 11, mwaka huu na katika pambano jingine la leoAC Milan itakuwa uwanja wa nyumbani wa San Siro nchini Italia kuikaribisha Atletico Madrid.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa kali kutokana na uborwa wa Atletico kwa sasa ikiongozwa na 'muuaji' wao Diego Costa, huku Milan ikipigana kurejesha heshima yake chini ya Clarence Seedorf baada ya kuwa na msimu mbaya katia Seria A safari hii.
Barcelona, PSG wenyewe wameshamaliza kazi zao na kusubiri michezo ya marudiano, je Arsenal au Bayern Munich itakayomliza mwenzake, au Milani kukubali kuendelea kudorora kwa Madrid tusubiri.