Messi akifunga penati iliyolalamikiwa na kocha Pellegrini |
Ibrahimovic akifunga moja ya mabao yake, chini akishangilia bao lake la kwanza |
Add caption |
Pellegrini anailalamikia penati iliyotolewa kwa wapinzani iliyosababishwa na kufungwa na Lionel Messi dakika tisa baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Messi aliangushwa nje kidogo na eneo la penati na Martin Demichelis na refa Jonas Eriksson kuamuru ipigwe adhabu hiyo na Messi kuifungia Barcelona bao la kuongoza kabla ya beki Dani Alves kuongeza la pili dakika ya 90 na kuiweka Barca katika nafasi nzuri ya kutinga robo watakapoikaribisha Manchester City kwenye mechi ya marudiano Machi 11.
Pellegrini amenukuliwa akisema anashangaa ni vipi UEFA hata ikamteua mwamuzi huyo kutoka Sweden kuchezesha pambano kubwa kama hilo, huku akidai mara kadhaa amekuwa wakiionea timu yake.
Hata hivyo matamshi hayo ya kocha huyo kutoka Chile yanaweza kumweka matatani kwa 'mabosi' wa UEFA.
Katia mechi nyingine ya michuano hiyo hatua ya 16 Bora, mabingwa wa Ufaransa, PSG ikiongozwa na Zlatan Ibrahimovic, iliisasambua Bayer Liverkusen nyumbani kwao kwa kuichabanga mabao 4-0.
Wanafainali hao wa michuano ya mwaka jana wakiwa kwenye uwanja wao wa BayArena mjini Leverkusen, nchini Ujerumani walishindwa kuamini kipigo walichopewa na Wafaransa hao ambao ni kama wamejihakikishia hatua ya robo fainali kwa vile Leverkusen watalazimika kuifunga PSG mabao 5-0 jijini Paris ili kuiondosha kitu kinachoonekana kuwa kigumu, japo soka lolote linaweza kutokea.
Mabao ya wababe hao wa Ufaransa yalifungwa na Blaise Matuidi dakika ya tatu kwa pasi ya Verratti, kabla ya Ibrahimovic kuongeza la pili dakika ya 39 kwa mkwaju wa penati na kisha kufunga jingine dakika 42 akimaliza pasi Matuidi.
Bao la nne lililoikata maini Wajerumani nyumbani kwao liliwekwa kimiani na mchezaji mpya wa timu hiyo kutoka Newcastle United, Yohan Cabaye aliyefunga katika dakika ya 88 akimaliza pasi ya Lucas.
No comments:
Post a Comment