Prisons |
Pambano hilo limechezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya ambapo mechi hiyo ya 'kiporo' ilishuhudia wenyeji wakipata mabo yao kupitia kwa Peter Michael aliyefunga mabao mawili, Omega Seme, Nurdin Chona, Lugano Mwangama na Frank William na kuiwezesha timu hiyo kuchupa hadi nafasi ya 9 ikiwa na pointi 19 sawa na JKT wanaoshuka hadi nafasi ya 10 kuipisha Prisons kwa tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa.
Kipigo hicho kinaweza kuwa mwanzo mbaya kwa JKT inayojiandaa kushuka dimbani Jumapili dhidi ya Simba, ikiwa chini ya kocha mpya Fred Minziro baada ya aliyekuwa kocha wao Mbwana Makatta kubwaga manyanga wiki chache zilizopita.
Timu hiyo katika mechi nne zilizopita imeambulia pointi moja tu baada ya kufungwa mechi tatu na kupata sare mchezo mmoja dhidi ya Oljoro JKT.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara:
P W D L F A GD PTS
01.Azam 16 10 06 00 29 10 19 36
02.Yanga 16 10 05 01 34 12 22 35
03.Mbeya City 18 09 08 01 24 14 10 35
04.Simba 18 08 08 02 33 16 17 32
05.Ruvu Sh. 18 06 07 05 20 19 01 25
06.Kagera Sugar 18 05 08 05 15 15 00 23
07.Coastal Union18 04 10 04 12 09 03 22
08.Mtibwa Sugar 18 05 07 06 21 22 -01 22
09.Prisons 17 04 07 05 15 16 -01 19
10. JKT Ruvu 18 06 01 11 13 27 -14 19
11.Mgambo 18 04 05 09 10 26 -16 17
12.Oljoro 19 02 09 08 14 28 -14 15
13.Ashanti 17 03 05 09 14 28 -16 14
14.Rhino Rangers18 02 07 09 12 22 -10 13
Wafungaji:14- Tambwe Amisi (Simba)
09- Elias Maguri (Ruvu Shooting), Kipre Tchetche (Azam)
08- Hamis Kiiza (Yanga), Juma Luizio (Mtibwa Sugar)
06- Themi Felix (Kagera Sugar), Mrisho Ngassa, Didier Kavumbagu (Yanga), Peter Michael (Prisons)
05- Tumba Sued (Ashanti Utd), Jerry Santo (Coastal Union), Jerome Lambele (Ruvu Shooting)
04- Jerry Tegete (Yanga), Jonas Mkude, Betram Mombeki (Simba), Bakar Kondo, Salum Machaku (JKT Ruvu),
03- Haruna Chanongo, Ramadhani Singano (Simba), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Humphrey Mieno, Mcha Khamis (Azam), Amir Omary (Oljoro), Jeremia John (Mbeya City), Said Dilunga (Ruvu Shooting)
Mechi zijazo za Ligi hiyo wikiendi hii;
Feb 22, 2014
Ruvu Shooting vs Yanga SC
Kagera Sugar vs Rhino
Mtibwa Sugar vs Ashanti Utd
Coastal Union vs Mbeya City
JKT Oljoro vs Mgambo
Azam vs Prisons
Feb 23, 2014
Simba SC vs JKT Ruvu
No comments:
Post a Comment