Mashindano ya
12 ya Kilimanjaro Marathon yanayotarajiwa kufanyika Moshi Machi 2, 2014
yamezinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Katika uzinduzi
huo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema: “Ninayo furaha kutangaza
kwamba huu utakuwa mwaka wa 12 kwa mbio za Kilimanjaro Marathon kufanyika chini
ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager.
Kwa mara nyingine,
ni fahari kubwa kwa Kilimanjaro Premium Lager kudhamini tukio hili maarufu na lenye
msisimko mkubwa katika kalenda ya michezo ya Tanzania.”
Kavishe alitangaza
nyongeza ya asilimia 25 kwenye zawadi za fedha kwa washindi wa mbio za kilometa
42 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, ambapo jumla ya zawadi ya fedha itaongezeka
kutoka Tsh milioni 15 hadi Tsh milioni 20, huku washindi wa kwanza, wa pili na wa
tatu wanaume kwa wanawake wakipokea jumla ya Tsh milioni nane na kiasi kilichobaki
kikigawanywa miongoni mwa washindi wanne hadi wa 10.
Kavishe alisema
kwamba ni bahati kubwa kwa Kilimanjaro Premium Lager kudhamini mashindano haya yenye
msisimko mkubwa katika kalenda ya michezo nchini Tanzania na kwamba Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager itatoa zawadi kubwa za fedha kwa wanariadha wakati wengine
watabaki wana kumbukumbu isiyofutika ya ukaribu wa hali yajuu.
Ili kuwahamasisha
na kuwapa motisha wanariadha wa Tanzania kuongeza viwango vyao na kutumia muda mfupi
kumaliza mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager imetenga Shilingi milioni mbili kama
bonasi au malipo ya nyongeza kwa wanariadha wa Tanzania watakaovunja rekodi kwenye
mashindano hayo.
Zawadi zitakazotolewa
kwenye 2014 Kilimanjaro Marathon zimenyumbulishwa kitakwimu kama ifuatavyo hapa
chini;
2014 KILI MARATHON PRIZES
|
2013 KILI MARATHON PRIZES
|
||||
MALE
|
FEMALE
|
MALE
|
FEMALE
|
||
1ST
|
4,000,000
|
4,000,000
|
1ST
|
3,000,000
|
3,000,000
|
2ND
|
2,000,000
|
2,000,000
|
2ND
|
1,500,000
|
1,500,000
|
3RD
|
1,000,000
|
1,000,000
|
3RD
|
850,000
|
850,000
|
4TH
|
900,000
|
900,000
|
4TH
|
650,000
|
650,000
|
5TH
|
600,000
|
600,000
|
5TH
|
500,000
|
500,000
|
6TH
|
400,000
|
400,000
|
6TH
|
350,000
|
350,000
|
7TH
|
350,000
|
350,000
|
7TH
|
250,000
|
250,000
|
8TH
|
300,000
|
300,000
|
8TH
|
200,000
|
200,000
|
9TH
|
250,000
|
250,000
|
9TH
|
150,000
|
150,000
|
10TH
|
200,000
|
200,000
|
10TH
|
100,000
|
100,000
|
SUB TOTAL
|
10,000,000
|
10,000,000
|
SUB TOTAL
|
7,550,000
|
7,550,000
|
GRAND TOTAL
|
20,000,000
|
GRAND TOTAL
|
15,100,000
|
Kavishe alisema
anatarajia kwamba zawadi hizo za fedha zitawavutia wanariadha mashuhuri na kuwapa
moyo wengine kuvunja rekodi za mashindano hayo.
Aliongeza kwamba
Kilimanjaro Marathon imepiga hatua kutoka tukio la mkoa hadi kuwa mashindano makubwa
ya kimataifa. “Tunatambuliwa na IAAF na Chama cha Kimataifa cha Mbio za masafa Marefu.
Licha ya mafanikio haya, tunaendelea kujitahidi kuboresha mbio hizi mwaka hadi mwaka,”
alisemaKavishe.
Tunashukuru
kwa jinsi walivyoungwa mkono na Wizara ya Michezo na mamlaka za Serikali ya Mkoa
wa Kilimanjaro, Riadha Tanzania, Chama cha Mbio za Ridhaa Kilimanjaro, pamoja na
wadhamini wenzawao ambao ni Vodacom (5km Fun Run), GAPCO, Simba Cement, CFAO
Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, FNB Bank, UNFPA, TanzaniteOne na Kilimanjaro
Water kwa kusaidia kuikuza Kilimanjaro Marathon kuwa moja ya mashindano makubwa
zaidi ya mbio za masafa marefu barani Afrika.