STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, November 13, 2013

Mwili wa Dk Mvungi kuletwa Ijumaa kuzikwa Jumatatu

Dk Mvungi alipokuwa akisafishwa kwenda Afrika kusini kwa matibabu zaidi
MWILI wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania, Dk Sengondo Mvungi (61) unatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa tayari kwa ajili ya mazishi yake, huku Chama cha NCCR-Mageuzi kikiwataka watanzania kuwa na utulivu kufuatia kifo cha kiongozi wao huyo muhimu.
Akitoa taarifa ya ratiba ya mazishi ya Dk Mvungi, Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alisema wamesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo ambaye alikuwa kiungo muhimu.
Mbatia alisema Dk. Mvungi ameacha pengo kubwa ndani ya chama ambalo halitazibika kutokana na kukitumikia kwa moyo mmoja.
Alisema baada kukaa kama chama, familia na serikali, walikubalina na kwamba mwili wake uwasili Novemba 15 mwaka huu toka Afrika Kusini na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo ambako utahifadhiwa.
Novemba 16 mwaka huu, mwili huo utapelekwa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam saa 3:00 asubuhi hadi 6:00 mchana kwa ajili ya ibada ya kumwombea.
Mbatia alisema baada ya ibada, mwili huo utapelekwa katika Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya watu mbalimbali kutoa heshima ya mwisho kuanzia saa 6:30 mchana hadi 10: 00 jioni.
Baada ya hatua hiyo, mwili huo utapelekwa nyumbani kwake Kibamba kupumzishwa ili siku ya Jumapili  Novemba 17  uweze kusafirishwa kijijini kwao Kisangara – Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili maziko yatakayofanyika  Novemba 18 mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete na mkewe Salma jana walikuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu Dk.  Mvungi kwa ajili ya kuhani.
Rais Kikwete walifika nyumbani hapo saa 6:00 mchana ambapo alipata fursa ya kumpa pole mke wa marehemu, Anna Mvungi, wanafamilia na wananchi waliofika katika msiba huo.
Pia viongozi kadhaa wa serikali, siasa, wanasheria na wananchi wengine walifika nyumbani hapo kuomboleza msiba huo.
Salamu za rambi rambi zimekuwa zikitolewa na watu mbalimbali vikiwemo vyama vya siasa na asasi za kijamii kufuatia kifo cha Dk Mvungi aliyevamiwa na kucharangwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa majambazi Novemba 3 nyumbani kwao Kibamba Msakuzi.
Dk Mvungi alifariki mchana wa jana akipatiwa matibabu nchini Afriuka Kusini alkikopelekwa baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI).

No comments:

Post a Comment