STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, November 29, 2013

Kocha mpya wa Azam kutua nchini kesho

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjYMYRwRJNTdZk47-t9l1I-1h_HV7hn7E52_3lwyskO763mJUnsmohhInBLojgb382ujZiEbi5AusRgouobp1e3wZovcT9ueeANh5NLDPXGmfuvo6AhyphenhyphenVlIPcPY0gAJ3McRRjGzOiFYwKA/s640/Joseph-Marius-Omog-AC-Leopa.jpg
Kocha mpya wa Azam, Joseph Omog anayetua nchini kesho
 KOCHA mpya wa klabu ya Azam, Joseph Marius Omog kutoka nchini Cameroon anatarajiwa kutua kesho asubuhi tayari kumwaga wino wa kuinoa timu hiyo.
Kocha huyo aliyekuwa akiinoa AC Leopards ya Congo Brazaville na kuipa ubingwa wa Kombe la Shirikisho mwaka jana atatua nchini kesho saa 3 asubuhi tayari kumaliza na na mabosi wake wapya.
Iwapo maafikiano yatapatikana, kocha huyo ataanza kuinoa timu hiyo kwa ajili ya duru la pili la ligi kuu na Kombe la Shirikisho itakayoshiriki mwakani kuanzia Jumatatu ambapo kambi ya timu hiyo itaanza rasmi.
Kocha huyo anakuja kuchukua nafasi ya Muingereza Stewart John Hall, aliyetemana na timu hiyo baada ya kupa mafanikio ya kunyakua nafasi ya pili mara mbili katika Ligi Kuu Tanzania Bara na kunyakua vikombe vya Mapinduzi na kucheza Kagame Cup hatua ya fainali.
Kwa mujibu wa akaunti ya klabu ya Azam, mashabiki wanaalikwa kwenda kumpokea kocha huyo kesho atakapowasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa ndege wa JK Nyerere.

Ajikata uume ili kukwepa usumbufu wa wanawake

Kijana anayedaiwa kuukata uume wake
Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimapenzi... 

Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa nje..

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu, aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.

Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za msingi.


The Fresh 2013

Yanga yaifuata Coastal fainali za Uhai Cup


http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2013/09/Yanga.jpg

TIMU ya soka ya vijana ya Yanga, imeonyesha dhamira yao ya kunyakua taji la Uhai 2013 baada ya jioni hii kuinyuka Mtibwa mabao 3-1 katika pambano la Nusu Fainali ya michuano hiyo inayohusisha timu za U20.
Kwa ushindi huo umeifanya Yanga sasa kujiandaa kukutana na Coastal Union katika pambano la fainali litakalochezwa Jumapili ili kupata bingwa mpya baada ya Azam kuvuliwa taji hilo jana.
Yanga na Coastal zinakutana kwa mara ya pili kwani zilikuwa katika kundi moja na ilishuhudiwa Yanga ikiinyoa Coastal mabao 2-1, hivyo kulifanya pambano hilo la Jumapili kutarajiwa kuwa gumu.
Yanga ilipata ushindi huo katika mechi hiyo ya leo iliyochezwa kwenye uwanja wa Chamazi kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Notikel Masasi aliyefunga dakika ya 17 na 32, kuizima Mtibwa iliyotangulia kufunga bao dakika ya 14 kupitia Shiza Kichuya.
Bao lililoikatisha tamaa Mtibwa iliyoishangaza Simba kwa kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuifumua 3-2 na kutiha hatua hiyo lilifungwa dakika ya 86 na Hamis Issa.

Warembo waanza kujinoa kwa shindano la Miss Tanzania USA

Lady Kate, Pamela, Ma Winny na Asha katika picha ya pamoja na Mamiss Tanzania USA.


Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant akiwaasa Mamiss Tanzania USA Pageant leo Jumamtano Novemba kwenye hotel ya Marriott
Pamela Egbe Messy mratibu wa Miss Africa USA Pageant akiwaelimisha walimbwende
MaWinny Casey Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na mratibu wa Miss Tanzania USA Pageant, Asha Nyang'anyi (kulia)
Mamiss Tanzania USA Pageant wakimsikiliza Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant alipokuwa.

KINANA AWASILI MBOZI ASUBUHI HII

 Vijana wa CCM wa Tawi la Mpemba, wilayani Momba, Mbeya, wakiwa na hamu ya kumsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye na msafara wake walikuwa wanakwenda wilayani Mbozi kuendelea na ziara ya kuimarisha chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kusikiliza kero za wananchi.
 Wafuasi wa CCM wakishangilia wakati Katibu wa NEC wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza nao aliposimama kwa muda katika shina la Vijana wa CCM la Mpemba akiwa njiani kwenda wilayani Mbozi, akitokea wilayani Momba.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wafuasi wa CCM katika Tawi la CCM la Mpemba, wilayani Momba.
 Kinana akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alipowasili mjini Mbozi leo.
 Msanii wa kikundi cha ngoma cha Hakuna Kulala, Catherine Kapessa akipuliza baragumu wakati wa mapokezi ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Ofisi za CCM
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimia baadhi ya viongozi wa CCM msafara wa Kinana ulipowasili Ofisi ya CCM Mbozi leo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma iliyokuwa ikipigwa na wasanii kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya leo
 

Mtanzania ang'ara Miss Earth Ufilipino

 Mwandishi Wetu
Nyota wa mrembo wa Tanzania anayewania taji la Miss Earth, Clara Noor imeanza kung’ara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika taji la fukwe ya Pagudpud iliyopo nchini Phillipines.
Mbali ya kutwaa taji hilo, Clara pia ameibuka mshindi wa tatu katika taji la vazi la Taifa na kuzipiku nchi nyingine nyingi na kuzawadiwa medali ya shaba.
Katika mashindano ya tuzo maalum, jumla ya tuzo 11 zilikuwa zinagombaniwa na warembo 88 walikuwa wanawania mataji hayo ambayo zawadi zake zilitolewa na wadhamini hao.
Clara alionyesha uwezo mkubwa katika taji hilo na kuwa mwafrika wa kwanza kushinda katika historia. Katika vazi la Taifa, Clara aliwavutia wengi na kupata ushindani mkubwa kutoka kwa mrembo wa warembo kutoka Afrika Kusini, Ashanti Mbanga na kutoka Nigeria, Marie Miller ambao walishika nafasi ya kwanza nay a pili.
Muandaaji wa Miss Earth Tanzania, Maria sarungi Tsehai alisema kuwa ni faraja kubwa kwa Clara kuitangaza Tanzania kwa kupitia mataji hayo mawili kwani mbali ya jina lake, kinachotangazwa pia ni nchi.
“Amefanya vyema mpaka sasa, tunatarajia kuona anaendelea kufanya vizuri na kutuletea sifa, mpaka sasa anastahili pongezi,” alisema Maria ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications.
Alisema kuwa fainali ya mashindano hayo yatafanyika Desemba 7 kwenye ukumbi wa Versailles Palace, Alabang, Muntinlupa City na kurushwa live na vituo vya televisheni vya STAR World, ABS-CBN, Velvet, The Filipino Channel, Ustream na Venevisión.

Sare ya Zimbabwe yaipaisha Tanzania viwango vya FIFA, Burundi haooo!

Taifa Stars ya Tanzania
TANZANIA imepanda nafasi tano zaidi katika viwango vya Fifa, hivyo sasa kuwa ya 124 kutoka 129 iliyokuwepo mwezi Oktoba, huku Zimbabwe waliotoka suluhu na Taifa Stars wiki iliyopita ikishuka kwa nafasi nne na sasa kuwa ya 106 toka 102.
Zambia ambayo jana ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kilimanjaro Stars ikiwa kama timu alikwa kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyoanza juzi jijini Nairobi, Kenya, imeshuka nafasi tano na sasa ni ya 72 katika viwango hivyo.
Katika nchi za Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Uganda ndiyo inayoshika nafasi ya juu ikiwa ya 86 duniani licha ya kushuka kwa nafasi moja mwezi huu.
Burundi ambayo imepanda kwa nafasi tisa, inashika nafasi ya pili kwa upande wa Cecafa ikiwa nafasi ya 112 duniani, ikifuatiwa na Kenya iliyopanda kwa nafasi moja na kuwa ya 117 duniani, huku Rwanda iliyopanda kwa nafasi mbili na kuwa ya 127, ikiburuza mkia kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Jirani zetu  DR Congo wanashika nafasi ya 84    baada ya kupanda kwa nafasi saba zaidi mwezi huu, huku kwa upande wa Afrika, Ivory Coast ikiongoza na kwa dunia ikishika nafasi ya 17.
Ghana iliyoshuka kwa nafasi moja, inashika nafasi ya pili kwa Afrika huku kwa dunia ikiwa ya 24 na kwa bara hili ikifuatiwa na Algeria iliyopo nafasi ya 26 duniani baada ya kupanda nafasi sita.
Hispania ndiyo kinara katika viwango hivyo ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina, Colombia, Ureno, Uruguay, Italia, Switzerland , Uholanzi, Brazil, Ubelgiji, Ugiriki na England ikiwa ya 13 baada ya kushuka kwa nafasi tatu mwezi huu.

Tottenham Hotspur yapoza machungu Europa League kuikabili Man Utd J'2


KLABU ya Tottenham Hotspur ilisahau machungu yote ya kipigo cha iabu cha mabao 6-0 toka kwa Manchester City katika mechi za Ligi Kuu ya England baada ya kuendeleza ushindi wa 100% katika UEFA Europa League kwa kuilaza Tramso wa Norway na kutinga hatua inayofuata.
Ushindi huo w augenini umeifanya Spurs kufikisha pointi kutokana na mechi tano ilizocheza ikifunga mabao 11 na kufungwa moja, inaweza kuwaweka vyema kabla ya kuwakabilia Manchester United katika mechi nyingine ngumu ya Ligi Kuu siku ya Jumapili.
Wenyeji Tramso walianza kujifunga wenyewe kupitia mchezaji wao Adnan Causevic aliyekuwa katika harakati za kuokoa mpira katika dakika ya 63 kabla ya Moussa Dembele kuihakikisha Spurs ushindi huo na kuongoza kundi lake la K wakifuatiwa na Azhi Machkachala ya Urusi.
Katika mechi nyingine za Ligi hiyo ndogo ya Ulaya  ni kama ifuatavyo;
Shakhter Karagandy 0 - 2    PAOK 
Kuban' Krasnodar     4 - 0     St. Gallen 
Rubin Kazan'     1 - 1     Maribor 
Anzhi     1 - 1     Sheriff     
Genk     3 - 1     Dynamo Kyiv    
Rapid Wien     2 - 1     Thun     
Slovan Liberec     1 - 2     Freiburg   
Sevilla     1 - 1     Estoril    
Olympique Lyonnais     1 - 0     Real Betis   
Rijeka     0 - 0     Vitória Guimarães       
Trabzonspor     4 - 2     Apollon    
Legia Warszawa     0 - 2     Lazio   
AZ     2 - 0     Maccabi Haifa     
Swansea City     0 - 1     Valencia    
Chornomorets     2 - 1     Dinamo Zagreb    
Ludogorets     2 - 0     PSV    
Elfsborg     0 - 1     Salzburg  
Esbjerg     2 - 1     Standard Liège     
Wigan Athletic     1 - 2     Zulte-Waregem    
Paços de Ferreira     0 - 0     Fiorentina  
Dnipro Dniprop…     4 - 1     Pandurii Târgu Jiu   
Bordeaux     0 - 1     Eintracht Fran…     
APOEL     0 - 0     Maccabi Tel Aviv    

Coastal yatangulia fainali za Uhai Cup, Yanga Mtibwa leo Chamazi

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSx_mC8rkrCPXVUDkI9jy-egKmdMWQlJNs_n5V9mel7Qf8Y8CEU9-Kn9E2eAPBwPow6xtMWl7FR1pOor-aV1buaiaHDDHVmNd9WJwqKMquGw1gkvFRDHdDJpf95Mqdet4APsogR0XwyzY5/s1600/Uhai+Cup+Logo-1.jpg
TIMU ya vijana ya Coastal Union ya Tanga, jana ilifanikiwa kutangulia Fainali za u20 Uhai Cup baada ya kuwavua ubingwa Azam kwa kuinyuka bao 1-0. katika pambano la Nusu Fainali ya kwanza ya michuano hiyo inayochezwa kwenye uwanja wa Chamazi, neje kidogo ya Dar es Salaam.
Bao pekee la Wagosi wa Kaya jana lilifungwa na mshambuliaji Yussuf Chipo dakika ya 32 na sasa timu hiyo ya Tanga inasubiri mshindi kati ya Yanga SC, na Mtibwa Sugar mechi inayochezwa leo kwenye nusu fainali ya pili.
Ushindi huo wa Coastal ni muendelezo wa ubabe wake kwa Azam kwani katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya mwaka huu, waliishinda mabao 2-1 na kulipa kisasi cha kulazwa katika fainali zilizopita ambapo Azam walitwaa taji hilo.
Coastal sasa inasubiri kujua itacheza na ni siku ya Jumapili kati ya Yanga au Mtibwa ambazo zitaumana jioni ya leo.
Yanga ilitinga Nusu Fainali juzi baada ya kuichapa Ashanti United kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa  kwenye Uwanja wa Azam Complex, huku Mtibwa ikiizima Simba kwa mabao 3-2.

Kili Stars yaanza kwa sare dhidi ya Chipolopolo, Uganda kuanza kutetea taji

Na Somoe Ng'itu, Nairobi
KILIMANJARO Stars imeanza michuano ya Kombe la Chalenji kwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopo) ambayo nchi yao inashika nafasi ya 72 katika viwango vya Fifa duniani vilivyotangazwa jana.
Timu hiyo ya Tanzania Bara ambayo nyota wake pamoja wa Zanzibar Heroes huunda timu ya Taifa (Taifa Stars), ilikuwa ya kwanza kufungwa kipindi cha kwanza kabla ya kipindi cha pili kusawazisha.
Chipolopolo inashiriki michuano  inayoandaliwa na Shirikisho la Sola la nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kama timu alikwa.
Mechi hiyo ya Kundi B, ilianza kwa dakika ya pili ya mchezo, mshambuliaji Elias Maguli kupenyeza pasi safi kwa Salum Abubakar 'Sure Boy' lakini kipa Nsabata Toaster wa Zambia alipangua kishujaa shuti la kiungo huyo wa Azam FC.
Katika dakika ya 22, winga hatari mwenye mabao sita Yanga msimu huu, Mrisho Ngasa, alikokota mpira hadi ndani ya boksi la Zambia, lakini akapiga shuti nje ya lango. Katika mchezo wa mwisho dhidi ya Zambia uliokuwa wa kirafiki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka jana, Ngasa aliifungia Timu ya Taifa (Taifa Stars) bao pekee katika ushindi wa 1-0.
Ngasa alipiga shuti pia katika dakika ya saba ya mchezo wa jana, lakini lilidakwa na kipa Toaster.
Zambia walipata bao katika dakika ya 41 lililodumu kipindi chote cha kwanza kupitia kwa Ronald Kampamba aliyemalizia krosi murua ya mkongwe, Felix Katongo.
Kili Stars walitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini waliponzwa na umaliziaji duni huku Zambia wakipiga mpira wa pasi fupi fupi laki jitihada zao zilikwamishwa na kipa Ivo Mapunda aliyeokoa michomo mingi langoni.
Beki Said Morad aliisawazishia Tanzania Bara dakika tatu baada ya kipindi cha pili kuanza akiunganishwa kwa kichwa kona safi iliyochongwa na Sure Boy ambaye alitangazwa mchezaji bora wa mchezo huo.
Ngasa alitaka kusahihisha makosa alipoachia shuti kali lakini likapanguliwa kishujaa na kipa Toaster.
Dakika ya 82 Haroun Chanongo alipiga shuti likadakwa.
Kwa matokeo hayo Burundi anaongoza Kundi B baada ya kuilaza Somalia kwa mabao 2-0 katika mechi ya awali iliyochezwa mchana kwenye uwanja huo.
Michuano hiyo itaendelea leo saa 8:00 mchana kwa Sudan kucheza dhidi ya Eritrea, mchezo utakaofuatwa na Uganda dhidi ya Rwanda saa 10:00 alasiri kwenye Uwanja wa Machakos.
Jumamosi Zanzibar Heroes itaumana na Ethiopia kwenye Uwanja wa Nyayo katika mchezo wa utangulizi na baadaye Sudan Kusini itapambana na Kenya kwenye uwanja huo huo.
Kili Stars itacheza mchezo wa pili dhidi ya Somalia Jumapili kuanzia saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Nyayo wakati Zambia itamenyana na Burundi kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10:00 jioni siku hiyo.
Kili Stars iliwachezesha: Ivo Mapunda, Erasto Nyoni, Said Morad, Kelvin Yondani, Himid Mao, Frank Domayo, Salum Abubakar 'Sure Boy'/ Ramadhani Singano 'Messi' (dk 88), Hassan Dilunga/ Athuman Idd 'Chuji' (dk 85), Mrisho Ngasa, Elias Maguli/ Haroun Chanongo (dk 72) na Amri Kiemba.
Zambia: Nsabata Toaster, Bronson Chama, Jimmy Chisenga/ Kabaso Chongo (dk 67), Christophe Munthali, Rodrick Kabwe, Stanley Nshimbi/ Alex Nyonga (dk 57), Sydney Kalume, Kondwani Mtonga, Felix Katongo/ Salalani Phiri (dk 73), Ronald Kampamba na Festus Ndewe.