STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 17, 2015

'MANYIGU' WA KAGAME KUWAPIMA STARS MABORESHO

AMAVUBI watakaokuja nchini Januari 21 kucheza na Stars Maboresho
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhX82vKFmbU_azF2jw6Sh1OefY0VH4MPXgegGJAQLnMmy6vNVnrI-U7UR0pkyKYfPWcecYEI-bvfVbXjelpAhelaeNjL5YqxsymlHKKyZfOv0aYMdCY5xQTD_WZWSuDm41Tr1kDs1jbA_yU/s1600/maboresho.png
Stars maboresho wanaotarajiwa kuvaana na Amavubi Januari 22
KIKOSI cha timu ya taifa ya Rwanda 'Amavubi' (Nyigu) wanatarajia kutua nchi katika kati ya wiki ijayo kuipima ubavu timu ya Taifa Stars Maboresho.
Tayari Kocha Mkuu wa Stars, Mart Nooij ameteua kikosi cha wachezaji 26 wa timu hiyo kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Januari 22, mwaka huu.
Nooij alisema kati ya wachezaji hao 10 ambao wanatoka katika mikoa ya kanda ya ziwa wataweka kambi Mwanza na wengine 10 wanaotoka upande wa Dar es Salaam wataweka kambi hapo Dar es Salaam.
Alisema kambi kwa ajili ya michuano hiyo itaanza rasmi kesho Jumapili  na siku inayofuata watakwenda Mwanza kuungana na wengine kwa ajili ya kambi ya pamoja.
“Mechi hiyo ni muhimu kwetu kwani wachezaji ambao watafanya vizuri tutawapandisha kucheza katika kikosi kikubwa,”alisema Nooij.
Nooij aliwataja wachezaji wa kikosi hicho kuwa ni; Aishi Manula, Benedict Tinoko, Miraji Adam, Andrew Vicent, Michael Gadiel, Emmanuel Semwanda, Joram Mgeveke, Edward Charles na Adam Salamba.
Wengine ni; Aboubakary Mohammed, Hassan Dilunga, Hussein Malombe, Shiza Ramadhani, Omari Nyenje, Kelvin Friday, Alfred Masumbakenda, Salim Mbonde, Atupele Green na Rashid Mandawa.
Pia wamo Manyika Peter, Salum Telela, Hassan Banda, Mohammed Hussein, Said Ndemla, Said Makapu na Simon Msuva.
Aidha,  kwa mujibu wa taarifa ya Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Soka Tanzani (TFF), Vedastus Lufano, kiingilio kwenye mechi hiyo itakuwa sh. 20,000 kwa viti maalumu (VIP), viti vya kawaida sh. 10,000 na mzunguko ni sh. 3,000.
Lufano aliwataja baadhi ya wachezaji wa Amavubi wanaotarajia kutua jijini Mwanza Januari 21 kwa ndege ya Rwanda Air, kuwa ni Marcel Nzarora, Olivier Kwizera, Sotel Kayomba, Ismail Nshutiyamagala , Emery Basiyenge na Michel Rushengoga.
Wengine ni Fitina Ombolenga, Janvier Mutijima, Haruna Niyonzima, Tean Baptista, Mugiraneza Savio, Nshuti Dominique, Patrick Sibomano, Jean Claude, Zagabe Andrew, Buteara Ernest , Sugira Danny, Ushengimana Betramed Iladukunda na Blenvue Mugenzi.
Lufano aliongeza kuwa taarifa iliyotumwa TFF kutoka Rwanda, Amavubi itaongozana na viongozi waliotajwa kuwa ni Stephen Costan, Vincent Mashami, Ibrahim Mugisha, Moussa Hakizimana, Nuhu Assouman, Boume Mugabe, Piere Baziki na Mkuu wa Msafara Bandora Felician.
Awali, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) Boniface Wambura alisema mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa  wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN). 
Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.

KIVUMBI CHA AFCON KUTIMKA HIVI KUANZIA LEO

MASHINDANO ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, yanaanza rasmi leo nchini  Guinea ya Ikweta kwa nchi 16 wakiwamo wengine kuanza kuichuana kuwania taji lisilo na mwenyewe baada ya Nigeria kushindwa kufuzu.
Michuano hiyo iliyohamishiwa Guinea ya Ikweta baada ya waliokuwa wawe wenyeji wa fainali za 2015, Morocco kuchomoa kwa kisingizio cha kuhofia ugonjwa Ebola ina makundi manne yenye timu 4 kila mmoja.
Timu mbili za juu ndizo zitakazofanikiwa kufuzu robo fainali na miji minne ndiyo inayotumika katika fainali hizo ambayo ni mjini mkuu Malabo, Bata, Mongomo na Ebebitin.
Makundi yapo kama ilivyo hapo chini;
http://www.diskifans.com/wp-content/uploads/2014/12/CAF-620x274.jpg
VIWANJA:
-Estadio de Bata, Mjini Bata, Watazamaji 37,500
-Nuevo Estadio de Malabo, Malabo, Watazamaji 15,250
-Estadio de Mongomo, Mongomo, Watazamaji 10,000
-Nuevo Estadio de Ebebiyín, Ebebitin, Watazamaji 5,000

Leo Jumamosi kutakuwa na michezo miwili ya ufunguzi ya Kundi A ambapo mechi ya awali itawakutanisha wenyeji Guinea ya Ikweta (Equatorial Guinea) dhidi ya mabingwa wa mwaka 1972, Congo Brazzaville watakapocheza kwenye uwanja wa Bata Mjini Bata na kufuatia Mechi ya Burkina Faso na Gabon Uwanjani hapo hapo.
Kesho Jumapili ratiba inaonyesha ni zamu ya timu za Kundi B ambapo mabingwa wa mwaka 2012 Zambia wataumana na DR Congo na usiku itakuwa zamu ya mabingwa mara tatu wa fainali hizo Tunisia dhidi ya wageni wa michuano hiyo Cape Verde.
Ratiba inaonyesha kila siku kuanzia leo kutakuwa na michezo mwili  na Fainali zake zitachezwa Februari 8 kwenye uwanja wa Bata, mjini Bata ambapo Afrika itashuhudia na kumtambua bingwa mpya wa AFCON.
Wenyeji Guinea ya Ikweta hii ni mara yao ya pili kuanza fainali hizo kwani mwaka 2012 waliziandaa kwa kushirikiana na majirani zao Gabon ambao safari hii wamepangwa kundi moja pamoja nao.
AFCON 2015:RATIBA
Jumamosi Januari 17

19:00 Equatorial Guinea v Congo [Estadio de Bata]
22:00 Burkina Faso v Gabon [Estadio de Bata]

Jumapili Januari 18
1900 Zambia v Congo DR [Nuevo Estadio de Ebebiyín]
2200 Tunisia v Cape Verde Islands [Nuevo Estadio de Ebebiyín]

Jumatatu Januari 19
1900 Ghana v Senegal [Estadio de Mongomo]
2200 Algeria v South Africa [Estadio de Mongomo]

Jumanne Januari 20
1900 Côte d'Ivoire v Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]
2200 Mali v Cameroon [Nuevo Estadio de Malabo]

Jumatano Januari 21
1900 Equatorial Guinea v Burkina Faso [Estadio de Bata]
2200 Gabon v Congo [Estadio de Bata]

Alhamisi Januari 22
1900 Zambia v Tunisia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]
2200 Cape Verde Islands v Congo DR [Nuevo Estadio de Ebebiyín]

Ijumaa Januari 23
19:00 Ghana v Algeria [Estadio de Mongomo]
22:00 South Africa v Senegal [Estadio de Mongomo]

Jumamosi Januari 24
1900 Côte d'Ivoire v Mali [Nuevo Estadio de Malabo]
2200 Cameroon v Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]

Jumapili Januari 25
21:00 Gabon v Equatorial Guinea [Estadio de Bata]
21:00 Congo v Burkina Faso [Nuevo Estadio de Ebebiyín]

Jumatatu Januari 26
21:00 Congo DR v Tunisia [Estadio de Bata]
21:00 Cape Verde Islands v Zambia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]

Jumanne Januari 27
21:00 South Africa v Ghana [Estadio de Mongomo]
21:00 Senegal v Algeria [Nuevo Estadio de Malabo]
Jumatano Januari 28
21:00 Cameroon v Côte d'Ivoire [Nuevo Estadio de Malabo]
21:00 Guinea v Mali [Estadio de Mongomo]

ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 31

19:00 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Estadio de Bata]==RF1
22:00 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nuevo Estadio de Ebebiyín]==RF2

Jumapili Februari 1
19:00 Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Estadio de Mongomo]==RF3
22:00 Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Nuevo Estadio de Malabo]==RF4
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 4

22:00 RF 1 v RF4 [Estadio de Bata]==NF1

Alhamisi Februari 5
22:00 RF2 v RF3 [Nuevo Estadio de Malabo]==NF2

MSHINDI WA 3
Jumamosi Februari 7

21:00 Aliefungwa NF1 v Aliefungwa NF2 [Nuevo Estadio de Malabo]

FAINALI
Jumapili Februari 8

22:00 Mshindi NF1 v Mshindi NF2 [Estadio de Bata]