STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, September 11, 2013

Walimu wajiandaa kugoma tena, kisa deni lao la Sh Bil 33

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLy8pkk8A5UEzHJnD7gZMhQ25ia2Z2aWm3mWxyySq1BfXEhznl2nxMyd3ae2xtH8Zp78t_p5qDcFAJvzos2YCXtMVmmm_cWM8NLFz25_QgYOtKbEyqhKG8ZOOG_Agk1Wg4xJHaTmpR_0hq/s640/1.jpg
WALIMU nchini wameipa serikali muda wa mwezi  mmoja kabla ya kuingia tena kwenye mgomo kwa ajili ya kushinikiza walipwe malimbikizo ya madeni yao yanayofikia Sh. Bilioni 33.
Tishio hilo limetolewa na uongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambapo kimesema kinatoa muda wa mwezi mmoja tu kwa serikali kuweza kulipa fedha hizo la sivyo wataingia kwenye mgomo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais wa chama hicho, 
Gratian Mukoba, alisema wamechoka kupewa ahadi hewa na serikali ndio maana wamefikia hatua hiyo.

‘Tumetoa mwezi huu wa tisa uwe wa mwisho kuililia serikali, baada ya hapo tutaamua hatua gani tufanye, maana tumekutana na makatibu wakuu wa wizara zinazowahudumia walimu lakini bado tunaishia kupewa ahadi hewa,” alisema Mukoba.

Mukoba aliongeza kuwa Agosti 14, mwaka huu, walikutana na makatibu wakuu wanaowahudumia walimu pamoja na Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma, wakatakiwa kuwasilisha madai yao yote.

“Tulikutana na makatibu, katika kikao hicho, tuliwafahamisha kuwa walimu wanaidai serikali zaidi ya sh bilioni 33 na mwisho wa kikao hicho tulikubaliana CWT iwakilishe madai hayo ndani ya wiki mbili,” aliongeza Mukoba.

Mukoba alisema wiki mbili zilipofika, walienda kuonana tena na Katibu Mkuu, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kuwasilisha vitabu vyenye madai mbalimbali ya walimu.

“Madai hayo tuliyaambatanisha kwenye barua Na CWT/004/UTMS/VOL.11/94 na madai hayo sasa yamefikia sh bilioni sita,” alisema Mukoba.

Mukoba aliishangaa serikali kuanzisha Mpango wa Matokeo Makubwa sasa “Big Result Now”, huko walimu ambao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo, wana maisha magumu kutokana na mishahara kuwa midogo na kuzidi kwa malikimbizo ya madeni yao.

“Walimu ambao ndiyo watelekezaji wakuu wa mpango huu japo hawaelewi au hawajapewa semina elekezi, lakini ndio watekelezaji wakubwa.

Naishangaa serikali kuwadharau walimu na nakuhakikishia mpango huo hautafanikiwa kama walimu hawapati haki zao,” alisema Mukoba.

Mukoba aliionya serikali ikamilishe madai ya walimu ili wafanye kazi kwa moyo tofauti na sasa ambapo wengi wamekata tamaa.

‘‘Walimu wa nchi hii wamekata tamaa. Mioyo yao imekufa ganzi kwa sababu serikali imekataa kuwalipa malimbizo yao.

Kwa nini serikali imeamua kuwatendea jeuri walimu kiasi hiki?” alihoji Mukoba.

Kombe la Chalenji kupigwa Kenya Nov.

Musonye (kushoto) mbele ya Kombe la Chalenji
MICHUANO ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati mwaka huu imepangwa kufanyika kuanzia Novemba 22 hadi Desemba 8 nchini Kenya.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Nairobi, katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye, alisema kuwa tayari maandalizi ya mashindano hayo ya kila mwaka yameanza.

Musonye alisema kuwa anaamini nchi wanachama zitatumia mashindano hayo kuandaa timu zao kwa ajili ya michuano ijayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwaka 2015.
"Tumeshaanza maandalizi ya mashindano ya Chalenji na kwa asilimia mwenyeji atakuwa ni Kenya, taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa," alisema Musonye.

Alisema kuwa sekretarieti ya shirikisho hilo imeshaanza kuwasiliana na nchi wanachama ili kuandaa timu na kutuma majina ya waamuzi watakaokwenda kuchezesha michuano hiyo.

Rais wa KFF, Sam Nyamweya, alikaririwa akizungumza jijini Nairobi mwishoni mwa wiki akisema kwamba Kenya imejiandaa kuwa wenyeji wa michuano hiyo na wanaamini watafanya vizuri kuliko miaka iliyopita.
Nyamweya alisema kuwa michuano hiyo inatarajiwa kufanyika katika miji miwili ambayo ni Nairobi na Kisumu.

"Ila bado Kisumu hawajathibitisha kuwa wenyeji," alisema rais huyo ambaye mwaka jana alishuhudia Harambee Stars ikilala dhidi ya wenyeji, Uganda (The Cranes) katika mechi ya fainali kwenye uwanja wa Mandela uliopo Namboole.

Mara ya mwisho Kenya kuandaa mashindano hayo ilikuwa ni mwaka 2009 na michuano hiyo ilifanyika Nairobi na Kakamega.

Timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) mwaka jana ikiongozwa kwa mara ya kwanza na kocha Kim Poulsen, ilimaliza katika nafasi ya nne baada ya kufungwa na 'ndugu zao' Zanzibar Heroes kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.

CHANZO: NIPASHE

Wanafunzi Darasa la Saba waanza mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjT7UvQDBDmuLVn_p3H5eug8q68KSNsJew7-nXPZkWNTWzV8chyEsYyyTgkkoX7Su7X1IdCkfX0iTVkVnqrH3Pvz3j10-7TZD7kyYljop9BsIP9k4rtKp37uvPfTkzjBeVrTH9u8L9CgKc/s640/MITIHANI+YA+DARASA+LA+SABA+MORO+2.jpg
Kazi itakuwa kama hivi, wengine wanajaza wengine wakitafakari kwa kina katika mitihani iliyoanza leo kwa wahitimu wa darasa la 7 nchini

JUMLA ya wanafunzi 868,030 wa Darasa la Saba nchini, leo na kesho wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu yao ya msingi katika  michepuo miwili, wa Kiswahili na Kiingereza.

Mitihani hiyo imeanza asubuhi ya leo katikma shule mbalimbali nchini, ambapo kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, mtihani huo utakaojumlisha masomo matano, utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo na kesho Alhamisi.

Kati ya idadi hiyo ya wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani huo, wavulana ni 412, 105 sawa na asilimia 47, na wasichana 455, 925 sawa na asilimia 52.52. Jumla ya masomo matano yanatarajiwa kutahiniwa na wanafunzi hao ambayo ni pamoja na Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.

Kwa mujibu wa Mulugo, wanafunzi 844, 810 wanatarajia kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili, ambao kati yao wavulana ni 400, 335 na wasichana 444,575, huku 22, 535 watafanya kwa lugha ya Kiingereza, ambao wavulana ni 11, 430 ma wasichana 11, 105.

Mulugo alitaja kundi lingine la wanafunzi ambao wanakwenda kufanya mtihani kuwa ni pamoja na lile la wasioona ambao idadi yao ni 88, wavulana 56 na wasichana 32, huku wale wenye uoni hafifu na ambao wanahitaji maandishi makubwa ni 597.

Kati ya watahiniwa hao wenye uoni hafifu, wanaotarajia kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili ni 546, wavulana 263 na wasichana 283, na wale watakaofanya kwa Kiingereza ni 51, wavulana 21 na wasichana 30.

Alisema maandalizi yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa fomu maalumu za OMR za kujibia mtihani na nyaraka zote muhimu huku akiwaagiza maafisa elimu wa mikoa na halmashauri kuhakikisha mazingira yanakuwa tulivu na kuzuia mianya yote ya udanganyifu wa mitihani.

Mulugo pia aliwataka wasimamizi  kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.

Sambamba na hilo, aliwaasa wanafunzi wote kutojihusisha na vitendo vyovyote vya udanganyifu wa mtihani kwani watakaobainika kufanya hivyo watafutiwa matokeo yao yote ya mtihani.
MICHARAZO inawatakia kila la heri wanafunzi hao katika mitihani yao ili waweze kuifanya kwa amani na utulivu na ahatimaye wafaulu Inshallah.

Ajiua akijifanyia operesheni ya kujiondoa uvimbe tumboni

MKAZI mmoja wa kijiji cha Sadoto, Kata ya Sengarewa wilaya Ukerewe, amefariki dunia baada ya kujifanyia upasuaji wa kujiondoa uvimbe tumboni mwenyewe.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka wilayani humo, zinasema kuwa, Sitta Manoni mwenye umri wa miaka 44 alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na uvimbe tumboni, lakini hakuwa na uwezo wa kwenda kujitibia hospitalini na hivyo juzi aliamua kuchukua kiwembe na kujipasua uvimbe huo.
Hata hivyo mashuhudu wa tukio hilo wamedokeza kuwa mara baada ya kujifanyia operesheni hiyo ya 'kienyeji' majirani zake waliamua kumkimbiza hospitalini baada ya kumuona yupo kwenye hali mbaya na kufariki njiani.

Serikali yamkumbuka Mzee Gurumo

IMG_6952Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi. Lilly Beleko kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akimkabidhi Mzee Muhidini Gurumo barua kama ishara ya Serikali kutambua mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki nchini pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi kazi hiyo, hivi karibuni nyumbani kwake Makuburi, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ya Mkurugenzi ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Bw. Addo Mwasongwe na kulia pembeni ya Mzee Gurumo ni Mkewe, Bibi. Pili Said Kitwana.IMG_6981Nguli wa Muziki wa Dansi, Mzee Muhudini Gurumo (aliyevaa shati la drafti) akiwa na watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, walipomtembelea nyumbani kwake Makuburi Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Serikali kupitia Wizara hiyo ilimkabidhi barua rasmi Mzee huyo kutambua mchango wake katika tasnia ya Muziki na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi Lilly Beleko, wa pili ni mke wa Mzee Gurumo, Bibi. Pili Said Kitwana na wa Pili Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara Upande wa Sanaa, Bibi. Joyce Hagu. Picha zote na Concilia Niyibitanga Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
………………..
Na Concilia Niyibitanga- WHVUM
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imempongeza Mzee Muhidini Gurumo kwa mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki nchini pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo.
Akiwasilisha barua ya Serikali ya kutambua mchango wa nguli huyo juzi nyumbani kwake Makuburi Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Lilly Beleko amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini  mchango wake katika muziki wa Dansi hapa nchini.
‘Serikali inathamini mchango wako katika Muziki hapa nchini na itaendelea kuzienzi kazi hizo na inakupongeza kwa kazi nzuri ulioifanya ya kuelimisha, kuhamasisha na kuburudisha jamii’. Amesema Bibi. Beleko.
Naye Rais wa Shirikisho la Muziki nchini, Bw. Addo Mwasongwe, amesema kuwa Shirikisho linampongeza kwa kazi zake nzuri na litaendelea kumtumia katika kazi za muziki ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri katika tasnia hiyo.
Nguli huyo wa muziki wa dansi nchini katika enzi zake za uimbaji ametunga nyimbo za kuelimisha jamii kufanya kazi kwa bidii, kudumisha usawa, amani na kuwakumbusha wazazi kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto katika maadili mema.
Mzee Gurumo ambaye ameanza kazi ya muziki mnamo miaka ya 1960 na kustaafu kazi hiyo mwaka huu amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kutambua kazi yake na amefarijika kwa kukabidhiwa barua ya kumtambua na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo.

Kili Music Tour 2013 kuhitimishwa kwa kishindo Dar J'Mosi


 Hitimisho la Kili Music Tour 2013.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusiana na tamasha kubwa la "Kili Music Tour litakalofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, ambapo kiingilio kitakuwa sh. 2500 pamoja na  bia moja ya bure. (Picha na Francis Dande)
 Ben Pol akizungumza kuhusu tamasha hilo.
 Nasib Abdul 'Diamond Platinum'
Kala Jeramiah