STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 3, 2014

Je, unalikumbuka kundi la Kaole Sanaa? Basi kaaeni chonjo

Issa Kipemba aliyekuwa akicheza kama Mshakunaku
Kingwendu Kingwendulile
Davina

Hii achana nayo, Issa Kipemba nouma

Issa Kipemba, Chini ni kazi yake mpya iliyopo njiani siyo ya kuikosa hii

Yanga kuivaa Al Ahly Cairo bila mashabiki

MAMLAKA za usalama nchini Egypt katika jiji la Cairo zimewaonya mashabiki wa Al Ahly kutoingia katika uwanja Cairo kuhudhuria mechi ya raundi ya pili ya CAF Champions league kati ya Al Ahly dhidi ya Young Africans S.C.  itakayochezwa mnamo March 9.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumapili, polisi wa Cairo walisema kwamba itapambana na jaribio lolote la mashabiki kujaribu kuingia uwanjani.

Azmi Megahed, msemaji wa FA ya Misri, alisema raia hawatoruhusiwa kuhudhuria mechi hiyo kutoka sababu za kiusalama.

Jumamosi wiki iliyopita, polisi walipambana na mashabiki wa Zamalek White Knights ambao walijaribu kuingia katika uwanja wa Cairo kuangalia mchezo kati ya Zamalek dhidi ya mabingwa wa Angola Cabo Schrob. Fujo hizo zilipelekea kwa kukamatwa kwa mashabiki 33.
SHAFIH DAUDA

Kumekucha Sikinde ebu sikia vibao vyao vipya

Baadhi ya waimbaji wa Sikinde
Baadhi wa wapuliza ala za upepo, Hamis Mirambo na Mbaraka Othman
BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Wana Sikinde Ngoma ya Ukae' imekamilisha vibao vyake vitatu vipya kwa ajili ya albamu yao mpya ya 'Jinamizi la Talaka'.
Kibao cha kwanza cha Jinamizi la Talaka baadhi yenu mmeshaushikia katika vituo vya redio kwa vile ulirekodiwa toka mwaka jana, lakini vingine viwili vya Mkwezi na Deni Nitalipa mtakuwa hamjavisikia.
Wala usichokechungulia hapa mtandao wao wa https://www.hulkshare.com/sikinde, ambapo unaweza kuzisikiliza Online na kutoa maoni ama ushauri ili kuboresha ama kufanyia marekebisho nyimbo hizo kabla ya kuzinduliwa rasmi wakati wa kuadhimisha miaka 36 tangu kuanzishwa kwake.

Maajabu! Chatu amzidi ujanja Mamba

 Nyoka huyo alijipinda kwa Mamba na kumbana hadi akafa
 Nyoka alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji
 Chatu huyo alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi
Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC
"Tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumbana mamba hasa katika sehemu ya miguu ya ili kumdhibiti.''
"Pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kuanza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua nyoka muda wa robo saa kumla mamba huyo.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu saa 5. Hatimaye wote walionekana kuchoka.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.
BBC SWAHILI

Mkenya Lupita Nyong'o aweka historia anyakua tuzo ya Oscar


Lupita Nyong'o akiwa na tuzo yake


Lupita akishow kwenye red carpet
MKENYA Lupita Nyong'o, ameweka historia baada ya kufanikiwa kunyakua tuzo maarufu duniani ya Oscar.

Tuzo hizo za 86 za Academy Awards 2014 maarufu kama oscars zilifanyika Dolby Theathre pande za Hollywood 
Mshiriki pekee toka pande za Afrika Mashariki, Mkenya Lupita Nyong’o ndiye ametunyanyua ile kinoma noma baada ya kuondoka na tuzo katika kipengele cha best supporting actress kupitia movie yake ya '12 Years a Slave'

Lupita ambaye aliwashinda waigizaji wenzie kama Jennifer Lawrence kupitia movie yake ya American hustle , Sandra Burlock kupitia movie yake ya Gravity, Lupita alipata shangwe za hatari wakati jina lake linatajwa kuwa mshindi wa tuzo hizo.
Hongera Lupita Nyong'o Watz mpooooo?!

Pambano la Simba, Ruvu laingiza Mil 20

PAMBANO la Ligi Kuu ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana (Machi 2 mwaka huu) imeingiza sh. 20,610,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,143,898.31.
Katika mchezo huo Simba iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na kuendelea kusalia kwenye nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Azam yenye pointi 40 na kufuatiwa na Yanga yenye 38 kisha Mbeya City inayokamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36.
Katika hatua nyingine mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Mlale JKT na Lipuli iliyokuwa ichezwe Machi 9 mwaka huu Uwanja wa Majimaji mjini Songea sasa itachezwa Machi 5 mwaka huu.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko hayo ili kuipunguzia gharama timu ya Lipuli ya Iringa ambayo jana (Machi 2 mwaka huu) ilicheza mechi mjini Songea dhidi ya Majimaji.


Yanga, Al Ahly zavuna Mil. 488/- Taifa

MBIOOOO
MECHI ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.
Mapato hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh. 35,000. Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000.
Uwanja sh. 50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.

Stars yatua salama Namibia

KIKOSI cha Taifa Stars kimeondoka leo alfajiri kwenda Windhoek, Namibia kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji itakayochezwa Machi 5 mwaka huu.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ina msafara wa watu 25 unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Timu imefikia hoteli ya Safari jijini humo.
Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Sam Nujoma, na kikosi cha Taifa Stars kipo chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi ambaye ana leseni A ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Namibia (Brave Warriors) inayofundishwa na kocha Ricardo Mannetti imeingia kambini jana (Machi 2 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo ambayo tiketi zake zilianza kuuzwa Februari 28 mwaka huu.