Nyoka alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji
Chatu huyo alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi
Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo
lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa
kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC
"Tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumbana mamba hasa katika sehemu ya miguu ya ili kumdhibiti.''
"Pambano
lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu
ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kuanza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua nyoka muda wa robo saa kumla mamba huyo.
''Bila shaka
Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,''
alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine
aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao
wawili walipambana kwa karibu saa 5. Hatimaye wote walionekana kuchoka.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment