Wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola, alisema Straika huyo ambaye mkataba wake na PSG imeisha hakuna anayejua atatua wapi na hivyo mashabiki wasubiri kushtukizwa tu.
Nahodha huyo wa Sweden mwenye miaka 34, kwa sasa anaendelea na maandalizi ya kuiongoza timu yake katika michuano ya Fainali za Kombe la Ulaya itakayoanza Juni 10 nchini Ufaransa.
"Sidhani kama atajiunga na United, na wala hakuna anayelala Sweden kwa sasa hakuna anayejua kitakachotokea," alisema Raiola.
Wakala huyo alisema bila shaka mwisho wa yote watu watashangazwa na maamuzi ya mkali huyo kwa klabu atakayojiunga nayo kwa msimu ujao.
"Bado hatuajamua, lakini itashangaza wengi mwishowe. Watu wanazungumza kuhusu United, ila ukweli utafahamika tu na ndio maana hatusemi mengi kwa waandishi wasubiri waone wenyewe," alisema wakala huyo.