Mosoti |
Zakaria Hanspoppe |
Simba imemlipa Mosoti fedha zake za malimbikizo ya usajili na fidia nyingine zinazokaribia Sh Milioni 64.2 Mei 19 mwaka huu ikiwa ni wiki moja na ushei kabla ya siku ya mwisho waliyopewa na FIFA kabla ya kuchukuliwa hatua za kukiuka maamuzi ya Baraza la Usuluhishi la klabu Shirikisho hilo la Dunia.
Kabla ya Simba kulipa fedha hizo ambazo Mosoti amethibitisha kupata taarifa mapema wiki hii, Yanga kupitia Msemaji wake, Jerry Muro, ilitaka Simba iwapelekee nyaraka za deni inalodaiwa na Mosoti ili walipe kupitia Mamilioni ya fedha walizovuna kupitia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.
Siku chache baada ya Muro kutoa kauli hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Zakaria Hans Poppe alisema klabu yao ina uwezo wa kulipa fedha hizo na isingehitaji msaada kutoka kokote.
Mosoti aliiburuza Simba FIFA kutokana na kuvunja mkataba wake wa kuichezea klabu hiyo kienyeji na hata ilipotolewa hukumu ya kumlipa Mkenya huyo, Simba ilipuuza ndipo mapema mwezi huu FIFA iliiagiza TFF kuilazimkisha Simba imlipe Mosoti ndani ya mwezi mmoja la sivyo Iishushe Daraja na yenyewe (TFF) itafungiwa kwa michuano ya kimataifa, jambo ambalo lingeizuia Yanga kucheza hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.
No comments:
Post a Comment