STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 25, 2014

Kun Aguero apiga hat trick akiibeba City ktk FA Cup

Sergio Aguero
Kun Aguero akiokota mpira nyavuni baada ya kufunga leo hat trick kwenye FA Cup
MSHAMBULIAJI aliyerejea tena dimbani baada ya kuwa nje kutokana na majeraha, Sergio kun Aguero, ameendeleza moto wake wa kufumania nyavu baada ya kuifungia Manchester City mabao matatu (hat trick) wakati wakiiangamiza Watford kwenye mechi ya raundi ya nne ya Kombe la FA.
City waliokuwa nyumbani walitanguliwa kufungwa mabao mawili ya haraka kupitia kwa Forestieri dakika ya 21 na Deeney dakika ya 30 na kudumua hadi mapumziko wenyeji wakiwa nyuma katika uwanja wa Etihad.
Hata hivyo kipindi cha kilianza kwa City kupigana kiume kurejesha mabao moja baada ya jingine, Kun akifunga dakika ya 60 na Aleksander Kalarov kusawazisha dakika ya 79 na Kun kuongeza mengin mawili dakika ya 87 na 93.
katika mechi nyngine za michuano hiyo Arsenal ilipata ushindi mnono mapema jana kwa kuizabua Coventry City kwa mabao 4-0, huku Nottingham Forest ikilazimishwa suluhu na Preston North End, AFC Bournemouth ikiwa nyumbani ilinyukwa na Liverpool kwa mabao 2-0, Sunnderland ikaendeleza makali yake kwa kuilaza Kidderminster kwa bao 1-0, Southampton ikashinda nyumbani kwa mabao 2-0 dhidi ya Yeovil Town na Huddersfield Town ililala kwao bao 1-0 dhidi ya Charlton Athletic.
Mechi nyingine za raundi hizo zilizochezwa pia leo zilishuhudia Hull City ikishinda ugenini 2-0 dhidi ya Southend Utd na Swansea City nayo ikishinda ugenini 2-1 dhidi ya Birmingham City, Wigan Athletic ikiishinda nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya Sheffield Wednesday.

Nigeria yaiduwaza Morocco, ikitinga nusu fainali CHAN 2014

http://en.starafrica.com/football/files/2014/01/B14AKCR14441.jpg
TIMU ya soka ya Nigeria imeiduwaza Morocco baada ya kuing'oa kwenye michuano ya CHAN 2014 baada ya kuifunga mabao 4-3 katika muda wa dakika 120 ya pambano la kwanza la Robo Fainali  ya kwanza kwenye uwanja wa Cape Town.
Nigeria iliyoonekana kama inaondoka kwenye michuano hiyo ililazimisha mchezo huo kwenda kwenye dakika hizo baada ya kuchomoa bao dakika za lala salama za dakika 90 na kufanya matokeo kuwa 3-3 na kuongezewa dakika 30 zilizowapa ushindi.
Katika muda wa dakika 90,  Morocco walitangulia mabao yake yake matatu  katika kipindi cha kwanza kupitai kwa Moutouali aliyefunga mawili katika dakika ya 33 na 40, Iajour dakika ya 37.
Kipindi cha pili Nigeria ilitulia na kuanza kurejesha bao moja baada ya jingine kupitia kwa  Uzochukwu aliyefunga dakika nne baada ya kuanza kwa kipindi hicho kabla ya Ali kuongeza la pili dakika ya  55 na Uzoenyi kusawazisha dakika ya 90 na kufanya mchezo kuongezwa dakika 30.
Katika muda huo wa nyongeza, Nigeria ilipata bao lake lililoivusha hadi nusu fainali ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tatu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008, liliwekwa kimiani na Abubakar Ibrahim katika dakika ya 111.
Robo fainali ya pili ya michuano hiyo inatarajiwa kuanza hivi punde kwa pambano kati ya Zimbabwe dhidi ya Mali mchezo utakaochezwa uwanja huo huo wa Cape Town.

Babi aianza vyema Ligi ya Malaysia UiTM yashinda ugenini

Abdi Kassim akiwa na wachezaji wenzake baada ya gemu yao ya jana
KIUNGO Abdi Kassim 'Babi' aliiongoza vyema klabu yake ya UiTM ya Malaysia kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kuala Lumpur SPA katika mechi za fungua dimba ya  Ligi Kuu ya nchi hiyo iliyoanza rasmi jana.
UiTM ikiwa ugenini ilipata ushindi huo ikiwa ni siku chache baada ya kunyukwa mabao 3-2 katika michuano ya FA, huku Babi akihusika na mabao yote ya timu yake.
Akizungumza na MICHARAZO toka Malaysia, Babi alisema pambano hilo la jana lilikuwa gumu na lenye ushindani na wanashukuru kuanza kwa ushindi katika ligi hiyo na kuifanya timu yao ikamate nafasi ya tano kwenye msimamo huo.
Babi alisema kikosi chao kinatarajiwa kushuka tena dimbani Jumatatu dhidi ya timu ya Johor pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Mini UiTM.
Katika mechi nyingine za fungua dimba za Ligi Kuu ya Malaysia, Felda United ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 na PBAPP, Negeri Sembilan iliishindilia DRB-Hicom kwa mabao 2-1 kwenye uwanja wake wa nyumbani, huku Kedah ikiwa nyumbani kuisasambua Perlis kwa mabao 4-1, Johor ilala nyumbani kwa mabao 3-1 kipigo walichopewa na PDRM na Pulau Pinang ilipata ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Sabah.








































Ronaldo, Benzema waipeleka Madrid kileleni Spain

 Real Madrid vs. Granada: La Liga Live Score, Highlights, Report
MABAO mawili ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Mchezaji Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo na Karim Benzema yameiwezesha Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Grenada katika pambano la Ligi Kuu ya Hispania.
Madrid walikuwa uwanja wa nyumbani na kujikuta wakibanwa hadi mapumziko wakiwa 0-0 na wageni wao kabla ya kipindi cha pili Ronaldo kufungua pazia kwa bao la dakika ya 56 kabla ya Benzema kuongeza la pili dakika ya 74.
Kwa ushindi huo Madrid imefikisha jumla ya pointi 53 na kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiziengua timu za Barcelona na Atletico Madrid zenye pointi 51 kila moja.





Duru la pili laanza kwa kishindo, Yanga yaiua tena Ashanti

Mrisho Ngassa akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Ashanti United katika mechi yao ya leo Taifa
Mbeya City na Kagera Sugar kabla ya pambano baina yao

Coastal Union ilipokuwa ikiumana na Oljoro uwanja wa Mkwakwani Tanga

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imedhihirisha haikwenda Uturuki kutalii baada ya kuinyuka Ashanti United kwa mabao 2-1, huku wazee wa Oman, Coastal Union ya Tanga ikijikuta ikilazimishwa sare ya 1-1 na Oljoro JKT katika mechi za fungua dimba la duru la pili la Lligi hiyo.
Yanga ilikwaruzana na Ashanti kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kipindi cha kwanza kiliisha bola timu hizo kushindwa kufungana.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa dakika ya 51 Didier Kavumbagu akimalizia pasi ya Simon Msuva aliyegongeana na Haruna Niyonzima, hata hivyo dakika chache baadaye Ashanti walirejesha bao hilo kupitia Mnigeria Dayton Obinna.
David Luhende aliyepamba mbele aliihakikishia Yanga ushindi wa mabao 2-1 baada ya kufunga bao la pili kwa shuti la karibu ndani ya lango ya Ashanti katika dakika ya 79.
Kwa ushindi huo Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni kwa kufikisha pointi 31 ikifuatiwa na Azam ambayo ilianza duru hilo kwa kishindo kwa kuilaza Mtibwa Sugar mabao 1-0 katika pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Bao hilo pekee liliwekewa kimiania na Kipre Tchetche akimalizia kazi ya Joseph Kimwaga na kuendeleza rekodi yao ya kutopotea mechi kwenye ligi hiyo na kuzidi kuipumulia Yanga kileleni ikitopfautiana nao kwa pointi moja tu.
Nayo Mbeya City iliendeleza rekodi yao ya kushinda kokote inapoenda kucheza kwenye ligi hiyo baada ya kuiduwaza Kagera Sugar kwa kuilaza bao 1-0 uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Katika mechi nyingine ya leo kwenye ligi hiyo iliyochezwa mjini Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani, Coastal iliyokuwa Oman ikijifua ilishindwa kulinda bao lao baada ya Oljoro JKT kusawazisha bao dakika za jioni ya kuzifanya hivyo hizo zigawane pointi moja moja.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mechi mbili Simba kuikaribisha Rhino Rangers ya Taboira kwenye uwanja wa Taifa na JKT Ruvu kuialika Mgambo JKT kwenye uwanja wa Chamazi.