|
Mratibu wa shindano la Redd's Miss Vyuo Vikuu Tanzania, Agnes Mathew |
|
Ney wa Mitego atakayenogesha shindano hilo Ijumaa ijayo |
|
Rich Mavoko naye atakuwepo siku hiyo |
JUMLA
ya warembo 16 wanatarajiwa kuchuana kuwania taji la urembo la Redds
Miss Vyuo Vikuu Tanzania 2013 linalotarajiwa kufanyika Ijumaa ijayo
(Julai 5) kwenye ukumbi wa San Cirro, Sinza jijini Dar es Salaam.
Warembo
hao wanatarajiwa kusindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa wasanii
nyota nchini Ney wa Mitego, Rich Mavoko, Mori P, Rocka na madansa
wengine.
Mratibu
wa shindano hilo, Agnes Mathew wa kampuni ya Aggy Classic Entertainment
alisema kuwa wasanii hao wawili ni baadhi ya watakaowasindikiza warembo
16 watakaochuana kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Shindano
la Redd's Miss Vyuo Vikuu Tanzania 2013, litakalofanyika Julai 5
litasindikizwa na burudani toka kwa wakali kama Ney wa Mitego, Rich
Mavoko, Rocka, Mori P na wengine," alisema.
Agnes
alisema maandalizi ya shindano yao yanaendelea vyema na kuwataja baadhi
ya warembo watakaochuana siku hiyo ambao kwa sasa wanaendelea kujifua
mazoezini katika ukumbi wa Grand Villa, chini ya mkufunzi wao, Bless
Ngowi kuwa ni Sia Mtui, Feube Urio na Rosemary Alloyce.
"Warembo wengine ni pamoja na Nyangeta Kiboja, Eveline Mathew, Juliet Msaki, Severine Minga," alisema Agnes.
Mratibu
huyo aliongeza kwa kuwataja wadhamini mbalimbali waliojitokeza
kulipiga tafu shindano lake kuwa ni pamoja na Ngorongoro Coservetion,
Redds, Lake gas, Cocacola, Cloud's Fm, Times Fm, Grand Villa Hotel,
Sibuka Tv &Radio, EATV/Radio na Magic FM.
Agnes alisema warembo
watakaoshinda mchuano hiyo mbali na kujinyakulia zawadi mbalimbali
zikiwemo fedha taslim pia watapata nafasi ya kushiriki fainali za Redd's
Miss Tanzania 2013 litakalofanyika baadaye mwaka huu na kutoa wito kwa
mashabiki wa burudani kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo ambalo
litakuwa na burudani nyingine mbali na muziki wa kizazi kipya kama njia
ya kulinogesha zaidi.
Mwisho