Sadio Mane aliyeingia rada za Liverpool |
Mkufunzi wa klabu hiyo, Jurgen Klopp anamtaka nyota huyo wa Senegal mwenye miaka 24 ili kuimarisha safu ya ushambuliajina amepanga kuufanya uhamisho wake kuwa wa kihistoria katika klabu hiyo.
Liverpool na Southampton zitaendelea kufanya mazungumzo kuhusu mpango huo, huku kitita hicho cha uhamisho huo kikiwa kuwa ni suala muhimu zaidi.
Southampton inadaiwa kutaka Pauni Milioni 40 kwa Mane aliyefunga mabao 11 katika mechi 37 alizocheza msimu uliopita wa EPL.
Kitita hicho ni zaidi ya Pauni Milioni 10 ya kile kinachopendekezwa kutolewa na Liverpool, jambo ambalo limefanya mazungumzo kurefushwa zaidi ili kupata muafaka kabla ya njyota huyo kuachiwa atue Anfield.
Southampton ipo mbioni pia kumsaka mrithi wa Ronald Koeman aliyejiunga na klabu ya Everton hatua ambayo huenda ikachelewesha mpango huo.
Klopp alipendezwa na Mane ambaye alihusishwa sana na uhamisho wa Old Trafford wakati wa Louis Van Gaal wakati alipofunga mara mbili baada ya Southampton kutoka nyuma 2-0 na kuiadhibu Liverpool 3-2.