STRIKA
USILIKOSE
Friday, June 24, 2016
Mchezaji alimwa kadi nyekundu kwa kupupua uwanjani
PERSHAGEN, Sweden
SIKIA hii. Inawezekana haijawahi kutokea kokote, ila mwamuzi mmoja wa soka nchini Sweden amemlima kadi mbili za njano kisha kumtoa kwa nyekundu, beki wa Pershagen SK, Adam Lindin Ljung-kvist kwa kosa la kupupua (kujamb**) uwanjani.
Beki huyo wa timu hiyo ya ligi ya daraja la chini alikumbwa nakisanga hicho katika mechi dhidi ya Järna SK na alipokuwa katika harakati za kushangaa kuhusiana na hatua ya refa huyo, alipigwa kadi nyekundu na kuondolewa uwanjani.
Mwamuzi huyo alitaja kitendo cha Adam cha kutoa ushuzi kama tabia isiyo njema kwa mchezaji.
Lakini kulingana na Adam, alidhani alikuwa akifanya hivyo kimaumbile tu na wala hakuwa na nia ya kumchafulia refa hewa.
Taarifa hiyo imeibua malumbano makubwa kote duniani katika mtandao wa kijamii, huku wengine wakisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji soka kupigwa kadi nyekundu kwa sababu ya kuchafua hewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment