Entente Sportivo Setif iliyong'oka Afrika kwa vurugu |
Hali ilivyokuwa katika mechi hiyo kwa vurugu za mashabiki wa ES Setif |
Katika mchezo huo uliopigwa wiki iliyopita mjini Setif, Algeria, Mamelodi iliitambia wenyeji kwa mabao 2-0 na kuibua hasira kwa mashabiki wa klabu hiyo ya Algeria kwa kulianzia mbungi wakirusha mawe, chupa na kufyatua fataki kasi cha kuhatarisha usalama na kufanya mwamuzi kulisimamisha pambano kabla ya muda.
Baada ya Kamati ya Utendaji ya CAF inayohusika na mashindano ngazi ya klabu kukutana na kupitia ripoti ya mchezo huo imeridhika na kuamua kuiondoa Setif kwa kukutwa na hatia ya kushindwa kuthibiti mashabiki wake.
Kwa maana hiyo matokeo ya mchezo huo yamefutwa na Mamelodi pamoja na timu za Enyima ya Nigeria na Zamalek ya Misri wamebakishwa kwenye kundi hilo la B, ambalo kwa sasa litakuwa likiongozwa na Zamalek waliifunga Enyimba ugenini kwa bao 1-0.
Kwa muda mrefu klabu kutoka Afrika Kaskazini kupitia mashabiki wake wamekuwa wepesi wa kufanya vurugu na kuvuruga mechi zinazochezwa viwanja vyao vya nyumbani na hata ugenini kwa kurusha fataki na vikokoro vingine hasa zikifungwa.
No comments:
Post a Comment