MISS
Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akipunga mkono mara baada ya
kuvikwa taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 usiku wa Septemba 21, Ndani ya
Ukumbi wa Mlimani City na kuwashinda warembo wenzake 29.
Na Father Kidevu Blog
HATIMAYE kitendawili cha nani
atanyakua taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 kimeteguliwa usiku huu na
mrembo Happiness Watimanywa kutoka Mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati
kufanikiwa kutawazwa Mshindi wa taji hilo na kuwashinda warembo wengine
29 waiokuwa wakiwania taji hilo.
Nyota ya Happiness ilionekana
dhahiri kung’aa vyema katika fainali hizo mwaka huu tangu pale
alipofanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa
mrembo wa kwanza kuingia nusu fainali.
Wakati Happiness akinyakua Taji
hilo pamoja na zawadi ya Gari na kitita cha shilingi Milioni 8 nafasi ya
pili ilikwenda kwa mrembo Latifa Mohamed kutoka Kitongoji cha Kigamboni
na Kanda ya Temeke na nafasi ya Tatu ikienda kwa Miss Tanzania Sports
Woman, Clara Bayo.
Pamoja nao warembo wengine walio ingia hatua hiyo ya tano bora ni Lucy Tomeka na Elizabeth Prety.
Hii
ndio tano bora ya Redd's Miss Tanzania 2013. Je nani hapa ataondoka na
taji, gari na kitita cha Milio ni 8? Warembo hao kutoka kushoto ni
Happiness Watimanywa (Miss Photogenic), Elizabeth Pretty, Clara Bayo
(Miss Sports Women), Lucy Tomeka na Latifa Mohamed.
No comments:
Post a Comment