Hekeheka kila mtu akisalimisha roho yake |
Milio ya risasi imeweza kusikika
katika jengo la Westgate mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al
shabaab wanawazuilia mateka ambao idadi yao haijajulikana hadi sasa.
Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika
ufyatulianaji huo na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu huku watu
wawili wakinusuriwa asubuhi ya leo.Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali wanazuiliwa ndani ya jengo hilo.
Watu 39 wameuawa baada ya wanamgambo hao kushambulia jengo hilo mwanzo katika eneo la kuegeshea magari na kisha kuingia ndani ya mikahawa na maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kuwpaiga watu risasi kuholela.
Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo.
Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa. Rais Kenyatta anasema kuwa wale waliohusika lazima wakabiliwe na mkono wa sheria.
Jamaa na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa zao wamezuiwa kuingia ndani ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa walifariki kutokana na majeraha yao.
Taarifa nyingine zinasema kuwa mpaka sasa majeruhi wa tukio hilo wamefikia 162.
BBC
No comments:
Post a Comment