KWA HABARI ZA BURUDANI, MICHEZO NA MATUKIO MBALIMBALI
STRIKA
USILIKOSE
Sunday, September 22, 2013
Azam, Yanga leo ni vita kali Taifa
Kipre Tchetche na Nadir Haroub 'Cannavaro leo itakuwaje Taifa?
WACHEZAJI wa wa Azam FC kwa pamoja wameahidi ushindi katika mchezo wa leo
dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa, Azam FC ikiwa
nyumbani.
Hata hivyo Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro amesema 'aah wapi...tunataka pointi tatu baada ya sare tatu mfululizo'.
Kwa
mujibu wa taarifa za mtandao wa Azam, wachezaji wa klabu hiyo
iliyoshinda mechi moja na kupata sare mbili katika mechi zake nne za
awali kama ilivyo kwa wapinzani wao, wamepania kushinda leo ili kutuliza
mashabiki wao.
Ahadi ya wachezaji hao ilitolewa mbele ya Makocha Kally Ongalla na Ibrahim Shikanda, Mwenyekiti Said Muhammad,
Katibu Mkuu Nassor Idrissa na Mratibu wa timu hiyo Patrick Kahemele
kwenye kikao cha pamoja kati ya wachezaji na viongozi kutathmini
mwenendo wa timu hiyo baada ya mechi nne za mwanzo za ligi.
Wachezaji hao wakiongozwa na John Bocco, Jabir Aziz na Salum
Abubakar, walisema matokeo ya sare nyingi walizopata katika mechi
zilizopita hayatokani na matatizo ya huduma isipokuwa ni mitihani ya
kawaida kwenye soka ambapo timu inaweza kucheza vizuri na bado
ikashindwa kupata matokeo.
Wachezaji wameahidi kuongeza nguvu kwa
kuanzia mechi ya leo ili kupata matokeo ya ushindi badala ya sare.
Wachezaji kwa pamoja walionesha masikitiko yao kwa matokeo yaliyopita
na kuahidi kuongeza kujituma kwenye mazoezi na mechi ili kurudisha
makali yaliyoifanya Azam kuwa timu ya kuogopwa.
Azam FC
itashuka uwanjani leo kukwaana na Yanga SC ambapo katika mechi nne
zilizopita Azam FC imeambulia kipigo toka kwa Yanga. Lakini timu zote
mbili zinashuka uwanjani zikiwa na matokeo ya kufanana na idadi sawa ya
pointi tatu
Azam FC leo
itamkosa Agrey Morris Ambrose ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mechi
iliyopita dhidi ya Ashanti United na nafasi yake itajazwa na David
Mwantika.
Wakati Azam wakijipanga hivyo kocha Minziro wa Yanga amesema vijana wake wapo kamili kuhakikisha wanaitungua Azam ili kuwafukuzia watani zao Simba waliopo kileleni.
Yanga kama Azam wana pointi 6, tano nyuma na zile ilizonazo Simba wanaoongoza wa kiwa na pointi 11 baada ya jana kubanwa na Mbeya City.
"Hatukubali kuona tukiendelea kupoteza pointi, tumerejea kwenye uwanja wa Taifa, ambazo ni mzuri na kuwapa nafasi wachezaji kufanya wanavyofanya hivyo tunaamini ushindi ni lazima," alisema.
Alisema kikosi chao kitawakosa baadhi ya wachezaji akiwamo kiungo mkabaji, Salum Telela ambaye ni majeruhi, lakini akidai waliosalia wapo tayari kwa vita na kwamba Azam ikae chonjo.
Timu hizo zinakutana mwezi mmoja na ushei tangu zilipokutana kwene mechi ya Ngao ya Jamii na Azam kulala bao 1-0 lililofungwa na Telela. Pia hilo ni pambano la 11 la Ligi Kuu baina ya timu hizo tangu mwaka 2008 ambapo Yanga imeshinda mara 5 na kupoteza 3 na michezo miwili iliishia kwa sare.
No comments:
Post a Comment