STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 25, 2014

Diamond aliangukia jeshi kwa kuvaa magwanda yao Fiesta

http://haazu.com/wp-content/uploads/2014/09/Diamond1.jpg
Msanii Diamond Plutnumz
BAADA ya mbwembwe za Meneja wake kudai kuwa walikuwa na kibali cha kuvaa magwamda ya Jeshi, msanii Diamond ameamua kuomba radhi kwa kitendo alichofanya kwa kutinga mavazi hayo kwenye onyesho la Fiesta Jumamosi iliyopita.
Diamond ameanguka kuomba radhi kwa Jeshi kupitia barau ambayo MICHARAZO imeiona ikiwa ni saa chache tangu akabadhi magwanda hao kwa Polisi wa kituo cha Oysterbay iliyomhoji kwa saa kibao kutokana na kitendo hicho ambacho ni kinyume cha sheria za nchi.
Icheki barua yenyewe ;

Jonas Nkya akanusha kurushiana risasi na mama'ye

Jonas Nkya
Jonas Nkya, mtoto wa Waziri wa Afya wa zamani nchini Dk Lucy Nkya ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM-Moro
MAPEMA leo kwenye mitandao mingi kulikuwa na taarifa zinahusiana na tukio la kurushiana risasi baina ya aliyekuwa Naibu Waziri wa zamani wa Afya na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Dk. Lucy Nkya na mtoto wake ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Morogoro Jonas Nkya.
Lucy Nkya
Waziri wa zamani wa Afya Dk Lucy Nkya ambaye ni Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki
Tukio hilo ambalo limetokea leo Morogoro baina ya wanafamilia hao, limehusishwa na ugomvi wa kifamilia jambo ambalo limeamsha hisia tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari Morogoro, Jonas Nkya amekanusha taarifa za kurushiana risasi na kueleza kuwa tukio hilo ni tukio la bahati mbaya baada ya bunduki yake kudondoka na kupelekea risasi mbili kufyatuka.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo, Jonas amesema, “.. silaha inakaa kiunoni, nakwenda kwenye gari nashuka pale ofisini pisto hii imeanguka imejipiga risasi mbili nje ya ofisi. Sasa nadhani majirani wakaogopa sijui mi sielewi, lakini kuna watu wanaishi pale. Sasa ndio ikafika hapo wakaja Polisi of course na nini.. tumejaribu kuwaeleza.. ndio hicho kilichotokea. Lakini mimi sijui.. wala sikujua kama mama yangu yuko ndani kwa sababu pale ofisini nimekwenda kufuata gari .”–Jonas
“.. Na ndio maana nasema kama mkipata muda na nyie mnaweza kwenda kumuuliza yule mama je tumegombana.. je kuna kitu kama hicho.. hiyo ndio habari iko hivyo.. hakuna ukweli kwenye hilo..”–Jonas

Real Madrid yaizamisha Barcelona 3-1, Suarez aanza vibaya

Karim Benzema scores Real Madrid's third in the win over Barcelona
Benzema akifunga bao la tatu la Real Madrid
Neymar gave Barcelona the lead after just four minutes with Suarez providing the assist at the Bernabeu
Neymar akishangilia bao lake la mapema kabla ya Real  Madrid kuwageuzia kibao
Ronaldo takes his penalty in the 35th minute to bring Real Madrid level in the El Clasico tie against Barcelona on Saturday
Ronaldo akifunga penati yake
Real Madrid players react after Pepe gave them the lead against Barcelona on Saturday evening at the Bernabeu
Real wakishangilia bao la pili lililofungwa na Pepe
Pepe (right) was able to gift Real Madrid an important lead against Barcelona in the El Clasico showdown on Saturday
Piga Keleleeee Pepe akishangilia bao lake
Real Madrid's Ronaldo and Benzema celebrate sealing the El Clasico win at the Bernabeu in front of their own fans against Barcelona
Benzema akipongezwa na Ronaldo kwa bao lake la tatu
Barcelona held the lead until the 35th minute after Neymar's early goal in the El Clasico tie against Real Madrid
Messi akimpongeza Neymar kwa bao la mapema lililokuwa la kufutia machozi kwao
Lionel Messi (right) looks frustrated during the El Clasico match as Real Madrid's Ronaldo (left) beat his Barcelona opponent on Saturday
Messi hoi mbele ya Ronaldo
REAL Madrid wakiwa uwanja wa nyumbani wa Santiago Bernabeu wameizamisha wapinzani wao wa jadi, Barcelona iliyoshuka dimbani kwa mara ya kwanza wakiwa na nyota wao Luis Suarez kwa mabao  3-1 katika pambano la La Liga.
Barcelona walianza kwa mkwara kwa kuandika bao la kuongoza katika dakika ya nne kupitia kwa Neymar akimalizia kazi nzuri ya Suarez aliyekuwa akicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya Hispania akitokea kifungoni.
Hata hivyo Cristiano Ronaldo aliendeleza rekodi yake ya kufunga mabao katika ligi hiyo kwa kufunga bao la kusawazisha katika dakika ya 35 kwa mkwaju wa penati na kufikisha bao la 16 katika mechi 9 za ligi hiyo.
Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Pepe katika dakika ya 50  kwa kichwa akimalizia mpira uliopigwa na Tom Kroos kabla ya Karim Benzema kuongeza bao la tatu lililowanyong;onyesha Barcelona na kuvunja rekodi yao ya kutopoteza katika ligi ya msimu huu.
Benzema alifunga bao hilo katika dakika ya 61 akimalizia kazi nzuri ya James Rodriguez na kuwapa Real Madrid ushindi uliowafanya wafikishe jumla ya pointi21 na kushika nafasi ya pili wakitofautiana pointi moja na Barcelona wenye pointi 22.

PSG yatakata nyumbani Ufaransa

http://e0.365dm.com/13/01/660x350/PSG-celeb-v-Lille-2013_2892057.jpg?20130127231513MABINGWA watetezi wa Ligi ya Ufaransa, Ligue 1, PSG imepata ushindi mnono nyumbani baada ya kuinyuka Bordeaux kwa mabao 3-0.
Mikwaju miwili ya penati iliyofungwa kila kipindi na Lucas katika dakika ya 45 na 50 na jingine la Ezequel Lavezzi katika dakika ya 81 yaliwapa wababe hao wa Paris ushindi huo na kufikisha jumla ya pointi  21 na kuwashusha wapinzani hao nafasi ya tatu na kukwea kwenye nafasi ya pili nyuma ya Olympique Marseille.
Timu hizo zote zilijikuta ikicheza pungufu kwa kupoteza mchezo mmoja mmoja, PSG wakianza dakika ya 28 baada ya Gregory van der Wiel kulimwa kadi nyekundu kabla ya Andre Biyogho Poko wa Bordeaux katika dakika ya 37.

Newz Alert! Polisi Znz yamnasa mtu na mabomu manne ya kivita

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar, linamshikilia mtu mmoja baada ya kumkamata ma mabomu manne ya kivita.
Hata hivyo jeshi hilo limesema litatoa maelezo kamili ambazo MICHARAZO itawajuza mara baada ya kuzipata.
Kadhalika katika tukio jingine, Mtoto wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Lucy Nkya,  Jonas Nkya amekanusha taarifa za kuwepo kwa tukio la kurushiana risasi na mama yake huyo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao leo.

Mtibwa yarejea kileleni, Rama Salum, Okwi, Tegete 'ambeep' Kavumbagu

Rama Salim (kushoto) na Emmanuel Okwi ambao wameendelea kufunga mabao katika Ligi Kuu na kumbeep Didier Kavumbagu
WAKATI Mtibwa Sugar ikirejea kileleni bila kutoka jasho leo, Mgambo JKT imejinasua mkiani na kuiachia msala timu ya Polisi Moro, huku kiungo mshambuliaji nyota wa Coastal Union, Rama Salum akimwashia 'endketa' mshambuliaji wa Azam, Didier Kavumbagu baada ya kufikisha bao la tatu leo.
Rama alifunga bao la kusawazisha la Coastal na kumfanya kushika nafasi ya pili akilingana na Ally Shomar wa Mtibwa wakiwa na mabao matatu, moja pungufu dhidi ya manne ya Kavumbagu.
Kadhalika Jerry Tegete ameanza na moto baada ya magoli yake mawili aliyofunga leo Shinyanga yamemfanya kuingia kwenye orodha ya wanaowania Kiatu cha Dhahabu.
Mshambuliaji huyo ameungana na wachezaji wengine saba kushika nafasi ya tatu sambamba na Emmanuel Okwi aliyefunga jioni ya leo dhidi ya Prisons-Mbeya.
Wakati katika mbio za ufungaji bora ikiwa hivyo, Mtibwa itakayoshuka dimbani kesho ugenini ikiwa ni kati ya timu mbili ambazo hazijaonja machungu ya kipigo sambamba na Simba, itaumana na Mbeya City baada ya kurejea kileleni kutokana na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Awali Azam waliwatangulia kwa faida ya herufi A wakiwa wamelingana kila kitu kabla ya leo kutibuliwa na JKT Ruvu waliowafumua bao 1-0 uwanja wa Chamazi na kushuka had nafasi ya pili licha ya timu kuwa na pointi 10 sawa na Yanga ambayo imerejea nafasi ya tatu.
Hata hivyo Mtibwa ina nafasi nzuri kwa vile ina mchezo mmoja mkononi kulinganisha na wenzake waliocheza mechi tano kila moja dhidi ya nne za Mtibwa.
Matokeo mengine ya ligi hiyo jioni ya leo imebadilisha msimamo maeneo ya kati na mkiani baada ya Mgambo kujinasua mkiani kwa kushinda 1-0 dhidi ya Ndanda na kufikisha pointi sita zilizowapeleka hadi nafasi ya nane wakilingana na Kagera Sugar waliolazimishwa sare ya 1-1 na Coastal.
Nazo timu za maafande wa JKT, Ruvu Shooting na JKT Ruvu zimefanikiwa kupanda hadi kwenye nafasi ya tano na sita kwa kufikisha pointi 7 baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo timu zote hizo zikiwa zinalingana kwa kila kitu isipokuwa wakitenganishwa kwa herufi zao za mwanzo, JKT wakiitangulia Ruvu.
Unaweza kuuchungulia msimamo wa ligi hiyo na orodha ya wafungaji kujionea mwenyewe.

MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                              P    W    D   L    F    A   GD  Pts
01. Mtibwa Sugar    04  03  01  00  06  01  05  10
02. Azam                05  03  01  01  06  02  04  10
03. Yanga               05  03  01  01  07  04  03  10
04. Coastal Union   05  02  02   01  07  05  02  08
05. JKT Ruvu          05  02  01  02   04  05  -1  07
06. Ruvu Shooting  05  02  01   02  04  05  -1  07
07. Kagera Sugar    05  01  03   01  04  03  01 06
08.  Mgambo JKT    05  02  00  03   02  04  -2  06
09. Prisons              05 01  02   02  05  05  00  05
10. Simba               05  00  05   00  05  05  00 05
11. Mbeya City        04  01  02  01   01  01  00  05
12. Stand Utd          05 01  02   02  03   08  -5  05
13. Ndanda Fc         05  01  00  04   07  10  -3  03
14. Polisi Moro         05  00  03  02   03  06  -3  03

Wafungaji Bora:

4- Didier Kavumbagu(Azam)
3-
Ally Shomari (Mtibwa), Rama Salum (Coastal)
2-
Shaaban Kisiga, Emmanuel Okwi (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Ame Ally (Mtibwa), Rashid Mandawa, Salum Kanoni (Kagera), Aggrey Morris (Azam), Jabir Aziz (JKT Ruvu), Jerry Tegete (Yanga)

Enyeama aitahadharisha CAF kuhusu AFCON 2015

http://www2.pictures.zimbio.com/gi/Mali+v+Nigeria+2013+Africa+Cup+Nations+Semi+afU4DoYXKi0x.jpg
Vincent Enyeama
NAHODHA na kipa tegemeo wa timu ya taifa ya Nigeria 'Super Eagles', Vincent Enyeama amelitaka Shirikisho la Soka la Afrika, CAF kusitisha michuano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015.
Michuano hiyo ilitarajiwa kufanyika Januari mwakani nchini Morocco kabla ya wenyeji hao kuchomoa kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola.
Enyeama anayekipiga katika klabu ya Lille, alifafanua kuwa michuano hiyo inapaswa kusitishwa kutokana na wasiwasi juu ya ugonjwa wa Ebola kuongezeka. 
Enyeama,32, ameeleza woga wake kuwa ugonjwa huo ambao umeshaua zaidi ya watu 4,500 mpaka sasa utasambaa zaidi kufuatia mkusanyiko wa watu watakaokuwepo viwanjani. 
Nyota huyo aliongeza kuwa hatari ni kubwa kama AFCON itaandaliwa wakati huu ambapo bado ugonjwa huo haujadhibitiwa, lakini amesema atashiriki kama nchi yake itafuzu michuano hiyo pamoja na hatari iliyopo.

Southampton yaendeleza rekodi England, West Brom chupuchupu

Sadio Mane, Southampton
Southampton wakishangilia bao lao leo
Mile Jedinak scored his second penalty of the season to give Crystal Palace a 2-0 half-time lead at West Bromwich Albion
West Brom walipokuwa wakiadhibiwa kabla ya kuchomoa mwishoni
BAO pekee lililofungwa na Msenegal Sadio Mane katika dakika ya 33 limeiwezesha Southmpton kupata ushindi mwembemba dhidi ya Stoke City na kuendeleza rekodi ya kutofungika nyumbani.
Ushindi huo umeifanya Southampton kufikisha pointi 19 na kukwea hadi nafasi ya pili wakiwaengua mabingwa watetezi Manchester Citry waliocharazwa mabao 2-1 katika mechi ya mapema leo Jumamosi na kupunguza pengo la pointi kati yao na vinara Chelsea wanaoongoza kwa pointi 22 na wakitarajiwa kushuka kesho kuumana na Mashetani Wekundu uwanja wa Old Trafford.Katika mechi nyingine za Ligi Kuu ya England, West Bromwich Albion wakiwa nyumbani walichomoa kipigo toka kwa Cryastal Palace kwa kulazimisha sare ya mabao 2-2.
Wenyeji walisubiri hadi dakika ya 90 kuchomoa bao kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Saido Berahino ambapo kabla ya hapo Victor Anichebe alifunga bao la kwanza dakika ya 51 na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Wageni walipata mabao yao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa  Hangeland aliyefunga dakika ya 16 kabla ya Jedinak kuongeza la pili sekunde chache kabla ya mapumziko kwa mkwaju wa penati na kuwapa Stoke uongozi wa 2-0 wakati wa mapumziko.

Ndanda yazamishwa tena nyumbani, Mgambo wawapigisha kwata

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSvHwYqtPQMuzPoWUu4QCWVjjgvVwLySqdBYExhW-LxDkl-tjqI3X__y-_vwNzmO6A72piQEbxsK79AqJ8vub5o2bTvjx1VL8FqSFT_-uMryVYDTOmZZVv18G_WiMV4YrQE_D_be0p_aWy/s1600/20140913_160438.jpg
Ndanda FC iliyopigwa tena nyumbani
TIMU ya soka ya Ndanda Fc ikicheza bila ya kocha aliyeipandisha daraja, Dennis KItambi imeendelea kutoa 'takrima' nyumbani baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Mgambo JKT kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara.
Pambano hilo ni la pili kwa Ndanda kulala nyumbani baada ya awali kulazwa mabao 3-1 na Ruvu Shooting na kusababishwa kutimuliwa kwa Kitambi aliyeoonekana pengine ni kikwazo cha timu hiyo kufanya vema.
Bao lililoizamisha Ndanda ikiwa na koicha mpya Hamim Mawazo liliwekwa kimiani dakika ya tatu tu ya mchezo kupitia Ali Nasoro Idd.
Katika mchezo mingine Ruvu Shooting imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Moro katika pambano lililochezwa uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani.
Bao pekee la mchezo huo liliwekwa kimiani na Zubeiry Dabi dakika ya 68 na kuifanya Ruvu kushinda kwa mara ya pili mfululizo na kufikisha pointi 7.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kwa pambano moja tu kati ya Mbeya City itakayoikaribisha Mtibwa Sugar kwenye dimba la Sokoine, jijini Mbeya.
Timu hizo zitakutana huku Mtibwa ikiwa kileleni mwa msimamo ikilingana pointi na timu za Yanga, Azam wakati Mbeya ikiwa na pointi tano baada ya mchezo uliopitwa kuzimwa nyumbani 1-0 na Azam fc.

Arsenal yaizamisha Sunderland, Sanchez apiga zote, Liver mmh

Alexis Sanchez gives Arsenal the lead


Mario Balotelli missed a gilt-edged chance with the last kick of the game for Liverpool at Anfield on Saturday
Balotelli akikiosa bao la wazi wakati Liverpool iking;ang'aniwa nyumbani
Balotelli evades the challenge of Jake Livermore (right) and Chester (centre) during the first half at Anfield on Saturday afternoon
Balotelli akipambana kuisaidia timu yake bila mafanikio
Sanchez lifted the ball over goalkeeper Mannone to make it 1-0 as Arsenal saw out the game with the first-half goal on Saturday
Sanchez akiangalia mkwaju wake ukiingia wavuni
Sanchez runs away in celebration on Saturday at the Stadium of Light after giving Arsenal a lead they would never lose
Akishangilia bao lake la kwanza
Sanchez makes it 2-0 by going around Mannone and securing Arsenal's 2-0 win against Sunderland on Saturday afternoon
Sanchez akifunga bao lake la pili dhidi ya Sunderland
Sanchez during his celebration at the Stadium of Light as Arsenal won 2-0 on Saturday against Sunderland
Shujaa wa Arsenal leo, Alexis Sanchez
MABAO mawili ya Alexis Sanchez moja la kila kipindi yameisaidia Arsenal kupata ushindi mujarabu uwanja wa ugenini dhidi ya Sunderland katika Ligi Kuu ya England, huku Liverpool waking'ang'aniwa nyumbani dhidi ya Hull City kwa kutoka suluhu.
Sanchez aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea Barcelona alifunga mabao yote kwa juhudi zake binafsi dakika dakika ya 30 baada ya beki wa Sunderland Wes Brown kushindwa kuokoa mpira na kumfanya mchezaji huyo kufunga bao kwa guu la kulia.
Sanchez aliongeza bao la pili dakika za nyongeza kabla ya pambano hilo kumalizika na kuwafanya vijana hao wa Arsene Wenger kufikisha Pointi 14 na kupanda hadi nafsi ya tano.
Katika pambano jingine lililochezwa uwanja wa Anfield Liverpool ililazimishwa suluhu ya Hull City licha ya kuwapo na nyota wake wote akiwamo Mario Balotelli aliyekosa mabao ya wazi.

Borussia Dortmund yazimwa nyumbani na Hannover 96

http://static.reviersport.de/include/images/articles/wide/000/288/658.jpeg
Hiroshi Kiyotake aliyeizima Dortmund nyumbani kwao

BORUSSIA Dortmund ikiwa na nyota wake wote imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Hannover 96 katika pambano la Ligi Kuu ya Ujeruman, Bundesliga lililomalizika hivi punde.
Bao pekee lililowazamisha wababe hao liliwekwa kimiani na Mjapani Hiroshi Kiyotake katika dakika ya 61 kabla ya washindi hao kujikuta wakisalia 10 uwanjani dakika za jioni baada ya mchezaji wake Gulselam kulimwa kadi nyekundu baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano.
Kipigo hicho kimeiacha Dortmund ikiwa na pointi saba na kuzidi kumpa wakati mgumu kocha Jurgen Kloop  aliyeifikisha timu hiyo katyika Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka juzi na kulala kwa wapinzani wao Bayern Munich

Yanga yaifumua Stand x3, Tegete afufuka, Azam yafa, Simba droo

http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/08/Pix-1.jpg
Tegete akiwa na kocha Marcio Maximo, mshambuliaji huyo leo amewapa raha wanayanga
https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/04/azam-fc.jpg
Azam waliotibuliwa rekodi yao ya kutofungwa katika ligi ya tangu msimu uliopita
http://static.goal.com/454900/454955_heroa.jpg
Simba wameshindwa kupata ushindi katika mechi zao tano baada ya leo kulazimishwa sare ya 1-1 jijini Mbeya
MSHAMBULIAJI aliyekuwa amezimika, Jerry Tegete jioni ya leo amedhihirisha kuwa bado wamo baada ya kuisaidia Yanga kupata ushindi mnono uwanja wa Kambarage-Shinyanga wakati walipoilaza Stand United kwa mabao 3-0 katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ambayo ilisimamishwa na watani zao Simba kwa kutoka suluhu mechi iliyopita waliwafundisha soka Stand United kwenye uwanja wao kwa mabao ya  Jaja aliyetangulia kufunga dakika ya 13 kabla ya Tegete kufunga mawili akitokea benchi na kuwadhihirisha mashabiki wa kandanda uwezo wa kufunga anao.
Nyota huyo wa zamani wa Taifa Stars alifunga bao la kwanza dakika ya 77 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 90 na kumpa raha Maximo aliyekuwa akicheza pambano la pili ugenini baada ya lile la Mtibwa Sugar na kucharazwa mabao 2-0.
Katika pambano jingine lililochezwa Chamazi, mabingwa watetezi walitibuliwa rekodi yao ya kucheza mechi mfululizo bila kufungwa baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Kipigo hicho kimehitimisha rekodi ya Azam ambayo ilikuwa haijaonja kipigo tangu msimu uliopita ikiwa imecheza mechi 38 ikigawa maumivu kwa wenzake.
Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na  Samuel Kamutu dakika ya 45 na kuiacha Azam wakisaliwa na pointi 10 baada ya mechi tano.
Nayo Simba ilikuwa ikiongoza kwa muda mrefu bao 1-0 dhidi ya Prisons wamejikuta wakiendeleza mdudu wa sare baada ya kutoka 1-1 kufuatia wenyeji kuchomoa bao jioni na kuifanya Simba kupata droo ya tano mfululizo katika ligi hiyo.
Simba ilianza kuandika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Emmanuel Okwi kabla ya wenyeji kuchomoa dakika ya 90 kupitia kwa Hamis Mahingo mmoja wa viungo mahiri kwa sasa nchini.
Ruvu Shooting ikiwa nyumbani uwanja wa Mabatini imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro.
Kutoka Bukoba, wenyeji Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union. Wenyeji walianza kupta bao dakika ya 70 kupitia kwa Salum Kanoni ambaye hata hivyo hakumaliza pambano ilo kwa kupewa kadi nyekundu kabla ya Coastal Union kusawazisha kupitia kwa Rama Salim

Suarez katika mtihani wa kwanza Barca ndani ya El Classico

Suarez akiwa na Neymar
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8-53ZSdb9-cdltdLFO2Oqe_NlMv7YdX30SDZq-HY2jPOQl1RvrmYBHTftj52IGMjiup-oA3b6ssFBNdgX-Xx7p4me8cNGXf8Hhtc-jJCuvrrWg_phGGdk2HoS2IIsI5cDvY1md7HiV0w/s1600/1414161533348_wps_26_Barcelona_s_coach_Luis_En.jpg
Luis Suarez
MSHAMBULIAJI nyota Luis Suarez anatarajiwa kuanza kuitumikia Barcelona kwa mara ya kwanza wakati vinara hao wa La Liga watapoifuata Real Madrid.
Timu hizo mbili zinakutana  katika mchezo wa kwanza wa El Clasico utakaochezwa baadaye leo na dunia iashuhudia nyota huyo na akina Messi na Neymar wakianza pamoja dimbani.
Suarez alikuwa ameruhusiwa kucheza baadhi ya mechi za kirafiki kwa klabu ya nchi yake toka aliposajiliwa kwa kitita cha paundi milioni 75 akitokea Liverpool baada ya kufungiwa miezi minne kwa kosa la kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chiellini katika Kombe la Dunia Juni mwaka huu. 
Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay, anatarajiwa kucheza mechi yake hiyo ya kwanza katika Uwanja wa Santiago Bernabeu akiwa sambamba na Neymar na Lionel Messi. 
Ujio wa Suarez unaweza kufunikwa na Messi ambaye amebakisha bao moja kuifikia rekodi ya mabao 251 katika La Liga iliyowekwa na Telmo Zarra aliyechezea Atletico Bilbao kati ya mwaka 1940 mpaka 1955. 
Kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta ana matumaini wachezaji wote hao wawili yaani Messi na Suarez wanatang’ara katika mchezo huo ili kuendeleza rekodi yao nzuri ya kushinda Bernabeu ambapo mpaka sasa wameshashinda mechi nne kati ya sita walizokutana katika uwanja huo.

West Ham United yaitoa nishai Manchester City

West Ham v Manchester CityMABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wamekumbana na kipigo cha kushtukiza ugenini baada ya kuzamishwa mabao 2-1 na West Ham United katika mchezo wa mapema wa ligi hiyo maarufu kama EPL.
Hicho kilikuwa ni kipigo cha pili kwa Machester City kwa msimu huu baada ya awali kushindw akuhimili vishindo vya  Stoke City waliowatambia kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Etihad kwa bao 1-0 mnamo Agosti 30.
Wenyeji waliochupa hadi nafasi ya nne kwa ushindi huo walianza kuandika bao la kuongoza dakika ya 21 kupitia kwa Morgan Amalfitano akimalizia kazi nzuri ya Valencia, bao lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili timu zote zilizoendelea kushambuliana na kufanya kosa kosa nyingi kabla ya wenyeji kujiandikia bao la pili dakika ya 75 kupitia kwa Diafra Sakho kabla ya David Silva kuipatia Manchester City bao la kufutia machozi dakika mbili baadaye akimaliza kazi ya  Jesús Navas.
Kipigo hicho kimeiacha Manchester City ikisaliwa na pointi 17 na kushindwa kupunguza pengo la pointi dhidi ya Chelsea yenye 22 ambayo itashuka kesho ugenini kuvaana na Manchester United. Watetezi hao wanaweza kuporomoka nafasi ya chini toka nafasi ya pili wanaoishikilia kwa sasa kwa sababu michezo mingine ya ligi inaendelea kuchezwa hivi sasa.