STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 5, 2014

RONALDO AFUNGUKA, ADAI ATAREJEA TENA OLD TRAFFORD

http://media1.santabanta.com/full1/Football/Cristiano%20Ronaldo/cristiano-ronaldo-16h.jpgMSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesisitiza shauku yake ya kurejea katika klabu ya Manchester United katika siku zijazo. 
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alifurahia kipindi cha mafanikio wakati akiwa Old Trafford kati ya mwaka 2003 na 2009 kabla ya kuondoka United na kwenda Madrid kwa kitita kilichovunja rekodi cha paundi milioni 94. 
Hata hivyo, Ronaldo, 29 bado amekuwa na kumbukumbu nzuri kwa klabu yake hiyo ya zamani na anatamani siku moja kurudi huko alipojitengenezea jina lake. 
Akihojiwa Ronaldo amesema anaipenda United na kila mtu anajua hilo amelisema mara nyingi sababu kubwa inayomfanya asiisahau klabu ni marafiki aliowaacha na mashabiki ambao walikuwa wakimpa ushirikiano wa kipekee. 
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa ana furahia kuwepo Madrid na bado ana mkataba wa miaka minne lakini amedai kuwa hawezi kujua kinachoweza kutokea huko mbele.
Mkali huyo anaamini kuna siku atarejea tena kukipiga Old Trafford kulikomwezesha kuitendea haki namba 7 ambayo hivi karibu imepewa Muargentina, Angel di Maria aliyekuwa akicheza nae Santiago Bernabeu.

Astaghafirullah! Boko Haram wazuia watu kuzika Nigeria?!

TAARIFA za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama moja ya miji ambayo ilitekwa na wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria

Seneta mmoja wa eneo hilo,Ahmed Zanna, aliambia BBC kwamba wakazi hawaruhusiwi kuwazika jamaa wao waliouawa na wapiganaji hao.
Inaarifiwa miili imetapakaa katika barabara za mji huo ambao Boko Haram imeuteka.
Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika barabara zake.
Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya wengine wakiuawa.
Seneta huyo ameitaka serikali ya Nigeria kupeleka wanajeshi mjini Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo ili kuulinda dhidi ya wapiganaji hao.
Mnamo siku ya Jumatano serikali ya jimbo hilo ilikanusha madai kuwa jimbo hilo limetekwa na wapiganaji hao.
Maafisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000 wameachwa bila makao kutfuatia mapigano katika mji wa Bama.
Bwana Zanna anasema kuwa barabara za mji huo zimejaa miili ya watu na Boko Harama imewakata wakazi kuwazika jamaa wao. ''Kwa hivyo hali ni mbaya na inaendelea kuzorota,'' asema bwana zANNA
Boko Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini Mashariki ya Nigeria, katika miezi ya hivi karibuni na kusababisha hofu kuwa huenda wakaufikia mji mkuu Maiduguri.
Bwana Zanna amesema kuwa itakuwa janga kubwa ikiwa Boko Haram wataushambulia mji wa Maidiguri ambao una watu zaidi ya milioni mbili.

BBC

Zlatan Ibrahimovic cabadra aweke rekodi ya mabao Sweden

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbXjR7kU2WsZMZN_e13V3fzD4ka3gjNFCrHk1a8gQc_ogu_9VUdRXHZhr1HZQDmGgQWQ-Sa-eDpuBl9DE4VRNmZrCcfy4Z5FR3s4tt7Bf2rPmlaRvalzhyphenhyphenuvDSupHPVPB-NPaqDCCqsZ2s/s1600/article-2744042-21106DAC00000578-424_636x421.jpg
England: After Joe Hart rushed off his line to clear the ball, Ibrahimovic spied an opportunity to lob him1409855865731_wps_15_Sweden_s_forward_and_teamMFUMANIA nyavu mahiri wa PSG ya Ufaransa,  Zlatan Ibrahimovic ameweka rekodi ya kuwa mfalme wa ufungaji wa mabao wa wakati wote wa Sweden.
Nyota huyo mwenye miaka 32 alifunga mabao safi katika mechi ya kirafiki baina ya Sweden dhidi ya Estonia na kuipa ushindi wa mabao 2-0 nchi yake na kumfanya afikishe mabao 50, akivunja rekodi ya Sven Rydell ambaye kwa mara ya mwisho alifunga mabao 49 dhidi ya Finland mwaka 1932.
Baada ya kuvunja rekodi, Ibrahimovic alivua jezi yake kutoa ujumbe kwa mashabiki. Ilisomeka: ‘Ni gjorde det mojligt,’ au: ‘You made it all possible.’ kwa tafsiri isiyo rasmi; “mumefanikisha hili kuwezekana”.
WAFUNGAJI 10 BORA WA SWEDEN
1. Zlatan Ibrahimovic - Magoli 50 katika mechi 99
2. Sven Rydell – Magoli 49 katika mechi 43
3. Gunnar Nordhal -Magoli  43 katika mechi 33
4. Henrik Larsson – Magoli 37 katika mechi 106

5. Gunnar Gren - Magoli 32 mechi 57
6. Kennet Andersson - Magoli 31 mechi 83
7. Marcus Allback - Magoli 30 mech 74
8. Martin Dahlin - Magoli 29 mechi 60
9. Tomas Brolin – Magoli 27 mechi 47
10. Agne Simonssen - Magoli 27 katika mechi 51
Baada ya kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa mwaka 2001, Ibrahimovic alifunga bao la kwanza katika mechi yake ya kwanza ambayo walishinda mabao 3-0 dhidi ya Azerbaijan katika fainali za kombe la dunia.
Katika michuano ya Ulaya mwaka 2004, wakati huo akiwa Ajax, mshambuliaji huyo alifunga bao la mashindano.
Juhudi zake pia zilimfanya afunge bao dhidi ya Italia na kuongeza ukali wake na hatimaye kusajiliwa na Juventus.
Lakini bao lake kali la kimataifa linalokumbukwa sana alifunga mwaka 2012 wakati wakiipa adhabu England.
Akiwa ameshafunga mabao matatukatika mechi hiyo Ibrahimovic alifunga bao kali akiwa umbali wa mita 35 kwa tik tak matata na kumuacha Joe Hart akizubaa langoni na alishinda tuzo ya FIFA ya 2013 ya bao bora la mwaka.

Kivumbi Afrika, mbio za kuwania tiketi ya Morocco zaanza rasmi

https://media.premiumtimesng.com/wp-content/files/2014/06/Eagles-Getty-images.jpg
Mabingwa Watetezi, Nigeria
http://level3.soccerladuma.net/cms2/image_manager/uploads/News/160996/7/default.jpgMBIO za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015 hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo ambapo nchi 28 zitakuwa zikitafuta nafasi 15 kwa ajili ya kujiunga na mwenyeji Morocco katika michuano hiyo Januari mwakani. 
Kuelekea katika michuano hiyo suala kubwa lililokuwa limetawala ni juu ya viwanja vitakavyotumika kwa baadhi ya mechi kutoka na wasiwasi wa ugonjwa hatari wa Ebola. 
Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF limeziamuru nchi za Guinea na Sierra Leone kuhamisha mechi zao za nyumbani katika viwanja huru kwasababu ya mlipuko wa ugonjwa huo kwenye nchi hizo. 
Guinea wao wamehamishia mechi yao ya kundi E dhidi ya Togo huko Casablanca nchini Morocco huku wakikabiliwa na majeruhi kadhaa katika kikosi chao akiwemo Florentin Pogba ambaye ni kaka mkubwa wa nyota wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba. 
Pogba alipata majeruhi wakati klabu ya ya Saint Etienne ilipochabangwa kwa mabao 5-0 na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain Jumapili iliyopita. 
Guinea pia itawakosa kiungo wa Lorient Abdoulaye Sadio Diallo na mshambuliaji wa Lyon Mohamed Lamine Yattara wakati wapinzani wao Togo wao watakuwa na ahueni baada ya mshambuliaji Emmanuel Adebayor kurejea katika majukumu ya kimataifa baada ya kukosekana kwa miezi 18. 
Mechi nyingine itakayochezwa baadae leo utakuwa mchezo wa kundi E utakaozikutanisha Senegal na Misri jijini Dakar. 
Washindi wawili kutoka katika kila kundi watafuzu na kuungana na Morocco katika fainali za Afcon Januari mwakani.
RATIBA YA LEO
Sudan    vs   South Africa 
Guinea   vs   Togo
Senegal  vs   Egypt 

KESHO:
DR Congo vs  Cameroon 
Ethiopia  vs   Algeria
Zambia    vs  Mozambique 
Niger    vs  Cape Verde
Nigeria vs  Congo
Burkina Faso  vs  Lesotho
Gabon  vs   Angola   
Ghana   vs  Uganda 
Côte d'Ivoire vs Sierra Leone
Mali vs Malawi 
Tunisia vs  Botswana

Rasmi! Marcos Rojo sasa ruksa kukipiga Manchester United

http://www.laacib.net/wp-content/uploads/2014/08/Rojo21.jpg 
WANACHEKAAA! Ndivyo unavyoweza kusema kwa mashabiki wa Manchester United, baada ya beki wao mpya Marcos Rojo kupata kibali cha kuanza kuitumikia timu hiyo.
Beki huyo  anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza klabu yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Queens Park Rangers Uwanja wa Old Trafford Septemba 14 baada ya kupatiwa hati ya kufanya kazi.
Rojo alisafiri hadi Lisbon Alhamisi ili kukamilisha taratibu za kupata hati hiyo ya kufanyia kazi England.
Kufanikiwa kwa mchezaji huyo kupata hati hiyo ya kufanyia kazi ni faraja kwa kocha Louis van Gaal, ambaye kikosi chake mina tatizo la safu ya ulinzi.

HALI YA HEWA YABASHIRI MAFURIKO NCHINI

Dkt. Agnes L. Kijazi

MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA OKTOBA - DISEMBA 2014 NCHINI
A:         UTANGULIZI                                      
Taarifa hii inatoa tathmini ya mvua za masika (Machi - Mei) 2014 na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi  cha mwezi Oktoba hadi Disemba, 2014(Vuli).
B:         TATHMINI YA MVUA KIPINDI CHA MACHI – MEI, 2014
Katika msimu uliopita wa mvua za Masika Machi hadi Mei, 2014. Maeneo mengi ya nchi yalipata mvua za wastani hadi juu ya wastani isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Mwanza, Singida na Dodoma ambayo yalipata mvua za chini ya wastani. Matukio ya vimbunga hususan Kimbunga ‘Hellen’ kilichotokea katika Rasi ya Msumbiji kusini magharibi mwa baharí ya Hindi kilisababisha ongezeko la mvua katika eneo la Pwani ya kaskazini.
Maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka:
Kanda ya Ziwa Victoria: Viwango vya mvua vilivyopimwa katika vituo vya Bukoba na Musoma vilikuwa juu ya wastani. Kituo cha Shinyanga kilipima mvua kiwango cha wastani wakati katika kituo cha Mwanza kiwango cha mvua kilikuwa chini ya wastani.
Nyanda za juu kaskazini mashariki: Vituo vya Arusha, Lyamungo na Kilimanjaro vilipima mvua juu ya wastani ilihali vituo vya Moshi na Same kiwango cha mvua kilikuwa cha wastani.
Pwani ya kaskazini na visiwa vya Unguja na Pemba: Vituo vya Dar es Salaam, Morogoro na Pemba vilipima mvua za juu ya wastani na vituo vya Zanzibar, Amani, Kizimbani pamoja na Tanga mvua zilikuwa wastani.

Dondoo muhimu

1. Mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha Oktoba-Disemba, 2014 Vuli unaonyesha kuwa;
           Hali ya mvua inatarajiwa kuwa ya  kuridhisha katika maeneo mengi ya nchi hata hivyo mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa  katika baadhi ya maeneo ya kusini mwa nchi hususan mkoa wa Ruvuma.
           Msimu huu mvua zinatarajiwa kuanza mapema mwezi Septemba katika maeneo ya ziwa Viktoria, nyanda za juu kaskazini mashariki na pwani ya kasikazini
 2. Athari na Ushauri
           Mvua za kutosha zinatarajiwa kwa shughuli za  kilimo katika maeneo mengi ya nchi.
           Vina vya maji katika mito na mabwawa vinatarajiwa kuongezeka katika maeneo mengi ya nchi.
           Maji yatumike kwa uangalifu na kuzingatia taratibu za uvunaji, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali maji
           Matukio ya migogoro inayosababishwa na mifugo, wanyamapori na shughuli za binadamu na kilimo hayatarajiwi kujitokeza kwa kiasi kikubwa.
           Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kuongeza matukio ya mafuriko na uharibifu wa mali na miundombinu.
           Milipuko ya magonjwa yanayosababishwa  na kutuama kwa maji na utiririshaji wa majitaka usiodhibitiwa inaweza kujitokeza.
           Hatua stahiki katika utunzaji wa mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama, na usambazaji wa madawa, maji na chakula ikiwa ni hatua za kujiandaa na kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea

Maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka:
Nyanda za juu kusini magharibi: Vituo vya Mbeya, Tukuyu, na Mahenge vilipima mvua juu ya wastani na kituo cha Sumbawanga kiwango cha mvua kilikuwa cha wastani.
Kanda ya magharibi: Mvua juu ya wastani ilipimwa katika kituo cha Kigoma ilihali vituo vya Kibondo na Tabora mvua zilikuwa ni za wastani.
Pwani ya kusini: Kituo cha Kilwa kilipima mvua juu ya wastani na vituo vya Mtwara pamoja na  Naliendele mvua zilikuwa za wastani.
Kanda ya kati: Vituo vya Singida na Dodoma vilipima mvua chini ya wastani na kituo cha Hombolo mvua za wastani. 
Kanda ya kusini: Kituo cha Songea kiwango cha mvua kilichopimwa kilikuwa juu ya wastani.
C: MIFUMO YA HALI YA HEWA
Katika kipindi cha miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2014 hali ya joto la bahari katika maeneo ya magharibi na kusini -magharibi mwa bahari ya Hindi inatarajiwa kuwa juu ya wastani, upande wa mashariki mwa bahari ya Hindi hali ya  joto la wastani inatarajiwa. Hali hii inatarajiwa kusababisha  upepo  wenye unyevunyevu  kutoka bahari ya Hindi kuelekea katika eneo la  Pwani ya Africa Mashariki. Aidha, hali ya joto la chini ya wastani katika eneo la mashariki mwa bahari ya Atlantiki (Pwani ya Angola) inatarajiwa kusababisha ongezeko la hewa yenye unyevunyevu kutoka katika misitu ya Kongo kuelekea katika maeneo ya magharibi na kusini Magharibi mwa nchi.
Hali ya joto la juu ya wastani katika eneo la Tropikali ya bahari ya Pasifiki linatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2014. Hali hiyo inatarajiwa kuchangia ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua. Hali ya joto la juu ya wastani katika eneo la kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi linaashiria kuwepo kwa matukio ya vimbunga katika msimu wa mvua za Vuli kuanzia mwezi Novemba, 2014.
D:         MWELEKEO WA MVUA OKTOBA - DISEMBA 2014: 
Kutokana na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa, mvua za kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2014 zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:
(i)         Mvua za Vuli (kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)
Msimu wa mvua wa Oktoba hadi Disemba (Vuli) ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki, pwani ya kaskazini, kanda ya Ziwa Viktoria na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Katika msimu huu mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya pwani ya kaskazini (mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), nyanda za juu kaskazini mashariki (mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara) pamoja na mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Msimu wa mvua za Vuli unatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2014 katika ukanda wa Ziwa Viktoria na kusambaa katika maeneo mengine. Hata hivyo, mvua hizo zinatarajiwa kuanza mapema katika maeneo ya ukanda wa pwani (Mkoa wa Tanga na kisiwa cha Pemba) na katika baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kaskazini Mashariki.

Kanda ya Ziwa Victoria: (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga): Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Septemba, 2014 katika mkoa wa Kagera na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma na kuendelea kusambaa katika mikoa ya Mwanza,  Geita, Shinyanga, Simiyu na Mara. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mara, Mwanza pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Maeneo mengi ya mkoa wa Shinyanga yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Septemba, 2014 katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba na kusambaa maeneo ya mkoa  wa Morogoro. Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.

Nyanda za juu Kaskazini Mashariki: (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):
Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Septemba, 2014 na zinatarajiwa kuwa juu ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na kaskazini mwa mkoa wa Manyara. Hata hivyo, kusini mwa mkoa wa Manyara, mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani.
(ii)        Mvua za Msimu (Novemba – Aprili) kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua.
Msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili ni mahususi kwa  maeneo ya  Magharibi mwa nchi, kanda ya  kati, nyanda za juu kusini-magharibi, kusini mwa nchi na pwani ya kusini. Katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2014 maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi Novemba, 2014. Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani katika maeneo ya mikoa ya Rukwa, Katavi pamoja na kusini mwa mkoa wa Kigoma. Hata hivyo, maeneo mengi ya mkoa wa Tabora yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.
Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2014 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani.
Nyanda za juu Kusini Magharibi: (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba, 2014 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi. Maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Mbeya, mvua zinatarajiwa kuwa juu ya wastani.
Maeneo ya kusini na pwani ya kusini (mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara)
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba, 2014 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani isipokuwa maeneo mengi ya mkoa wa Ruvuma, yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani katika baadhi ya maeneo.
Izingatiwe kuwa pamoja na kuwapo kwa uwezekano wa matukio mengi ya mvua kubwa katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua juu ya wastani, hali hiyo pia inaweza kujitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Matukio ya Vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi yanatarajiwa kuchangia katika mwenendo wa mvua nchini. Maeneo ambayo hali ya mvua inaweza kuathiriwa zaidi na vimbunga ni pamoja na kanda ya kati, Nyanda za juu Kusini Magharibi, Magharibi mwa nchi na maeneo ya ukanda wa Pwani.

E: ATHARI NA USHAURI
Maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani isipokua baadhi ya maeneo ya kusini mwa nchi yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani. Matarajio ya mvua hizo pamoja na ushauri kwa baadhi ya sekta za kiuchumi na kijamii zimeainishwa kama ifuatavyo;
Kilimo na Usalama wa Chakula
Katika  maeneo mengi ya nchi hali ya unyevunyevu  wa udongo inatarajiwa kuwa ya kutosheleza shughuli za kilimo. Hata hivyo, kwa maeneo machache ya kusini mwa nchi (hususan Mkoa wa Ruvuma) vipindi vya upungufu wa mvua vinatarajiwa mwanzoni mwa msimu na hivyo kuathiri kiwango cha unyevunyevu wa udongo. Hali ya unyevunyevu wa udongo kupita kiasi inayoambatana na vipindi vya mvua  kubwa inaweza kusababisha ongezeko la magugu, matumizi makubwa ya pembejeo, hivyo kuongeza gharama za uzalishaji. Wakulima wanashauriwa kuandaa mashamba  na pembejeo mapema  pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalam wa kilimo kwa matumizi sahihi ya ardhi na mbegu.

Malisho  na maji kwa ajili ya mifugo na wanyama pori
Hali ya malisho na upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo na wanyama pori inatarajiwa kuwa nzuri katika maeneo mengi nchini. Hata hivyo, wafugaji  wanashauriwa kuzalisha malisho na  kuyahifadhi kwa matumizi wakati wa kiangazi. Aidha, wafugaji wanashauriwa kufuata maelekezo ya wataalam wa ugani katika maeneo yao hususan matumizi ya maji na malisho  na kukabiliana na  magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza. Kutokana na hali ya mvua inayotarajiwa, matukio ya migogoro inayosababishwa na mifugo,  wanyamapori na shughuli za binadamu na kilimo hayatarajiwi kujitokeza kwa kiasi kikubwa.

Maliasili na Utalii
Mamlaka za usimamizi wa shughuli za utalii na hifadhi za wanyamapori zina shauriwa kuchukua hatua stahiki katika kuzuia uharibifu wa  miundombinu kama barabara na madaraja ndani ya hifadhi dhidi ya adhari za mvua kubwa na za juu ya wastani katika maeneo husika.  Aidha, wawindaji, wapiga picha za kitalii na makampuni ya kitalii yanashauriwa kuchukua tahadhari ya uwepo wa mafuriko kutokana na mvua zinazotarajiwa.
Maji na Nishati
Mtiririko wa maji katika mito na vina vya maji katika mabwawa vinatarajiwa kuongezeka katika maeneo mengi ya nchi kutokana na mvua za msimu wa Vuli. Pamoja na matarajio ya kuwepo kwa mvua za juu ya wastani inashauriwa kuwa maji yatumike kwa uangalifu na kuzingatia taratibu za uvunaji, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali maji.
Mamlaka za Miji
Inashauriwa  kuchukua hatua  za kuhakikisha kuwa mifumo na njia za kupitisha maji  zinafanyakazi  katika kiwango cha kutosha kuhimili mvua zinazotarajiwa ili kuepusha maji kutuama na kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu, upotevu wa maisha na mali katika maeneo husika.
Sekta ya Afya
Ushauri unatolewa kwa jamii na sekta husika kuchukua hatua stahiki katika kuzuia  milipuko ya magonjwa yanayosababishwa  na kutuama kwa maji na utiririshaji wa maji taka usiodhibitiwa katika maeneo yao.
Menejimenti ya Maafa
Mamlaka za maafa na wadau wengine wanashauriwa kuchukua hatua stahiki katika utunzaji wa mazingira, upatikanaji wa maji safi na salama, na usambazaji wa madawa, maji na chakula ikiwa ni hatua za kujiandaa na kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea kutokana na vipindi vya mvua  kubwa na mvua za juu ya wastani zinazotarajiwa.
Vyombo vya habari
Vyombo vya habari vinashauriwa kufuatilia, kupata na kusambaza taarifa sahihi za mienendo ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kutumia wataalam wa sekta husika katika kuandaa na kufikisha taarifa za masuala mtambuka ya hali ya hewa kwa jamii. Aidha, jamii nayo inashauriwa kufuatilia na kuzingatia taarifa sahihi za hali ya hewa na mirejeo yake kupitia vyombo vya habari.

Angalizo: Mwelekeo wa mvua uliotolewa hapa umezingatia zaidi kipindi cha msimu (miezi mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya mvua na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika   uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi. Watumiaji wa taarifa za utabiri huu wanashauriwa pia kufuatilia tabiri za saa 24, siku 10 pamoja na wa mwezi kama zinavyotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini.


Dkt. Agnes L. Kijazi
MKURUGENZI MKUU

NI DIAMOND PLATNUMZ TENA! CHANNEL O YAMTEUA X4 ORODHA HII HAPA

http://larrybway91.files.wordpress.com/2014/04/diamond-platnumz.jpg?w=594SUPASTAA Diamond ameendelea kutusua anga la kimataifa baada ya Channel O ya Afrika Kusini kumteua katika vipengele vinne kuwania tuzo ya CHAOMVA 2014.
Diamona aliyetwaa tuzo ya AFRIMMA hivi karibuni na kushindwa kiduchu kunyakua tuzo za MTV na BET ameteuliwa kwenye vipengele vya Most Gifted Video of the Year, Most Gifted New Comer, Most Gifted Afro Pop na Most Gifted East Africa.
Tumpigie kura za kutosha na tumuombee Mungu hata kama HUPENDI ilimradi tu ashinde!
ORODHA KAMILI HII HAPA:
MOST GIFTED MALE
CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA
DAVIDO – AYE
RIKY RICK FT OKMALUMKOOLKAT – AMANTOMBAZANE
K.O. FT KID X – CARACARA
SARKODIE – ILLUMINATI

MOST GIFTED FEMALE
THEMBI SEETE – THUNTSHA LEROLE
BUCIE FT HEAVY K – EASY TO LOVE
LIZHA JAMES FT UHURU – QUEM TI MANDOU
TIWA SAVAGE FT DON JAZZY – EMINADO
SEYI SHAY – IRAWO

MOST GIFTED NEWCOMER
DREAM TEAM FT TAMARSHA, AKA & BIG NUZ – TSEKEDE
CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA
EMMY GEE FT AB CRAZY & DJ DIMPLEZ – RANDS AND NAIRAS
DIAMOND – NUMBER ONE
PATORANKING – GIRLIE O (REMIX)


MOST GIFTED DUO, GROUP OR FEATURING
UHURU FT OSKIDO & PROFESSOR – Y-TJUKUTJA
DJ CLOCK FT BEATENBERG – PLUTO (I REMEMBER)
R2BEES FT WIZKID – SLOW DOWN
K.O. FT KID X – CARACARA
KCEE FT WIZKID – PULL OVER

MOST GIFTED DANCE
UHURU FT OSKIDO & PROFESSOR – Y-TJUKUTJA
DAVIDO – SKELEWU
DJ CLOCK FT BEATENBERG – PLUTO (I REMEMBER)
P SQUARE – PERSONALLY
BUSISWA FT VARIOUS – NGOKU

MOST GIFTED RAGGA DANCEHALL
BUFFALO SOULJAH – BASAWINE
OREZI – RIHANNA
JESSE JAGGZ FEAT WIZKID – BAD GIRL
PATORANKING – GIRLIE O (REMIX)
SHATTA WALE – EVERYDOBY LIKES MY TING

MOST GIFTED AFRO POP
DAVIDO – AYE
MAFIKIZOLO FT MAY D – HAPPINESS
DIAMOND – NUMBER ONE
FLAVOUR ADA ADA
IYANYA – JOMBOLO

MOST GIFTED KWAITO
UHURU FT OSKIDO & PROFESSOR – Y-TJUKUTJA
CHARACTER FT MONO T & OSKIDO – INXEBA LENDODA
BIG NUZ FT KHAYA MTHETHWA – INCWADI YOTHANDO
DJ VETKUK VS MAHOOTA – KHABA LENJA
DJ CNDO – YAMNANDI INTO

MOST GIFTED R&B
2FACE FT T PAIN - RAINBOW
JIMMY NEVIS FT KWESTA – BALLOON
GB COLLECTIVE FT BRIAN TEMBA & REASON – CHOCOLATE VANILLA
DONALD – CRAZY BUT AMAZING
NIYOLA – TOH BAD

MOST GIFTED HIP HOP
CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA
KHULI CHANA FT DA L.E.S & MAGESH – HAPE LE HAPE 2.1
PHYNO – ALOBAM
K.O. FT KID X – CARACARA
AKA – CONGRATULATE

MOST GIFTED SOUTHERN
DJ CLOCK FT BEATENBERG – PLUTO (I REMEMBER)
CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA
AKA – CONGRATULATE
ZEUS – PSYCH
K.O. FT KID X – CARACARA

MOST GIFTED WEST
R2BEES FT WIZKID – SLOW DOWN
DAVIDO – AYE
BURNA BOY FT D’BANJ – WON DA MO
OLAMIDE – TURN UP
DR SID FT DON JAZZY – SURULERE


MOST GIFTED EAST
SAUTI SOL – NSHIKE
DIAMOND – NUMBER ONE
NAVIO – NO HOLDING BACK
EDDY KENZO – SITYA LOSS
ELANI – KOOKOO

MOST GIFTED VIDEO OF THE YEAR
EMMY GEE FT AB CRAZY & DJ DIMPLEZ – RANDS AND NAIRAS
DAVIDO – AYE
K.O. FT KID X – CARACARA
BURNA BOY – RUN MY RACE
TIWA SAVAGE FT DON JAZZY – EMINADO
DR SID FT DON JAZZY – SURULERE
RIKY RICK FT OKMALUMKOOLKAT – AMANTOMBAZANE
CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA
SARKODIE – ILLUMINATI
DJ CLOCK FT BEATENBERG – PLUTO (I REMEMBER)
AKA – CONGRATULATE
DIAMOND – NUMBER ONE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPfsySjCulA6nI6NANBb-74R99q6AlmjsTTFY7BlaqovuPWEvH2mhvXvzyDq1BU8sDFB0DD3SKugGwn0zuH7qjboNOhAs1fttc8Xy_dzLSEdlqV2DgoVa8Ku_EhdAFbQBqCeRHduQ8cvE/s640/532cebddf6210a2e0b489f323059cc1a.jpeg

van Persie atatahadharisha Falcao Old Trafford

http://i4.eurosport.com/2014/09/03/1306699-28127090-640-360.jpgRADAMEL Falcao hajahakikishiwa namba katika kikosi cha kwanza cha Manchester United, kwa mujibu wa mshambuliaji wa Mashetani Wekundu, Robin van Persie.
Mchezaji wa kimataifa wa Colombia, Falcao (28), alijiunga na Man  U kwa mkopo wa mwaka mmoja uliowagharimu paundi milioni 6.
"Nakaribisha ujio wake, anatufanya tuwe bora zaidi," Van Persie aliiambia Fox Sports NL.
"Katika klabu kubwa daima unahitaji wachezaji bora, ambao pia wanafiti katika falsafa. Falcao ni lazima apiganie namba, kama ilivyo kwangu mimi."
Falcao alifunga magoli 11 katika mechi 20 alizochezea klabu ya Monaco ya Ligi Kuu ya Ufaransa msimu uliopita, kabla ya kuumia goti Januari, maumivu yaliyomweka nje ya Kombe la Dunia nchini Brazil.
Kulikuwa na uvumi kwamba ameletwa Man U ili kuchukua nafasi ya Van Persie (3)1, ambaye amevumishiwa kuhitaji kufanyiwa upasuaji wa goti.
"Nimevutiwa kwamba watu wamefikiria kitu kama hicho," alisema Mholanzi huyo, ambaye alitua Old Trafford akitokea Arsenal kwa paundi milioni 24 mwezi Agosti 2012 na alifunga magoli 26 ya ligi katika msimu wake wa kwanza na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa.
"Sijui yametokea wapi hayo na naweza kusema huku mkono wangu nikiwa nimeuweka kwenye moyo wangu kwamba sitakuwa hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji."

Taifa Stars yaifuata Burundi ikiwa na hasira ya 3-0

http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/stars%20jezi.jpg?itok=YI5JETByhttp://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/field/image/team-stars.jpg?itok=qYvzIZN8KIKOSI chenye wachezaji 20 cha timu ya taifa (Taifa Stars) kimeondoka nchini leo alfajiri kwenda Bunjura, Burundi huku kocha wa timu hiyo, Mholanzi Mart Nooij akiahidi kulipa kisasi cha kufungwa 3-0 dhidi ya taifa hilo katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya 'Etamba Murugamba' itakayopigwa nchini humo Jumapili.
Katika mechi iliyopita ya kirafiki iliyozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Aprili 26, mwaka huu, kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa "kimefinyangwafinyangwa" na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kulazimisha waanze wachezaji watano wa 'maboresho', kililala 3-0 dhidi ya Warundi na kuharibu pilau la sherehe zilizokuwa zimefana za Miaka 50 ya Muungano.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuagwa kwa Taifa Stars, Nooij alisema amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha kinaibuka na ushindi ili kulipa kisasi cha kufungwa nyumbani na pia kujihakikishia kinapanda katika viwango vya soka vya kimataifa vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
"Ninatambua Burundi ina wachezaji wazuri na wa kimataifa kina (Amisi) Tambwe, (Pierre) Kwizera na (Didier) Kavumbagu lakini kwa kikosi tunachokwenda nacho, tuna uhakika wa kushinda ugenini na kulipa kisasi maana walitufunga kwetu," alisema Nooij.
Aliwataja wachezaji 20 anaokwenda nao Bunjumbura kuwa ni pamoja na makipa Mwadin Ally (Azam FC) na Deogratias Munishi 'Dida' (Yanga).
Wengine ni Shomari Kapombe (Azam FC), Oscar Joshua (Yanga), Said Morad (Azam FC), Nadir Haroub 'Canavaro' (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Joram Mgeveke (aliyesajiliwa Simba kutoka kikosi cha maboresho ya Taifa Stars), Simon Msuva (Yanga), Erasto Nyoni (Azam FC), Himid Mao (Azam FC), Amri Kiemba (Simba), Haruna Chanongo (Simba), Salum Abubakary 'Sure Boy' (Azam FC), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya ya Qatar), Hamis Mcha (Azam FC), Juma Luizio (Zesco FC ya Zambia), Mrisho Ngasa (Yanga), Mbwana Samata na Thomas  Ulimwengu (wote TP Mazembe ya DRC).
Nooij alisema mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor', beki kisiki Agrrey Morris na kipa Aishi Manula wameachwa katika msafara wa Burundi kwa sababu mbalimbali zikiwamo majeraha na kutokuwa na uhakika wa kucheza Jumapili.
Alisema Bocco na Morris ni majeruhi huku akieleza kuwa makipa Dida na Mwadini wanatosha kwa mechi hiyo, hivyo haoni sababu ya kwenda na Manula.
Stars itaingia uwanjani mwishoni mwa wiki ikiwa na kumbukumbu ya kutolewa na Zimbabwe kwenye mbio za kuwania kushiriki fainali zijazo za Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika Morocco mwakani.
Naye Somoe Ng'itu anaripoti kuwa washambuliaji wawili wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe, Pierre Kwizera na Didier Kavumbagu wa Azam, waliondoka nchini jana na kuelekea kwao Burundi kwa ajili ya kujiunga na timu yao ya taifa inayojiandaa kuivaa Taifa Stars keshokutwa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola, alisema kuwa Tambwe, Kwizera na nyota wengine wa Taifa Stars walipewa ruhusa jana kwa ajili ya kujiunga na timu zao za taifa.
Matola alisema kuwa hata hivyo, kuondoka kwa nyota hao hakutaharibu programu ya mazoezi kwa sababu huko wanapokwenda pia wanakwenda kucheza mechi ya kimataifa.
"Kwa upande wetu tuko vizuri, kikosi kimeiva na msimu ujao tutatoa ushindani kwa kila tutakayekutana naye," alisema Matola.
Taifa Stars na Burundi zinakutana katika mchezo unaotambuliwa na kalenda ya FIFA.
Tayari wachezaji wanaocheza nje ya nchi, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mwinyi Kazimoto anayecheza klabu ya Al Markhiya ya Qatar wameshawasili nchini.
Awali Stars ilitarajia kucheza dhidi ya Morocco lakini Waarabu hao waliikacha wakidai kwamba wamewakosa nyota wao wanaocheza nje ya nchi hiyo.

Uhaba wa walimu Elimu ya Dini tatizo kubwa nchini-IEP

http://www.educatedanxiety.com/wp-content/uploads/2014/08/quran-2.jpgNA SULEIMAN MSUYA
JOPO la Elimu la Waislam (IEP) limesema pamoja na mafanikio yanayopatikana katika kuhakikisha kuwa elimu ya dini inapatikana nchini kote bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uchache wa waalimu wenye taaluma hiyo.
Hayo yamebainishwa Afisa Mwandamizi wa (IEP) Suleyman Daud wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Daud alisema tangu utaratibu huo wa kutoa elimu ya dini uanze wamepata mafanikio makubwa jambo ambalo linawapatia hamasa ya kuendelea kuboresha ili uweze kutoa tija kwa vijana wa Kiislaam hapa nchini.
Alisema jitihada zao zimejikita katika kuwapatia elimu ya dini vijana wakiislam ambao wanamaliza vyuo mbalimbali hapa nchini kuanzia ngazi ya cheti, stashahada na shahada ili waweze kutoa elimu kwa vijana wa shule za msingi.
“Napenda kuwaambia Watanzania jamii ya Kiislam kuwa juhudi zetu zinaenda vizuri za kuwapatia vijana wao elimu ya dini ila changamoto kubwa ni uchache wa walimu wenye elimu hiyo kuwafundisha” ,alisema.
Afisa Mwandamizi huyo wa (IEP) alisema pamoja na changamoto hiyo ya uchache wa waalimu mafanikio yamekuwa yakiiongezeka kwa shule nyingi kuongezeka katika kufanya mitihani hiyo ambayo haina athari yoyote katika matokeo ya darasa la saba.
Daud alisema katika mtihani wa mwaka jana mikoa 26, wilaya 94 na shule 2,100  ya Tanzania Bara na Visiwa zilishiriki watahiniwa walikuwa 68,096 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 38.04.
Aidha Afisa alisema kwa matokeo ya mwaka huu wa 2014  mtihani ambao ulishirikisha mikoa 26, wilaya 115, shule 2559 na wahitimu 74192 na ufaulu ni sawa na asilimia 46.45 ambao ni ongezeko la asilimia 8.
Alisema mitihani hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka kwa wanafunzi wa wakiislam wanaomaliza la saba  ambapo lengo lao ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2017 mitihani hiyo iwe inatambulika kwenye Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Daud alisema pamoja na ukweli kuwa mitihani hiyo kutotambulika katika baraza la mitihani bado vijana wa kiislaam wamekuwa wakishiriki bila kuleta pingamizi hasa katika shule ambazo zinaendeshwa kwa taratibu za kiislaam.
Afisa Mwandamizi huyo alisema katika kufikia malengo hayo juhudi zinahitajika kutoka kila pande hasa kwa wazazi kwani ni wazi kuwa elimu hiyo inawajengea uadilifu na upendo vijana hao.
‘Unajua kwa muda mrefu elimu ya dini imekuwa ikitolewa kwa wanafunzi wa sekondari pekee jambao ambalo imeifanya NECTA kulitumia somo hilo katika kutafsiri matokeo ya mwanafunzi hivyo lengo letu ni kuhakikisha elimu hiyo inakuwa rasmi katika elimu ya msingi”, alisema.

Nigeria kitanzini mbele ya FIFA

http://goodlife.com.ng/uploads/Sanni-Azeez_87_dream-team.jpg 
NIGERIA imejiweka matatani mbele ya Shirikisho la Soka Duniani, FIFA kutokana na mgogoro mkubwa wa uongozi uliopo katika Shirikisho lao la soka la NFF.
Kutokana na hali hiyo FIFA limeipa Nigeria muda wa mpaka Septemba 8 kwa kiongozi wa NFF Chris Giwa awe amejiuzulu au wafungiwe. 
Katika barua yake iliyotumwa kwa katibu mkuu wa NFF Musa Amadu, FIFA wameeleza kuwa kamati yake ya dharura imeamua kuisimamisha nchi hiyo mpaka mtajwa atapoachia madaraka na katibu mkuu aweze kuendelea na majukumu yake bila kubughudhiwa. 
FIFA pia ilifafanua kuwa kamati ya utendaji NFF iliyoteuliwa Agosti 25 mwaka huu ikiwa chini ya Rais Aminu Maigari itatakiwa kuitisha mkutano mkuu haraka ili kuchagua wajumbe wa kamati ya uchaguzi kabla ya kuitisha mkutano mwingine wa uchaguzi kwa ajili ya viongozi wapya wa shirikisho hilo. 
FIFA imeweka wazi katika barua yake hiyop iliyosainiwa na kamtibu mkuu wake Jerome Valcke kuwa mara NFF itakapofungiwa nchi hiyo haitapata nafasi ya kushiriki michuano yoyote ya kimataifa ikiwemo hata ile ya kirafiki. 
Hata hivyo uamuzi huo wa FIFA kusogeza mbele muda huo umetoa ahaueni kwa mchezo wao wa kufuzu Mataifa ya Afrika dhidi ya Congo utakaofanyika Jumamosi hii huko Calabar lakini kuna wasiwasi wa mchezo wao dhidi ya Afrika Kusini unaotarajiwa kufanyika Septemba 10 usifanyike kama maagizo hayo hayatazingatiwa.