TAARIFA za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama moja
ya miji ambayo ilitekwa na wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram
Kaskazini Mashariki ya Nigeria
Seneta mmoja wa eneo hilo,Ahmed Zanna, aliambia BBC kwamba wakazi hawaruhusiwi kuwazika jamaa wao waliouawa na wapiganaji hao.
Inaarifiwa miili imetapakaa katika barabara za mji huo ambao Boko Haram imeuteka.
Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika barabara zake.
Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya wengine wakiuawa.
Seneta huyo ameitaka serikali ya Nigeria
kupeleka wanajeshi mjini Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo ili
kuulinda dhidi ya wapiganaji hao.
Mnamo siku ya Jumatano serikali ya jimbo hilo ilikanusha madai kuwa jimbo hilo limetekwa na wapiganaji hao.
Maafisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000 wameachwa bila makao kutfuatia mapigano katika mji wa Bama.
Bwana Zanna anasema kuwa barabara za mji huo
zimejaa miili ya watu na Boko Harama imewakata wakazi kuwazika jamaa
wao. ''Kwa hivyo hali ni mbaya na inaendelea kuzorota,'' asema bwana
zANNA
Boko Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini
Mashariki ya Nigeria, katika miezi ya hivi karibuni na kusababisha hofu
kuwa huenda wakaufikia mji mkuu Maiduguri.
Bwana Zanna amesema kuwa itakuwa janga kubwa
ikiwa Boko Haram wataushambulia mji wa Maidiguri ambao una watu zaidi ya
milioni mbili.
BBC
BBC
No comments:
Post a Comment