MUIGIZAJI nyota nchini Kajala Masanja anatarajiwa kumsindikiza mtoto wake Paula kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula bata na watoto wenye ulemavu wa akili wanaolelewa katika eneo la Sinza.
Kwa mujibu wa muongozaji na 'meneja' wa Kajala katika uzalishaji filamu, Leah Richard 'Lamata' Paula atasherehekea siklu yake ya kuzaliwa keshokutwa na Kajala ameamua kuiandalia sherehe hiyo kuwafariji watoto hao walemavu.
"Mtoto wa Kajala anatarajiwa kufanyiwa sherehe ya kuzaliwa kwake na mama yake yaani Kajala na shughuli nzima itafanyika katiia kituo cha kulelea watoto wenye Ulemavu wa akili Sinza, mtoto huyo atatumia siku hiyo kula na kucheza na watoto hao," alisema Lamata.
Lamata alisema Kajala ameamua kufanya hivyo kama njia ya kuwafariji watoto hao sambamba na kumpa darasa mwanae juu ya kutambua umuhimu wa kuwaheshimu na kuwajali watu wenye hali tofauti za kimaumbile na sherehe hiyo itahudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo nyota wa filamu nchini.
STRIKA
USILIKOSE
Monday, July 14, 2014
SUMAYE chupuchupu kufa ajali ya ndege
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (pichani), amenusurika kifo hivi karibuni
baada ya ndege ya shirika la Precision Air, iliyokuwa ikitoka Mwanza
kwenda Dar es Salaam kupata hitilafu ya injini.
Ndege hiyo, ambayo iliondoka Mwanza saa 2:30 usiku, ilipata hitilafu
ya injini moja muda mfupi tu baada ya kuruka, hali iliyomlazimu rubani
wa ndege hiyo kubadili mwelekeo na kutua katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Akizungumza na Mtanzania jana, Sumaye, ambaye alikuwa mmoja
wa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo, alithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo.
Sumaye alisema kitendo cha injini kupata hitilafu, ilimlazimu rubani
wa ndege hiyo kuruka na injini moja mpaka KIA, ambako walitafutiwa ndege
nyingine ili kuendelea na safari.
Alisema kutokana na tatizo hilo, abiria walilazimika kuondoka KIA kwa
kugawanywa kwenye ndege tofauti zilizokuwa zikielekea Dar es Salaam
ambapo Sumaye aliondoka saa 7 kasoro usiku.
Msemaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bestina
Magutu, alipotafutwa ili kujua kilichotokea kwenye ndege
hiyo, alisema kuwa hakuwa na taarifa zozote za hitilafu ya ndege hiyo.
“Hebu ongea nao wenyewe, sijapata taarifa zozote mpaka sasa, nimetoka ofisini jana sikuwa na taarifa,” alisema Magutu.
Naye Mratibu wa Masoko wa Precision Air, Hilaly Mremi, alipozungumza na Mtanzania alikiri kutokea kwa hitilafu hiyo ya ndege.
“Kwa kifupi hakuna ajali iliyotokea, hitilafu zinazotokea kwenye
ndege ni za kawaida kama ambavyo gari inaweza kuharibika na kupakiwa
pembeni,” alisema Mremi.
Alisema safari za shirika hilo zinaendelea kama kawaida na kutaja namba ya ndege hiyo kuwa ni TW 415.
Ndani ya wiki hii, ndege mbili za shirika hilo zimenusurika ajali baada ya kupata hitilafu wakati zikiwa angani.
Mbali na ndege hiyo aliyokuwemo Sumaye, ndege nyingine ya shirika
hilo yenye namba ya safari Pw 77 na ya usajili TWC, iliyokuwa ikitoka
Mwanza kwenda Kilimanjaro ilinusurika kupata ajali juzi jioni na hivyo
kulazimika kurudi na kutua kwa dharura uwanjani hapo baada ya kupata
hitilafu ikiwa angani.
Mbali na Sumaye, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, naye aliwahi
pia kupata ajali mwaka jana akiwa kwenye ndege za shirika hilo.
Lowassa alikuwa miongoni mwa abiria 37 waliokuwa wamesafiri na ndege
hiyo ambayo ilipasuka magurudumu manne ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa
Ndege wa Arusha.
Katika ndege hiyo pia kulikuwa na maofisa mbalimbali wa Serikali na
Jeshi la Wananchi, ambao walikwenda kuhudhuria sherehe ya kutolewa
kamisheni kwa maofisa wa jeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi
Monduli (TMA).
MTANZANIA
Riyama aiogopa kesho ya Isike Samuel
Riyama Ally |
Isike Samuel |
Riyama aliyewahi kutamba kwenye makundi mbalimbali na kisha kwenye michezo ya kwenye runinga kabla ya kuibukia kwenye filamu, akitajwa miongoni mwa waigizaji wa kike walioshirikishwa katika filamu nyingi nchini, 'atauza sura' katika filamu hiyo mali ya Isike Samuel.
Akizungumza na MICHARAZO, Isike alisema filamu hiyo ya 11 kuiandaa kupitia kampuni yake ya Classic Vision pamoja na Riyama pia imewashirikisha wakali kama Hemed Suleiman 'PHD', Frank Kusenha, Steve wa Maisha Plus na yeye mwenyewe (Isike).
"Najiandaa kuachia filamu yangu ya 11 iitwayo 'Naiogopa Kesho' ambayo nimeiigiza mimi na kuwashirikisha kina Riyama Ally, Hemed, Frank Kusenha na wengine. Ni bonge la filamu ambayo mtu hapaswi kuikosa kwa mafunzo yake," alisema.
Isike aliyejitosa kuigiza na kuzalisha filamu tangu akiwa kidato cha pili akiwa na umri wa miaka 16 tu, alisema anaamini kazi hiyo itafunika sokoni kama ilivyokuwa kwa filamu zake nyingine za nyuma ambazo ni; 'Ivan Tears', 'Eyes on Me', 'Identity Card', 'Lonely', 'Tulizana', 'Rudi Kaburini', 'Sad Moment', 'Mr Masumbuko', 'Two Sisters' na 'Family Apart'.
Messi apozwa Brazil, 'James Bond' anyakua kiatu cha Dhahabu
James Rodriguez wa Colombia aliyetwaa kiatu cha dhahabu |
Lionel Messi wa Argentina aliyeteuliwa kuwa MCHEZAJI BORA |
NI UJERUMANI 2014, WANAUME WAWEKA REKODI BRAZIL
Ujerumani wakishangilia taji lao baada ya kuilaza Argentina na kutwaa Kombe la Dunia 2014 |
Raha Tupu kwa Wanaumeeeeee! |
Vita ilikuwa naona hii pichani |
UJERUMANI imeweka rekodi ya kutwaa taji la Kombe la Dunia katika Bara la Amerika ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu za Ulaya baada ya kuinyuka katika muda wa nyongeza Argentina waliokuwa waliopoiteza nafasi nyingi kuweza kumaliza kazi na kulibakisha taji hilo baranai humo.
Bao la dakika ya 113 kupitia kwa mtokea benchi Mario Gotze lilitiosha kuwapa Ujerumani taji la nne la michuano hiyo huku wakiweka rekodi nyingine ya kucheza mechi zao saba bila kupoteza hata mchezo mmoja na ikiongoza kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga 18 na kufungwa manne tu.
Pambano hilo lililokuwa na kosakosa nyingi, Argentina ikipoteza nafasi nyingi za kufunga, lilishuhudia dakika 90 zikimalizika kwa sare ya 0-0 na kuongezwa dakika 30 za nyongeza.
Katika dakika hizo pambano liliwaweka roho juu mashabiki wa timu zote na Messi alikaribia kufunga bao la kusawazisha na pengine kuupelekea mchezo huo kwenye matuta, lakini Mchezaji Bora huyo wa michuano hiyo ya Brazili alipaisha kimaajabu mbele a Kipa Bora wa mashindano hayo ya 2014, Manuel Nieuer.
Mario Gotze aliyeingia uwanjani badala ya Miloslav Klose dakika mbili kabla ya muda wa kawaida kumalizika alipata pande safi ya Andre Schuerrle na kutuliza gambani kabla ya kumtungua kipa wa Argentina, Sergio Romelo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kunyakua taji hilo kama nchi kamili ya Muungano wa Ujerumani Mbili ambazo zilikuwa zimetengena kwani mataji yake matatu ya awali ya mwaka 1954, 1974 na 1990 ilinyakua kama Ujerumani Magharibi
Subscribe to:
Posts (Atom)