|
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, Prof John Nkoma akifungua mkutano dhidi yao na Bloggers |
|
Maafisa wa TCRA wakiwa makini kufuatilia mkutano huo leo Mlimani City |
|
Wana Blogu wakiwa makini ni Peter Mwenda na Super D |
|
Mkongwe Beda Msimbe alikuwa makini kufuatilia mada iliyowasilishwa katika mkutano huo |
|
Wana Blogu wakifuatilia |
|
Wanahabari waandamizi wakijadiliana wakati wa mkutano huo |
|
Injinia Andrew Kasaka akiwasilisha mada ya Muongozo wa Utangazaji wa Uchaguzi |
|
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assa Mwambene akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo |
|
Assa Mwambene akizungumza na wanablogu |
|
Viongozi wa Kamati ya Muda ya Chama cha Wamiliki wa Blogu |
|
Mwenyekiti Joacquim Mushi (kati) akiwa na viongozi wenzake |
|
William Malecela mmoja wa jumbe wa Kamati ya Muda wa Wamiliki wa Blogu |
|
Mwenyekiti Mushi akizungumza na wanablogu baada ya kuteuliwa kuongoza chama hicho |
|
Wa Micharazo Mitupu naye alikuwapo kupata ujuzi zaidi |
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania, TCRA wamekutana na wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kuwapa semina juu ya misingi ya kuendesha mitandao yao kipindi cha chaguzi zijazo.
Mkutano huo wa pamoja umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya Mlimani City, ambapo Afisa Mwandamizi wa Utangazaji wa TCRA, Injinia Andrew Kasaka, aliwasilisha mada maalum.
Katika uwasilishaji wake, Injinia Kasaka alisema ni vyema wamiliki wa Blogu kuzingatia miiko, maadili ya taaluma ya habari kutokana na ukweli blogu zimekuwa na mchango mkubwa katika fani hiyo.
Aidha aliwahimiza wamiliki wa mitandao hiyo kuwa na uzalendo ili kuepusha kutumiwa na kuvuruga amani na utulivu wa nchi kama ilivyowahi kutokea katika mataifa mengine.
"Pia aliwataka wamiliki hao kusajili blogu zao ili watambulike na kuwa rahisi katika kuaminika, sambamba na kuahidi kuendesha semina zaidi mikoani katika Kanda zao za TCRA kuwapa elimu wamiliki juu ya kufahamu mipaka inayowazunguka.
"Mnapaswa kuzingatia kuandika na kuchapisha Habari zenye ukweli, zisizoumiza wengine na zenye kuchochea maendeleo ya nchi sambamba na kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha, kwa sababu blogu zina nguvu kubwa kwa sasa katika teknolojia ya Mawasiliano," alisisitiza Injinia Kasaka.
Kabla ya kuwasilishwa kwa mada, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof John Nkoma, alisema mamlaka hiyo imehitisha mkutano huo baada ya kubaini nguvu kubwa zilizopo kwa mitandao hiyo baada ya awali kufanya mkutano kama huo kwa vyomo vya habatri ya utangazaji kwa maana ya redio na televisheni.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Assa Mwambene alieleza namna ya baadhi ya mitandao ya kijamii inavyotumia uhuru uliopo kwa kujadili vitu ambavyo havijengi.
"Serikali tuliamua kuwahabarisha wananchi juu ya kuumwa kwa Rais na kwenda kutibiwa nje, lakini taarifa hii imekuwa chanzo cha mijadala isiyo na tija, kitu ambacho hakipendezi," alisema.
Aliongeza kuwa "Hatuko hapa kwa ajili ya kutaka kuwabana maana mnaweza kusema Mwambene anatoka serikalini hivyo labda ndiye niliyotoa wazo hili, hapa tunataka kusaidia kuendesha blogu zenu kwa umakini," alisema Mwambene wakati akifunga mkutano huo.
Pia alisistiza mitandao ya kijamii na wanahabari kutumia vyema uhuru wa habari kuepuka kuleta uchochezi au mambo yatakayoivuruga nchi akisema "Uhuru bila mipaka ni hatari".
Katika uchangiaji wa mada wanablogu walipendekeza kuwepo na utaratibu wa mikutano kama hiyo na elimu zaidi kwa wale ambao hawana taaluma ya habari kuepuka kuingia matatani kwa kutoa taarifa ambazo wakati mwingine huwa hazina ukweli na zinazoumiza.
Katika mkutano huo uliunda Kamati ya Muda ya Chama cha Bloggers, ambacho kinaongozwa na Mwenyekiti Joacquim Mushi, Makamu wake akiwa Francis Godwin, Katibu akiwa Khadija Kalili na wajumbe ni Aaron Msigwa, Shamim Mwasha, Henry Mdimu, William Malecela na na Othman Maulid.
Baadhi wa wajumbe walitoa maoni yao na kusema semina hiyo ni nzuri ila hawajui ni vipi imekuja wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi na siyo wakati mwingine wowote.
Hata hivyo hofu ilitolewa mapema na Prof Nkoma wakati akijibu maswali ya watu waliotaka kujua iweje kanuni hizo ziguse uchaguzi tu na kuelekeza mipaka ya blogu kufanya kazi zao.