Kenya wataendelea kubaki na taji lao la Chalenji |
BAADA ya Ethiopia kuchomoa uenyeji wa michuiano ya Kombe la Chalenji 2014 na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA kuiomba Sudan kuokoa jahazi, imethibitika safari hii haitakuwapo.
CECAFA imekwama kupata mwenyeji mpya baada ya Sudan nao kukataa ombi hilo.
Michuano hiyo ilitarajiwa kuanza
Novemba 24 hadi Desemba 9, mwaka huu huko Ethiopia bingwa mtetezi akiwa ni
Kenya.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya
Soka vya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Nicholas Musonye, alisema baada ya
Ethiopia kujitoa, imekuwa ngumu kupata nchi mbadala ya kuandaa michuano kwa
haraka.
“Hatukupenda, lakini imeshindikana
kabisa, tulifanya kila juhudi lakini mambo yamekuwa ni magumu,” alisema
Musonye.
Alisema imekuwa ngumu kupata wadhamini pia kwani waandaaji walijitoa
dakika za mwisho, hali iliyowachanganya.
No comments:
Post a Comment