Yaya Toure akiwa na tuzo ya BBC aliyotwaa mwaka jana, mwaka huu ataibuka tena kidedea? |
Yaya ambaye pia Mwanasoka Bora wa Afrika, ameteuliwa kutetea tuzo hiyo ya BBC pamoja na Emerick Aubameyang kutoka Gabon na klabu ya Borussia Dortmund, Yacine Brahimi kutoka Algeria, Vincente Enyeama wa Nigeria na Gervinho wa Ivory Coast.
Katika orodha hiyo wachezaji wanne walicheza katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazil ambapo kwa mara ya kwanza katika historia timu mbili kutoka Afrika zilifanikiwa kuvuka hatua ya makundi.
Golikipa Enyeama alicheza katika hatua ya timu 16 bora katika michuano hiyo akiwa na Nigeria wakati Brahimi naye alifikia hatua hiyo akiwa na timu yake ya taifa ya Algeria.
Yaya licha ya kutofanikiwa kuivusha nchi ya Ivory Coast hatua ya makundi ya Kombe la Dunia yeye na Gervinho wamekuwa na msimu mzuri katika vilabu vyao hivyo kuwapata nafasi ya kuwepo katika orodha hiyo.
Yaya ameisaidia City kunyakuwa taji lake la pili la Ligi Kuu katika kipindi cha miaka mitatu wakati Gervinho amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha AS Roma toka alipondoka Arsenal kwa kuifungia timu hiyo mabao 10 katika mechi 39 za Serie A.
Kwa upande wa Aubameyang pamoja na kutocheza Kombe la Dunia kwa sababu ya nchi yake ya Gabon kutofuzu michuano hiyo amewekwa katika orodha hiyo kutokana na kuwa katika kiwango kizuri katika klabu yake ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Mshindi wa tuzo hiyo natarajiwa kutangazwa Desemba mosi mwaka huu.
Make Money
No comments:
Post a Comment