STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, November 11, 2014

AFCON 2015 ipo haipo? Morocco yajivua rasmi

http://en.africatopsports.com/wp-content/uploads/2014/04/caf-logo.jpgSHIRIKISHO la Soka Afrika, CAF limetangaza kusaka mwenyeji mpya wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, baada ya nchi ya Morocco kuigomea.
CAF sasa inatarajiwa kutangaza mwenyeji mpya wa kuandaa michuano hiyo baada ya Morocco kushikilia msimamo wake wa kutoandaa kwa hofu ya Ebola.
Hata hivyo hofu imetanda kwamba huenda michuano hiyo isiwepo kabisa kwa mwaka ujao kutokana na nchi kadhaa zilizoombwa kuandaa kuchomoa.
CAF inafanya mazungumzo na nchi za Algeria, Angola, Equatorial Guinea, Ghana, Afrika Kusini na Misri, ambapo nchi za Ghana na Afrika Kusini zilishaonyesha kutokuwa tayari kubeba mzigo huo. 
Kwa hali hiyo ni kwamba hata mechi za kuwania kufuzu fainali hizo zilizosalia miongoni mwa timu zinazocheza makundi zinaweza zisiwe na maana yoyote.
Timu zinazochuana katika hatua ya makundi zilitarajiwa kushuka dimbani wikiendi hii kabla ya kumalizia mechi zao za mwisho wiki ijayo ambapo timu 15 zitafuzu kuungana na wenyeji wake.
Mpaka sasa nchi za Algeria na Cape Verde zimeshafuzu hatua hiyo baada ya kung'ara katika makundi yao kabla mechi hazijafikia tamati.

No comments:

Post a Comment