KIKOSI
cha Uruguay kimetua Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia na mshambuliaji
Luis Suarez amewasili nao akionekana kuwa fiti na tayari kuwasha moto.
Timu
hiyo ya Amerika Kusini imetua mjini Belo Horizonte jana, kwa ajili ya
maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kuwania Kombe la michuano hiyo
mikubwa zaidi duniani.
Uruguay
inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo Jumamosi
dhidi ya Costa Rica, kabla ya kumenyana na England na Italia katika
mechi nyingine za Kundi D.