'Muuaji' Giuseppe Rossi akishangilia moja ya mabao yake matatu yaliyoiangamiza Juventus |
KIBIBI cha Turin, Juventus leo imekiona cha mtema kuni baada ya kusasambuliwa mabao 4-2 ugenini na Fiorentina, licha ya kutangulia kujipatia mabao katika pambano la Ligi Kuu ya Italia Seria A.
Bao la penati la Muargentina, Carlos Tevez katika dakika ya kabla ya Paul Pogba kuongeza jingine dakika tatu baadaye yaliipa uongozi Juventus hadi wakati wa mapumziko.
Hata hivyo wenyeji waliingia kipindi cha pili na moto mkali na kurudisha bao moja ya jingine na kuongeza mengine mawili ya ushindi na kuibuka na ushindi huo mnono.
Giuseppe Rossi alipiga hat trick katika pambano hilo akianza kwa bao la penati dakika 66 kabla ya kuongeza jingine dakika 10 baadaye na kumalizia kazi dakika ya 81, ambapo kabla ya hapo Joaquim aliifunga bao la tatu dakika ya 78 na kupeleka msiba kwa Kibibi kizee.
Katika mechi nyingine genoa ikiwa nyumbani imeikwanyua Chievo mabao 2-1, Hellas Verona ilitakata kwao kwa kuilaza Parma mabao 3-2, Sampdoria iliizamisha Livorno mabao 2-1 na Sassuolo ikaizamisha Bolgna kwa magoli 2-1. Pambano jingine linalotarajiwa kucheza baadaye ni kati ya Torino na Inter Milan.