Gareth Bale alihama Spurs masimu uliopita |
WINGA machachari wa Real Madrid, Gareth Bale amezungumzia dokezo la kurejea Tottenham hapo baadaye.
Nyota
huyo aliondoka White Hart Lane msimu uliopita kwa rekodi
ya dunia ya uhamisho na ameendelea kuimarisha kiwango chake nchini
Hispania.
Lakini
licha ya kuonekana ametulia ndani ya kikosi akiwa sambamba na Cristiano
Ronaldo ndani ya Bernabeu, Bale amesema bado anaipenda Tottenham.
"Tottenham
siku zote itaendelea kuwepo ndani ya moyo wangu. Natumaini mashabiki
bado wananipenda inagawa nimeondoka," alisema wakati akiongea na BT Sport.
"Nawapenda mashabiki wa Spurs. Huwezi jua ninaweza kurejea siku moja".