Wahenga FC |
PAMBANO la kukata na mudnu kati ya mahasimu wawili wa soka la maveterani jijini Dar es Salaam, Golden Bush Veterani na Wahenga FC lililokuwa limepangwa kuchezwa kwenye uwanja wa TP Afrika, Sinza, limehamishiwa uwanja wa Kinesi, Ubungo.
Sababu za kuhamishwa kwa pambano hilo litakalofanyika siku ya Ijumaa wakati watanzania wakiadhimisha miaka 49 na Muungano, ni kutokana na uwanja huo maarufu kama 'Nangwanda Sijaona' kujaa maji ya mvua zinazoendelea kunyesha na sasa utapigwa Kinesi unaofahamika zaidi kama 'St James Park Stadium'.
Msemaji wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' alitoa taarifa hiyo ya kuhamishwa kwa pambajo hilo toka uwanja wa TP hadi Kinesi muda mchacxhe uliopita akisisitiza kuwa, wamepania kuwaumbua wapinzani wao ambao walipokutana nao mara ya mwisho waliwanyuka mabao 2-1 mbele ya kamanda Thobias Andengenye.
"Kwa wale wenye nia ya kuja kushuhudia pambano hilo la kukata na shoka wafike Kinesi, kutokana na uwanja wa awali tuliokuwa tupambane kujaa maji ya mvua," alisema Ticotico mmoja wa washumbuliaji wa timu hiyo.
Ticotico alisema mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 jioni na huenda ikachezeshwa na nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay Tembele.