Robin van Persie aibebesha Man Utd taji la 20, mpiku Suarez
Van Persie akishangilia bao lake la tatu jana usiku |
Wachezaji
wa Manchester United wakishangilisi ushindi wao jana baada ya kuinyuka
Aston Villa mabao 3-0 na kutwaa ubingwa wa 20 wa Ligi Kuu ya England |
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uholanzi, Robin van Persie jana usiku aliwezesha klabu yake ya Manchester United kutwaa taji la 20 la Ligi Kuu ya England, huku mwenyewe akiondoa 'gundu' na kumpikua Luis Suarez katika orodha ya wafungaji.
Mkali huyo alifunga mabao yote matatu yaliyoizamisha Aston Villa kwenye uwanja wa Old Trafford kwa kipigo cha mabao 3-0.
Van Persie aliyafunga mabao hayo katika dakika 33 tu ya pambano hilo na kuihakikisha Man United kuivua taji mahasimu wao Manchester City, huku akikwea kwenye kilele cha wafungaji akimzidi Suarez kwa bao moja zaidi akiwa na mabao 24.
Mholanzi huyo ambaye alikuwa na Arsenal kwa misimu kadhaa bila kuonja ladha ya kutwaa taji lolote, alianza makeke yake dakika ya pili ya mchezo huo akimalizia pasi ya Ryan Giggs.
Van Persie aliongeza bao la pili dakika ya 13 akimalizia kazi ya Wayne Rooney aliyekuwa akicheza mechi yake ya 400 akiwa na Man United kabla ya kumalizia udhia kwa kufunga bao la tatu dakiika ya 33 akiwezeshwa tena na Giggs.
Man United imetwaa taji hilo la 20 na kupikua rekodi ya Liverpool waliowakamata mwaka jana kwa kulingana nao kutwa aubingwa mara 19 wakiwa bado wamesaliwa na mechi nne mkononi.
No comments:
Post a Comment