Bale akipambana mbele ya vijana wa Real Sociedad |
Moyes aliyeiongoza Sociaded kuilaza Barcelona bila kutarajiwa hivi karibuni alishuhudia vijana wake wakipotea Bernabeu licha ya kutangulia kufunga la mapema dakika ya kwanza tu tangu kuanza kwa mchezo huo.
Aritz Elustondo aliiandikia wageni bao dakika ya kwanza akimalizia kazi nzuri ya Rubén Pardo kabla ya James 'Bond' Rodríguez kulisawazisha dakika mbili baadaye akimlazia kazi ya Marcelo.
Beki mfungaji wa Real Madrid, Sergio Ramos aliionmgeza timu yake bao la pili dakika ya 37 na kudumu hadi mapumziko wenyeji wakiwa mbele kwa mabaoi 2-1.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema aliwapa furaha mashabiki wa Real Madrid ambao walimkosa nahidha wao, Cristiano Ronaldo anayetumikia adhabu ya kandi nyekundu aliyopata katika mechi hiyo iliyopita kufanya undava uwanjani aliingozea timu hiyo bao la tatu dakika ya 52 akiunganisha krosi ya Gareth Bale.
Benzema alirudi tena kambani dakika ya 76 akifunga bao la nne na kuifanya Real Madrid kuzidi kujikuta kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 20, pointi nne zaidi ya wanaowafukuzia Barcelona wanaocheza leo na Atletico Madrid walioshinda jana ugenini kwa mabao 3-1.
Matokeo mengine ya mechi hiyo, Rayo Vallecano ilikubali kichapo nyumbani cha mabao 2-1 mbele ya wageni wa Deportivo La Coruna, Atletico Madrid wakishinda ugenini mabao 3-1 dhidi ya Eibar, Granada wakishinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Elche na Celta Vigo wakiilaza Cordoba kwa bao 1-0.
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa michezo ifuatayo;
Levante vs Athletic Bilbao (saa 8 mchana)
Almería vs Getafe (saa 1 usiku)
Sevilla vs Espanyol (saa 3 usiku)
Barcelona vs Villarreal (saa 5 usiku)