STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 11, 2015

Azam yaifumua Mtibwa Sugar 5-2 warudi kileleni

KLABU ya Azam wamerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifumua bila huruma Mtibwa Sugar kwa mabao 5-2.
Azam ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wealipata ushindi huo mnono na wa kwanza kushuhudiwa katika mechi za ligi msimu huu katika pambano pekee lililochezwa kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Frank Domayo 'Chumvi' alifunga mabao mawili moja kila kipindi sawa na alivyofanya Kipre Tchetche na Didier Kavumbagu alifunga moja kuiangamiza Mtibwa ambao hicho ni kipigo chao cha pili mfululizo.
Mtibwa walioanza msimu huu kwa mkwara na kuongoza ligi hiyo kwa muda mrefu kabla ya kuporomoka mara baada ya kurejea kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ilifunikwa eneo la kiungo na Azam.
Vijana hao wa Mecky Mexime walipata mabao yao ya kufutia machozi kupitia kwa Juma Nampaka na Ame Ali ambayo hata hivyo hayakusaidia Wakata Miwa hao kufurukuta mbele ya mabingwa watetezi hao.
Kwa ushindi huo umeifanya Azam kurejea tena kileleni wakifungana pointi 25 sawa na Yanga, lakini tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa yanawapa nafasi ya kukalia kiti cha uongozi.
Mtibwa wenyewe wameendelea kusalia katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 18 sawa na ilizonazo timu za Kagera Sugar na Coastal Union.
Yanga na Azam zinazochuana kieleleni mwishoni mwa wiki zitakuwa kwenye majukumu ya kimataifa wakati Yanga itaikaribisha BDF XI ya Bostwana na wenzao Azam wataumana na El Merreikh wanaotarajiwa kutua nchini kesho tayari kwa pambano hilo litakalochezwa Jumapili.
Pambano la Yanga litacheza Jumamosi na viingilio vimeshjatangazwa kwa kiingilio cha chini kikiwa ni Sh 5000 tu.
Wakati lile la Yanga kiingilio cha chini kabisa ni Sh 2000 na vingine ni VIPB Sh 5000 na VIP A 10000 na tyiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa.

Mourinho amchongea Van Persie kwa FA

MENEJA wa vinara wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekishambulia Chama cha Soka cha Uingereza(FA) kwa kuamua kutochukua hatua yeyote kwa mshambuliaji wa Manchester United, Robin Van Persie kwa tuhuma za kumtwanga kiwiko mchezaji wa upinzani.
Van Persie alionekana akimpiga kiwiko James Tomkins wakati wa mchezo ambao United ilitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya West Ham United Jumapili iliyopita lakini mwamuzi Mark Clattenburg hakuona tukio hilo huku FA nao wakilifumbia macho.
Uamuzi huo unamfanya Mourinho kutowaelewa FA kwani anatarajiwa kumkosa nyota wake Diego Costa katika mchezo wa leo dhidi ya Everton baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania kufungiwa mechi tatu kwa kukutwa na hatia ya kumkanyaga kwa makusudi Emre Can mwezi uliopita.
Akihojiwa Mourinho amesema watu haohao ambao wamemfungia mchezaji wake Costa ndio hao ambao hawataki kumfungia Van Persie kwa kosa lake alilofanya.
Mourinho aliendelea kudai kuwa anajua kama angekuwa mchezaji wake lazima angefungiwa kwani tukio kama hilo lilimtokea Ramires na alilimwa adhabu.

Sanchez, Ramsey wazua hofu Arsenal

http://www3.pictures.zimbio.com/gi/Aaron+Ramsey+Alexis+Sanchez+Leicester+City+N8Hb6G9P6Rgl.jpg
Ramsey, Sanchez



KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ana wasiwasi kuhusu hali za nyota wake Alex Sanchez na Aaron Ramsey baada ya kupata majeruhi katika mchezo Ligi Kuu walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Leicester City.
Ramsey alitolewa nje ikiwa ni dakika tisa tu toka aingie akitokea benchi katika kipindi cha pili baada ya kupata majeruhi ya msuli wa paja, huku winga wa kimataifa wa Chile, Sanchez yeye alitolewa nje kufuatia kuchezewa faulo na Matthew Upson ambayo ilimfanya kushindwa kuendelea na mchezo huo uliochezwa Emirates.
Wenger amesema ana wasiwasi na nyota wake hao kwani hana uhakika watakaa nje ya uwanja kwa kipindi gani wakijiuguza. Mabao yaliyofungwa na Laurent Koscielny na Theo Walcott yalitosha kuwapa Arsenal ushindi huo muhimu baada ya kuchapwa na  Tottenham Hospur
Mabao yaliyofungwa na Laurent Koscielny na Theo Walcott yalitosha kuwapa Arsenal ushindi huo muhimu baada ya kuchapwa na mahasimu wao Tottenham Hotspurs mwishoni mwa wiki iliyopita.